Tubadili majina ya Daraja la Mfugale na Kijazi

Mbona hili JPM aliishalimaliza hilo? Alisema kwamba, yeye ameyaita hivyo kwa mamlaka aliyokuwa nayo. Ikitokea Rais mwingine akaja na akaamua kuyabadilisha, sawa. Kwahiyo, wewe endeleza ushawishi, JPM aliishamaliza mwendo wake!
Alikuwa na mambo ya kishamba na ulimbuken mkubwa sana hao jamaa zake hawakuwa na hadhi yeyote ya kuwekwa majina yao huko.
 
Tutabadilisha upuuzi huu na puuzi nyingi nyingine, ni suala la muda tu.
 
Acheni chuki zenu, tuongee mambo mengine ya maendeleotuache kubishana majina ya watu walioitumikia nchi na kuleta maendeeo
 
Kwa sababu wakati wa kuyaweka hamna aliyehitaji wazo la wana JF naamini kama kuna sababu ya kuyatoa halitatoka kwenye baraza hili pia. Kuna watu wanataka kumwingiza Mama chaka wakidhani yeye hajui kuwa aliyemtangulia alikuwa na base ya watu ambayo bado inamuenzi. Na ni ile iliyokuwa inatandika kanga barabarani wakati akipitishwa na kuvunja uzio wa Airport.
 
Kabisa, kuto kuleta fujo

Kijazi irudishwe Ubungo Interchange

Na mfugale irudie Tazara flyover
Mungu Fundi sana. Wameng'ang'ania kujipa majina ya miundombinu na COVID19 imewang'oa wote kuanzia Magufuli, Mfugale na Kijazi
 
Naunga mkono hoja
 
Mungu Fundi sana. Wameng'ang'ania kujipa majina ya miundombinu na COVID19 imewang'oa wote kuanzia Magufuli, Mfugale na Kijazi
Kwani kuita majina ya viongozi kumeanza kipindi cha Magufuli? Mbona mnakuwa na unaa wa kijinga hivi! Hizo barabara zimeitwa hadi majina ya watu wa nje huko, maeneo kibao yameitwa kwa kumbukumbu za watu, inakuwaje leo wao wakiendeleza huo utamaduni mnawananga!
 
Majina mengi yametoka baada ya wenyewe kufariki. Mengine yamekuwa yanatolewa na Mamlaka za Miji na Majiji lakini siyo hawa washirika wa Rushwa watatu toka Wizara ya Ujenzi/ TANROADS miaka 20 iliyopita. Wanapeana majina wenyewe kwa wenyewe
 
Waswahili kwa kujitoa ufahamu mnaongoza.
 
Aisee MUNGU fundi sana!
Yaani majamaa yangeendelea kuishi kila kitu kingeishia kuwa Magufuli, Mfugale, Kijazi.
Pengine hata majina ya koo tungelazimishwa kubadili!
Tanzania bila shaka ingeitwa Chatonia!

NB: Lakini yale majamaa yalielewana sana!
 
Wewe ni nani sasa mpaka ubadili alichopanga mpendwa wetu Magufuli.. kwanini hukusema akiwa hai kama wewe kweli upo straight[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
huwezi kujenga nchi kwa kubadili badili majina kila mara baada ya watu kufariki. Ukianza hivyo, nchi haitakuwa na ramani ya kueleweka kwani kila atakayekuja madarakani atakuwa anabadili majina kuendana na utashi wake hivyo ramani mpya kuchorwa kila baada ya miaka kumi.

Kwa chuki yako dhidi ya Magufuli, huenda ukataka hata sheria zote alizosaini akiwa madarakani zifutwe; na huo utakuwa ndio mwanzo wa banana republic.
 
Pia tuite MBEZI BUS TERMINAL siyo ......... ...
 
Haya yote ni mazao ya mshamba yule. MAJINA haya km yataendelea kubaki yatabaki kuwa kumbukumbu mbaya sana ya madhila makubwa yaliyofanywa na utawala ule.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…