Tuchangiane uzoefu katika malezi: Malezi yako yalikuwaje, unahisi yamekuathiri, ungependa kulea watoto wako kama ulivyolelewa?

hahahahahahah mkuu hapo kwenye mwanamke akipita mbele yako hapo

asante kwa ufafanuzi mkuu mi sina mengi ya kusema hapo kwenye kurithi maana najua machache sana kuhusiana na hilo
 
Asante sana mkuu BenKaile umetoa ufafanuzi mzuri sana juu ya vitu vinavyoathiri malezi

lakini mkuu back to you,wewe binafsi na utu wako unadhaani unatokana na malezi uliyopewa na wazazi wako au unadhani ni vile tu jinsi ulivyo? unadhani malezi uliyopewa yamekuathiri kwa namna moja ama nyingi eiza hasi au chanya? ungependa kulea watoto wako kama ulivyolelewa?
 
oh asante pia kwa hapa nimekuuliza swali ambalo hapa umetoa majibu yake japo nusu sikuwa nimeona mkuu

ila swali kwako mkuu,kwa nini usingependa kulea watoto wako kama vile ulivyolelewa? ni kwa mantiki kwamba ulilelewa kufuata na nyakati zile?unahisi kuna vitu umekuwa na huvipendi na ni kwa sababu ya malezi au ni nini hasa chanzo?
 
Nachukua strengths ktk malezi yangu ya utoto naachana weakness. Binafsi hii ni kipindi cha kusahihisha makosa na kujenga kizazi bora zaidi cha baadae.
sure sure mkuu umejibu vyema kabisa kuhsua kuacha gaps na kuchukua mazuri

but mami unahisi utu ulionao sasa ni matunda ya malezi uliyoyapata? umewahi kuona jirani au Rafiki au mtu yeyote yule ambaye malezi yamempa utu wa ain Fulani utusimulie kisa hicho ili tuzidi kujifunza hata Zaidi?
 
Mkuu BAK madini yako yana umuhimu sana katika hii mada tafahdali tia neno

nakusubiria hapa hapa
 
Reactions: BAK
https://jamii.app/JFUserGuide you baba.... https://jamii.app/JFUserGuide youuuu..mpaka leo unanifanya ni hishi kwa shida tu uka mwacha mama. ukaweka malaya mmoja tena kwenye jasho la. familia na nakupa taharifa kihama chako kinakuja mda si mrefu.....niacheni kwanza maana namengi yakuandika apa maana kurasa azitoshi
 
Mi ninaamini kua asilimia kubwa kwa WaTz tumepitia malezi ya kibabe na nidhamu ya woga ikiwemo na mm mwenyewe "obey the last order ". Ila malez sahihi kwangu ni urafiki na ukaribu baina ya mzazi/mlez na watoto wake. Nimekua nikipokea ushaur ktoka kwa boy of 3 age hasa kw mambo yamhusuyo mwenyewe. Inansaidia sn kubaini mambo yake na mawazo yake yooote. Hop itatupeleka pazur
 
Viroboto , chawa- nguoni na kichwani, kunguni, utitiri, mbu, Vyoote mimi. kuosha vyombo, kuteka maji kisimani! Kutengwa wakati wa sala! yaani......

Binafsi nilijitenga na wenzangu shuleni sababu kaptula ya shule ilichanika matundu makubwa matakoni tena bila chupi ndani,

Manake nilichekwa na watoto wenzangu, na kuonekana kituko, kuchunga ng'ombe mbugani pekupeku siku za likizo, ndo zilikuwa zangu.sikujua viatu.

kujisaidia ni vichakani tu sometimes unaona kabisaaa minyoo juu ya kinyesi chako, sababu ya utoto unaona kawaida. hkn pa kusemea!

Bora niende Shule nitii sheria za shule ili nikae salama kunako kivulini cha drs, na mwalimu kuliko kubaki nyumbani nikalime shamba asubuhi then nikachunge mifugo siku nzima,
ambayo haikuwa na tija kwangu mfano kwa kunywa maziwa , hata kununuliwa shati au kaptula ya kuchungia.

Kusema kweli bila kuficha kila, usiku, ulipokuwa ukiingia Roho inauma sana, juu ya utitiri, chawa na viroboto vitakavyo ning'ata usiku kucha,

Nguo pekee ya kuchungia; Shukrani, ilikuwa ni sweta la kijani lililo sheheni chawa, tena bila vishikizo alinipatia marehemu dada yangu,
nalo lili nasa miiba ya porini kibao, kishikizo pekee kilikuwa mkono wangu wa kushoto. na ule wa kulia nilishika fimbo ya kuswagia mifugo. ngozi ya tumbo ilibadilika ajili ya ukurutu! mchana wadudu hawaumi sana km usiku!

Miaka hiyo Hakuna majira niliyo furahia km Asubuhi ikianza na mchana, jioni ilikuwa simanzi sana. sikutarajia kuijua key board. at the age of 8-9 yrs, nikaanza fanya vibarua kwa kificho ili nipate hela!

But all in all niliona ni sehemu tu ya kawaida kimaisha!

Bahati sana, bila kutegemea, nikafaulu kwenda Sec. huko baba mkuu Akili ndo ilifunguka paaa! nikaona km Ulaya nilivo heshimiwa, na walimu, wanafunzi.

Dawati, kitanda, ni vya peke yako, chakula kizuri nabembelezwa kula kwa mara ya kwanza eti nisigomee chakula! duuu!, mimi huyu! .....mngejua!

Ktk yale maisha yangu. ilikuwa ni kawaida kula ugali mgumu wa mtama, na mboga za majani chukuchuku daily, wali mkavu kwa nadra sana,
but Sec. duuu! Wali nyama Maharagwe, ndizi, mbatata, tena umeungwa vizuri na mafuta, maarufu km wese!.

Na kweli ya Mungu kadri nilivo panda Madarasa mfululizo. Mpaka kupata kazi, nilipendwa na kuheshimiwa sana na wanafunzi pamoja na wafanya kazi wenzangu,

pia jamii za watu niliokutana nao, tena mno! kuliko nilikotoka. mfano nilipoenda semina kwa mara ya kwanza Bagamoyo, sikuamini niliyotendewa seminani! na posho juu!

Hakika ya Mungu sikurudi tena kwa Shangazi yangu hata likizo tu, mpaka amekufa, wala sikumpenda kiviiile japo sikuonyesha chuki! Mpaka leo nikioa mwanamke ana tabia za ki-shangazi yangu, ananikata steam palepale!

Alikuwa hachapii wala kukufokea, but her facial expression spoke thousands of words, she really, and completely abandoned me like no body business, funny enough, and shamelessly, she did it to me, at that early age! very bad!
I dare say she was really evil. she deserve to drove to the pit of Hell!

Mpaka leo sijawahi ishi maisha ya hovyo, yaliyo jaa udhariri, Concealed hope, dharau, kejeli, umaskini, ujinga, Ubaguzi km yale, May God forbid!

MTOTO NI MAMA YAKE MZAZI TU, NDIYO ATAKUWA MTU BORA KATI YA WATU BORA, KINA DADA BEBENI WATOTO WENU WENYEWE,HATA KM HUNA HELA!
WATOTO WANGU NIKIKOSANA NA MAMA YAO. NI BORA WAKAE NA MAMA YAO TU! NITATOA MATUNZO PALE INAPO BIDI!
 
Wale tuliolelewa kama maiti au kama tuliovamia dunia vile tunacomment wapi? Fuc.k my parents. Wengine tuko duniani kuwasindikiza wenzetu shit!
 
Wale tuliolelewa kama maiti au kama tuliovamia dunia vile tunacomment wapi? Fuc.k my parents. Wengine tuko duniani kuwasindikiza wenzetu shit!
Duh mkuu sina chakusema zaidi ya Mungu akukumbuke na akumulikie nuru ya uso wake....
 
Ni kweli mtoto umleavyo ndivyo akuavyo...

Nashukuru Mungu wazazi wangu wamenipatia malezi bora sana, ambayo sina cha kujutia...



Cc: mahondaw
 

wow umeongea kitu chenye ukweli mkubwa sana kiongozi,sasa labda utuambie ni kwa jinsi gani ulliweza kuibadilisha akili yako kutoka kwenye malezi uliyopewa mpaka hayo unayowapa watoto wako sasa?maanake tulio wengi tunaathiriwa yaani yale malezi tuliyopewa tunataka kuwapa watoto wetu hayo pia.
 
Wale tuliolelewa kama maiti au kama tuliovamia dunia vile tunacomment wapi? Fuc.k my parents. Wengine tuko duniani kuwasindikiza wenzetu shit!
Dah kiongozi hii ni serious sana aisee,unaweza kushare na sis nini kilitokea? kwa sababu hili ni jambo zito mnoo hasa hapo kwenye ....my parents,ujue bado wao ni wazazi wako na huwezi kulibadili hilo,ndio waliokuleta duniani wangeweza kukuua ikiwa wangetaka lakini hawakufanya hivyo,huoni kama umekasirika mnooo kiongozi?
 
Dah umepitia mengi sana na ya kuhuzunisha mkuu,pole mnoooo,lakini hongera pia kwa kuviruka viunzi vyote hivyo na sasa umedhililisha ubora wako,unahisi malezi yale yaliathiri utu wako ambao labda kuna vitu unastruggle navyo mpaka leo,kwa sababu ya malezi uliyoyapitia?
 
Ndio...natamani saana kulea kama nilivolelewa mimi na zaidi (nililelewa vema)

Malezi niliolelewa yamenijenga kua mtu mpole,mcheshi...nisiehukumu watu,na mwelewa na ambaye ninaweza kuishi na kila mtu (mtu wa aina yeyote)
Tunatamani kufahamu zaidi, tudadavulie kwa mifano ya hapa na pale
 
Akhsante sana Mkuu! ajabu ni kuwa wakt ule wa utoto sikuona Mateso ki viile! nilijionea kawaida tu! kwanza hata sikuwahi kuwaza kuna maisha bora, ya kupata kazi! sikuwahi kufikiri kuna ku pass mitihani huko juu! siku ya kwanza ku-pass vizuri nilikuwa naambiwa tu na watu umefanya vizuri endelea ivo!

nilisoma tu shule! kwa sababu ilikuwa ni mahali tulivu, ile tu kukaa drsani kivulini, nilihusudu mnoo! kuliko juani , nikichunga ng'ombe, ambao hawakunipa faida yeyote!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…