Tuchukue tahadhari sana Corona sasa ipo DRC congo!

Tuchukue tahadhari sana Corona sasa ipo DRC congo!

Hizo akili timamu kweli unazo mkuu? Ndiyo zimekutuma kuomba majanga?
 
DRC katoka ku eradicate ebola last week, leo anko Corona katua

Sent from ONEPLUS 5T using Tapatalk
 
Sasa hao DRC nao wajinga wanaona fahali kumtangaza mweupe 1 kuwa amepata corona badala ya kumuamliza huko juu kwa juu
 
Kila taifa ilipaswa kufunga boda zake zote kwa muda na huu ugonjwa unasambaa kwa ajil ya muingiliano wa watu

Kuliko kosewa Ni kuruhusu muingiliano kutoka China kwenda mataifa mengne ili paswa ilivyogundulika tu ilipaswa waliokuwa China wabaki huko huko tu kusiwe na muingiliano wowote

kilicho akilini kitumie
 
Hli gonjwa mpaka sasa halijaua mtu mweusi nafikiri kuna adaptive cell ama race inafuata
 
Hili Likorona lilikua la kuhujumiana wao kwa wao, ndio maana linaenea kwa Wazungu, Waarabu na Wachina. Naona Mrusi halijambishia hodi, au atakua yeye ndio mpishi wa haya mambo.
Russia mbona sijapokea taarifa zake
Russia wamekuwa nayo kwa muda sasa ila haisambai haraka, sasa wanawatu 10 waliowahi kudhurika.

Screenshot_2020-03-10 Coronavirus COVID-19 (2019-nCoV).png

Center for Systems Science and Engineering (CSSE)
 
Russia wamekuwa nayo kwa muda sasa ila haisambai haraka, sasa wanawatu 10 waliowahi kudhurika.

View attachment 1383769
Center for Systems Science and Engineering (CSSE)

Duh Noana hata Australia na Wahindi pia, sema hao hawapigi makelele sana kama Marekani na Uropa. Afrika yetu jameni tuendelee maombi tu maana hiki kitu kinatesa mataifa yenye teknolojia zote, sasa sisi na misongamano yetu kwenye madaladala tutaisha.
 
Russia watayari wana wagonjwa karibia kumi, sema Korea kaskazini kwa mzee Kiduku ndio sijasikia hata mmoja.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kiduku atakua ametoa maagizo waliwe shaba, ukigundulika nacho unaliwa ya kichwani, yule hapendi kucheleweshwa na vitu vidogo vidogo wakati anawaza kuzindua manyuklia.

Inawezekana katoa agizo pia kwamba ukitoa taarifa za uwepo wa Corona kwake, na wewe pia inakula kwako.
 
Coronavirus: Congo DRC yathibitisha kisa cha kwanza cha virusi vya Corona

Mhudumu wa afya


Haki miliki ya pichaREUTERS

Kisa cha kwanza cha virusi vya Corona kimethibitishwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Msemaji wa wizara ya Afya amesema Jumanne.

Mgonjwa huyo ni Mkongo wa miaka 52 aliye na kibali cha kuishi Ufaransa, ambaye aliingia nchini humo siku mbili zilizopita na alikuwa amewekwa karantini baada ya uchunguzi aliofanywa katika uwanja wa ndege wa Kinshasa kubaini kuwa ameambukizwa virusi hivyo.

Alikuwa akipewa matibabu katika kituo cha zamani cha kuwatibu wagonjwa wa Ebola mashariki mwa mji mkuu wa Kinshasa.

Wizara ya afya ya DRC imesema kuwa inajaribu kwatafuta watu wengine waliyesafiri na mgonjwa huyo ili wawekwe karantini katika juhudi za kudhibiti maambukizi.

Waziri wa afya Eteni Longondo ametoa wito utulivu na kuzingatia usafi kwa kuosha mikono yao mara kwa mara.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni nchi ya 11 ya Afrika kuthibitisha maambukizi ya ugonjwa hatari wa Covid-19.

Ugonjwa huo ambao ulianzia China umewauazaidi ya watu 3 800. DR Congo kwa sasa imeimarisha uchunguzi katika viwanja vyake vinne vikuu vya ndege kwa kuwakagua kwa makini wasafiri walio na viwango vya juu vya joto- hatua ambayo imekuwa ikichukuliwa kama sehemu ya kupambana na maaambukizi ya virusi hatari vya Ebola.
 
Back
Top Bottom