Viroboto , chawa- nguoni na kichwani, kunguni, utitiri, mbu, Vyoote mimi. kuosha vyombo, kuteka maji kisimani! Kutengwa wakati wa sala! yaani......
Binafsi nilijitenga na wenzangu shuleni sababu kaptula ya shule ilichanika matundu makubwa matakoni tena bila chupi ndani,
Manake nilichekwa na watoto wenzangu, na kuonekana kituko, kuchunga ng'ombe mbugani pekupeku siku za likizo, ndo zilikuwa zangu.sikujua viatu.
kujisaidia ni vichakani tu sometimes unaona kabisaaa minyoo juu ya kinyesi chako, sababu ya utoto unaona kawaida. hkn pa kusemea!
Bora niende Shule nitii sheria za shule ili nikae salama kunako kivulini cha drs, na mwalimu kuliko kubaki nyumbani nikalime shamba asubuhi then nikachunge mifugo siku nzima,
ambayo haikuwa na tija kwangu mfano kwa kunywa maziwa , hata kununuliwa shati au kaptula ya kuchungia.
Kusema kweli bila kuficha kila, usiku, ulipokuwa ukiingia Roho inauma sana, juu ya utitiri, chawa na viroboto vitakavyo ning'ata usiku kucha,
Nguo pekee ya kuchungia; Shukrani, ilikuwa ni sweta la kijani lililo sheheni chawa, tena bila vishikizo alinipatia marehemu dada yangu,
nalo lili nasa miiba ya porini kibao, kishikizo pekee kilikuwa mkono wangu wa kushoto. na ule wa kulia nilishika fimbo ya kuswagia mifugo. ngozi ya tumbo ilibadilika ajili ya ukurutu! mchana wadudu hawaumi sana km usiku!
Miaka hiyo Hakuna majira niliyo furahia km Asubuhi ikianza na mchana, jioni ilikuwa simanzi sana. sikutarajia kuijua key board. at the age of 8-9 yrs, nikaanza fanya vibarua kwa kificho ili nipate hela!
But all in all niliona ni sehemu tu ya kawaida kimaisha!
Bahati sana, bila kutegemea, nikafaulu kwenda Sec. huko baba mkuu Akili ndo ilifunguka paaa! nikaona km Ulaya nilivo heshimiwa, na walimu, wanafunzi.
Dawati, kitanda, ni vya peke yako, chakula kizuri nabembelezwa kula kwa mara ya kwanza eti nisigomee chakula! duuu!, mimi huyu! .....mngejua!
Ktk yale maisha yangu. ilikuwa ni kawaida kula ugali mgumu wa mtama, na mboga za majani chukuchuku daily, wali mkavu kwa nadra sana,
but Sec. duuu! Wali nyama Maharagwe, ndizi, mbatata, tena umeungwa vizuri na mafuta, maarufu km wese!.
Na kweli ya Mungu kadri nilivo panda Madarasa mfululizo. Mpaka kupata kazi, nilipendwa na kuheshimiwa sana na wanafunzi pamoja na wafanya kazi wenzangu,
pia jamii za watu niliokutana nao, tena mno! kuliko nilikotoka. mfano nilipoenda semina kwa mara ya kwanza Bagamoyo, sikuamini niliyotendewa seminani! na posho juu!
Hakika ya Mungu sikurudi tena kwa Shangazi yangu hata likizo tu, mpaka amekufa, wala sikumpenda kiviiile japo sikuonyesha chuki! Mpaka leo nikioa mwanamke ana tabia za ki-shangazi yangu, ananikata steam palepale!
Alikuwa hachapii wala kukufokea, but her facial expression spoke thousands of words, she really, and completely abandoned me like no body business, funny enough, and shamelessly, she did it to me, at that early age! very bad!
I dare say she was really evil. she deserve to drove to the pit of Hell!
Mpaka leo sijawahi ishi maisha ya hovyo, yaliyo jaa udhariri, Concealed hope, dharau, kejeli, umaskini, ujinga, Ubaguzi km yale, May God forbid!
MTOTO NI MAMA YAKE MZAZI TU, NDIYO ATAKUWA MTU BORA KATI YA WATU BORA, KINA DADA BEBENI WATOTO WENU WENYEWE,HATA KM HUNA HELA!
WATOTO WANGU NIKIKOSANA NA MAMA YAO. NI BORA WAKAE NA MAMA YAO TU! NITATOA MATUNZO PALE INAPO BIDI!