Ertugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 14,705
- 30,041
Tabia yoyote hapa duniani hutengenezwa au watu hujifunza na mwisho wa siku ndio inakuwa sehemu ya maisha yao ya kila siku.
Leo ningependa kuzungumzia kuhusiana na kujenga tabia ya kuweka akiba hata kwa kiasi kidogo sana cha buku mbili tu kwa mwezi ( 2,000/=)
Tukiwa na tabia ya kuweka akiba basi baada ya muda fulani kuweka akiba ndio itakuwa sehemu ya maisha yetu,nimekushauri kuanza na hiyo buku mbili kwakuwa kuna watu ambao ni kweli kipato chao ni kidogo sana,yani akipokea kama ni mshahar basi unakutana na mambo kibao na mwisho wa siku hakuna kinachobakia.
Sasa mtu kama wewe anzia na buku mbili ndani ya mwezi mmoja hiyo ni 2,000 ,baaada ya miezi mitatu au minne hutozungumzia tena hiyo 2,000 ila itakuwa elfu kadhaa,je hapo ukiwa mwenye nidhamu nzuri ya pesa,hiyo pesa haitakuwa imekusaidia wakati wa changamoto fulani fulani,kwa mtindo wako wa zamani wa kutoweka akiba ungepaswa kwenda kukopa ili utatue changamoto yako lakini kwakuwa now una kiakiba chako basi unaitatua pasina kwenda kukopa tena.
Siku zote kuanza kitu ndio huwa changamoto lakini ukishakianza tu basi inakuwa ni mseleleko tu,huwa tuna kawaida ya kusema mwezi ujao nitaweka akiba lakini ukifika huweki akiba,unajikuta umeanzisha tabia nyengine ya kuahirisha mambo,na ndio inakuwa tabia yako.
Sasa ndugu yangu wewe uliye bahatika kusoma uzi huu,ebu kwa nia ya dhati kabisa tuanze sote kuweka akiba mwisho wa mwezi wa July hata kwa buku mbili tu,kumbuka hapa tunaanza kujifunza tabia mpya ambayo huenda hatukuipa umakini au umuhimu lakini trust me baada ya muda fulani utakuja kunishukuru hata ndani ya moyo wako.
Inasemwa tatizo sio unaingiza kiasi gani ila ishu hapa je huwa unaweka kiasi gani au huwa unabakia na kiasi gani,ukishaanza hii tabia ya kusave na akiba yako kuongezeka utafurahia juhudi yako unayoifanya na soon utaanza kuyaepuka mambo yote ambayo yanatumia hela yako kijingajinga.
Kumbuka hata mwendo wa kilomita 1,000 ulianza na hatua moja,idadi ya hatua zako kwa muda fulani zitakufisha kwenye umbali wa kilomita 1,000.
Ni hayo tu!