Tucopy na kupaste sample ya IGA ya UK (Muingereza) na UAE (Mwarabu) katika uwekezaji, japo ni ya mwaka 1992, lakini inafundisha uzalendo kwa nchi zao

Una complicate mambo sana.

Mleta mada: umeandika tuige sheria IGA (which is BIT) ya uingereza.
Mchangiaji: nimekueleza hiyo BIT ya uingereza na IGA ya Tanzania hazina tofauti na misingi ya zote mbili VCLT 1969. Tofauti ya BIT na IGA are the former is generic, whereas the latter is specific to a project.

Mleta mada: umesema BIT ya uingereza ina muda wa miaka 10.
Mchangiaji: nimekueleza japo hiyo BIT ina miaka 10. Lakini investment zitakazoingiwa sheria hiyo hiyo bado ni enforceable kwa 20 baadae toka kuisha kwake kwa mikitaba iliyoingiwa.

Mchangiaji: baada ya miaka 20 kutakuwa na negotiations nyingine kama kuna investments zina endelea ambapo BIT aitakuwa na nguvu as an ‘implied term’ ya mkataba (that’s the whole purposes ya sheria yeyote kwenye mkataba).

Mchangiaji: nini kitatokea pasipo na BIT wanasheria makini watatumia kanuni za law of contract ku draft terms za kuendeleza hiyo mikataba ambapo swala la usuluhishi wa migogoro watahakikisha ni neutral venue kama ilivyo kwenye BIT/IGA yeyote. Na kutakuwa na kipengele kinachoelezea mkataba unavyoweza kuisha nikakutajia na namna tatu ambazo ni completetion of performance, a frustrating event and a serious breach (sasa kuna mambo mengi hapo ya kimazingira kwenye kila aspect).

But then yote hayo yapo pia kwenye IGA ya Tanzania yameandikwa tofauti tu.

Mikataba ya biashara rules zake ni principle za contract law; ata hizo sheria zina codify tu principles ambazo nyingi vyanzo vyake ni case laws za uingereza (mostly) na marekani (in small instances).
 
Nielimishe,IGA ina tofauti gani na contract? Na kwa nini makubaliano yalipelekwa bungeni yanakuwa sheria au inakuwaje?
 
Nielimishe,IGA ina tofauti gani na contract? Na kwa nini makubaliano yalipelekwa bungeni yanakuwa sheria au inakuwaje?
IGA = Treaty

IGA sio contract it’s an agreement

Contract has ‘consideration’ (value of exchange), IGA doesn’t have consideration so it can’t be a contract on its own.

A treaty needs to be ratified under VCLT 1969 if its to become valid.

By ratifying a treaty inakuwa sheria ya nchi kwa jambo husika (enforceable), not on its own though; bali unapoingia mikataba ya kibiashara baadae.

Kilichomo kwenye IGA (kwa sababu ni sheria, after ratification) kinakuwa ni aspects za ‘implied term’ kwenye mkataba itakayoingiwa mbeleni (otherwise IGA on its own is useless).

Kingine muhimu kwenye hiyo mikataba ya baadae ni consideration terms za kwenye concession agreement mtakazokubaliana huko mbele ambacho hakipo kwenye IGA (actually consideration ndio sababu kubwa ya migogoro).
 
walimu wana kazi sana
nashindwa hata nikusaidie nini,una mambo mengi, nadhani pia hujui unataka nini kwenye maswali yako, okay mwanzano nilikujibu kuhusu vclt, 1969 kuwa sio specific law to investment law, coz basement yake ni recognition of international jcontracts,

tofauti ya IGA na BIT unayotaka kuileta nadhani pia hujui, pengine ni lugha au kutokujua, those terms are used interchangeably, shortly, IGA= (Inter-governmental), inter ni prefix yenye maana ya between, kwa sababu neno linalofuata ni government, it means between two government, na agreement ( ambayo wengi mnachanganya na kudanganya watu, ni makubaliano, hapana ni mkataba, = kwa hiyo ni mkataba baina ya nchi mbili.

neno Bilateral (Bi-lateral), etymologically is from latin lingua, bi-means two, na lateral (two sides), na treaty (means agreement), kwa hiyo literally iko translated as agreement between two sides.

hizo terms zote katika sheria za mkataba wa kimataifa, for purpose of our discussion yaani uwekezaji zinatumika interchangeably, two means the agreement between two states, ( na hapa ndio vienna convention on law of treaties ina apply)

kwa hiyo mikataba hiyo ila lengo la kulinda uwekezaji, hakuna kitu kinachoitwa specific or generic. these are ground for protection of investors as against the host government.
they all bound by vienna na ndio rationale ya kwenda bungeni, to make concluded as such.

pili mkuu, unatupiga za mbavu, mikataba ya uwekezaji na mikataba ya biashara ina tofauti sana, japo inarandana, principle and rules zake ni tofauti, they may bave a baseline on the law of contract kwa sababu ni ndio msingi wa mikataba yote but they depart, kwa maana ya nature ya investment na biashara ziko tofauti.

tatu mkuu, fanya homework yako vizuri kwenye discharge ya contract, mikataba ya uwekezaji need serious mind, reliance on copy and paste ya completion of perfomance? serious breach? and frustration of contracts. ( lazima mpigwe kama akili ndio hizi kama ngoma ya DPW). imekula kweli hiyo boss.

iga ya uk, na UAE na kwetu na dubai ni vitu viwili tufauti, kuanzia kwenye compliance to the law of vienna of 1969, to the patriotism of the whole contract. kimsingi tumepigwa, mchana kweupe.
nendeni mkatoe elimu vijijini, watanzania wawaelewe, kula hawaitaji sana minds, upande wa khanga biashara kwishiney
 
Acha kumlisha matango pori mwenzako kauliza very serious, with innocent mind.
, IGA ni Mkataba, be serious pls, unataka kusema dpw wakianza kuoperate tukavunja makubaliano ya hiyo IGA hawawezi kutushitaki? wataondoka tu sababu ni makubaliano?

( makubaliano ya nchi mbili ni mkataba) rejea vienna convention on the law of treaties, 1969. kasome definition ya states, how is dubai identified, some instruments, ule ni mkataba.
kumbuka sio kila makubaliano ni mkataba ila makubaliano yenye nguvu ya kisheria ni mkataba. ( all agreements that can be enforced in the eyes of law is contract)

makubaliano yeyote yenye nguvu ya kisheria ni mkataba, angalia kwenye IGA ya JMT na Dubai Emirate, dispute settlement zina kazi gani?, choice of forum zina kazi gani?, choice of law zina kazi gani? rights and obligation zina kazi gani, hizi zote silent element za mkataba. huu ndio upotoshaji mkubwa unaofanywa na wanazi wa waungaji mkono wa DPW.
pande yeyote ikivunja mkataba huu inaweza kushtaki, na ikalipwa. na kwa bahati mbaya mkataba huu umeelemea upande mmoja, na tumejiweka kwenye nafasi ya kushitakiwa, maana ukipita huu mkataba rais yeyote akifuata lazima autupilie mbali.
 
Unajipotezea muda tu kujaribu kumuelewesha ingawa sisi wengine tunakushukuru.

Amandla...
 
Kwa kuanzia kutokana na hoja zako inaonekana foundation ya maswala ya mikataba huna.

Unapoona kuna sheria mahala popote elewa hiyo ni implied term. Ata mkataba wa kimataifa kama hiyo VCLT 1969 uwezi andika treaty bila ya vigezo vya humo for the most part.

Intergovernmental mental agreement na Bilateral Investment Treaty ni kitu kile kile.

Nimekueleza tofauti yake BIT ni general maana yake nini nchi inapoingia makubaliano na nchi nyingine mwekezaji wa kiwanda cha sukari, mkulima, mchimba madini, mvuvi etc atalindwa na na hiyo Treaty kwa sababu aina specification on investment.

IGA ni more specific on project/s atleast kwa hii ya Tanzania; it covers most items ambazo zipo kwenye BIT but centred on the specific investment and one sided on performance.

Both IGA and BIT kwa sababu msingi wake ni VCLT ili zitumike katika nchi husika inahitajika ratification ya mamlaka/taasisi sahihi ili ziwe sheria kwenye nchi.

Dhumuni la kufanya BIT/IGA sheria ni kwa sababu sheria za nchi ni implied terms kwenye mkataba.

Mkataba wa kibiashara/investment (technical term is commercial agreements) vigezo vyake vinavyoitambulisha ni sawa.

Commercial agreements inaisha kwa namna tatu nilizokuelezea; ila hayo mambo matatu yana vipengele vyake vingine na definitions zake, remedies zake (so ina cover mambo mengi sana) kuandika kila kitu ni report and no one has time for that.
 
IGA sio mkataba wa kibiashara, bali ni makubaliano ya kuingia kwenye kuingia mkataba wa kibiashara (ndio maana auna consideration). Makubaliano yoyote yasiyo na consideration (value of exchange) uwezi shitaki nayo mtu mahakamani.

Sasa makubaliano ya kibiashara (commercial agreements) yana aina tatu za terms.

1. Expressed terms most common ni consideration hapa ndio mnaelezana A anatoa nini B anatoa nini; na kila mtu anaelewa anapata nini in return.

Ndio maana kila siku mnaambiwa mambo ya muda hayapo kwenye IGA kwa sababu awajakaa kitako kuyajadili. Maana muda unategemea na amount of time in return of investment.

2. Customary terms (Implied terms) hizi ni industry norms ambazo zinatumika ata usipoweka kwenye expressed terms za mkataba. Mfano uwezi kunikodisha shamba halafu unitoe kabla ya kuvuna hiko hakipo na mifano mengine kadha wa kadha.

3. National Laws (implied terms) hizi ni sheria za nchi ambazo zitatumika mfano kodi, matumizi ya ardhi and so forth ambazo zina implications kwenye mkataba ata usipoziweka kwenye expressed terms (unless kuna exclusion exclause).

Sasa IGA/BIT lengo ni hili la tatu kuwa implied terms on future contracts kwa bandari ni ‘project agreements’ za baadae.

Mfano dispute resolution, termination of contract yote yapo kwenye IGA. Kwa maana hiyo hayo mambo hayana ulazima tena wa kuwa expressed kwenye future project agreements. Hila yasingekuwepo kwenye IGA definitely yangekuwa sehemu ya expressed terms.

So BIT inachofanya ni kuwakinga wawekezaji wa kigeni automatic kwenye baadhi ya terms but consideration hiyo ni lazima pande mbili zikae chini kwanza.
 
mkuu sheria za uwekezaji foundation zake ni mutual agreement between states parties in favour of the investors, or better say protecting investors, kwa sababu nature ya investment ni tofauti kati ya nchi na nchi, hakuna multilateral investment agreement binding to all states, hence states zinaweza amua makubaliano haya.

na ili makubaliano haya yakubaliwe kwenye jicho la sheria, the procedure under VCLT, 1969 ni lazima zicomply, kwa sababu ni states zinaingia.

ukiangalia mkataba wa mchongo tulioingia, hata dubai kimsingi sio nchi amekuwa defined as "state", it means ni agreement between two states parties, on the condition of protecting investors. that why naendelea kukuambia kuwa (inter-na- bi) zote ni lateral (sides) na zote ni treaty (agreement) entered between two states or government essentially they are one. the same are used interchangeably. na sifa zao za mikataba hii ni nchi zinaingia, kwa ajili ya entities. kwa hiyo yote ni mikataba, na zote ni sheria after ratification, and they acquire the same status, and can be tested before a competent forum.

narudia tena investment ni specific field, and not general when comes to its peculiarity, fanya homework yako vizuri its more than commercial agreement ni investment agreement ndio maana crafting yake ni tofauti.

acha kukariri kuhusu discharge, narudia tena investment contract may be simiral to commercial contract, but they are different things, ndio maana mkataba wa JMT na Dubai umekuwa mgumu kwa wataalamu wetu, ndio maana waarabu katupiga mchana kweupe, kwa kwenda na falacy ya generalization that investment ni commercial
 
kwani unadhani ni kitu cha ajabu unachojua wewe tu? ni bilateral boss, kasome VCLT, 1969 na soma mchakato wake ndio uje kutudanganya tena,

ila ni bilateral mkuu.
Nilyemuuliza swali alikuwa anadai mkataba kati ya UK na UAE ni Bilateral Agreement wakati IGA kati ya URT na Dubai sio Bilateral Agreement. Ndio maana nilimuuliza kama anajua maana ya Bilateral Agreement. Sasa kama unakubaliana nae basi tuelimishe sisi ambao sio learned kama ninyi kwa nini moja ni Bilateral Agreement na nyingine sio wakati zote ni mikataba kati ya "two parties".

Amandla...
 
wasemaji wa DPW wanapotosha sana,
sikubaliani nae kabisa, kwangu narudi kwenye lugha fupi tu sana tena sio ya kisheria ya kihesabu, uliyosomea mkuu


ngoja niiweke kwenye hesabu, (inter-government), kuna maneno mawili yaani, inter ikimaanisha between, kwa hiyo (Inter + governmental)= agreement between the governments,
therefore, intergoverment agreement = agreement between states, (kwa kingereza between inatumika panapokuwa na vitu viwili.

bilateral, etymologically limetokana na kilatini, bi means two, lateral means (sides)+ treaty (agreement at the level of state)= agreement between two states.

therefore, intergovernment agreement = bilateral agreement.

zote ni bilateral treaty, na ndio maana IGA kati ya Dubai na JMT imekwenda bungeni kwa mujibu wa ibara ya 63 (3) (e) ili kukidhi takwa la kisheria, zote zimenacquire status za sheria after the ratification, IGA ni katiba ya sheria za uwekezaji, IGA ni Protection of investor as against the host government.

the words are used interchangeably mkuu, terms zote zinamaanisha mkataba baini ya mataifa mawili, au serikali mbili, na makubaliano yeyote kati ya mataifa mawili yenye nguvu ya kisheria yanaitwa treaty
 
Mkubwa nadhani tunaongea kitu kimoja ila tuna tofauti ndogo; mainly due to your position on what you think is an investment contract and that is what steering you to a different conclusion to mine (which is the right one).

Yes kila nchi inaweza kuwa na sera zake tofauti za uwekezaji na nyingine zina malengo ya kuwavutia wawekezaji hilo sibishii.

Mfano sheria ikisema mwekezaji anaruhusiwa capital allowance mpaka ya dollar million moja hilo swala alihitaji kuliweka kwenye mkataba kwa sababu litakuwa kwenye finance act so it’s an implied term au kama ata pata grace-period kwenye tax hilo pia litakuwa kwenye sheria so alitakuwepo kwenye mkataba.

Kama kuna mambo ambayo hayapo kisheria then hizo privilege zitakuwa expressed kwenye mkataba kwenye majadiliano ya concession agreement/project agreement or whatever to do with the commercial contract.

What’s a commercial agreement (contract) ni mkataba wowote wenye value of exchange. Ata makubaliano ya wewe na mtoto wako kwenda kufunga geti la nyumba kila siku halafu baada ya week unampa tsh 10000 provided mmeandikiana au kuna shahidi; usipomlipa anaweza kwenda mahakamani.

Kinachoangaliwa ni five elements of contract; offer, acceptance, consideration, legality and capacity; provided those five elements are present thats a commercial agreement.

So even a $42 billion dollar investment will have those features and that’s what counts.

Makubaliano yoyote ya utakayoyaita ya kibiashara hasa yasiyo na consideration hayawezi kuwa enforced in the court of the law.

IGA and BIT usually don’t have consideration but might have other elements of what constitute as an elements of a commercial contract. But without a consideration it’s not a contract.

What a BIT/IGA does is to eliminate the need of having unnecessary repetitive expressed terms.
Mfano itaonyesha issues za ‘business efficacy’ ya mkataba wenyewe, ‘exclusion and limitations clauses’, dispute resolution process, legal capacity ya kuingia mkataba, stabilisation clauses, termination and so forth. Na ndio mambo yaliyo kwenye IGA kwa sehemu kubwa.

Lakini hakuna consideration terms, hakuna maelezo ya kina kuhusu maswala conditions, warranties and innominate terms. Hayo mambo definitions zake yatakuwa huko kwenye expressed terms za concession agreements.

Na hayo yaliyo kwenye IGA kwa sababu ni sheria ya huo uwekezaji so hizo articles ni implied terms za concession agreement za baadae.

Ndio maana mnaambiwa mambo bado hayaja kamilika. Na hiyo IGA as yet responsibility ya serikali kwa sasa ni kukaa chini na kujadili huo uwekezaji ila hawana lazima ya kukubali wanaweza sema consideration terms sio nzuri kwa TPA so atuwezi ingia mikataba ya project agreement. Ikipita miezi 12 toka isainiwe hakuna project agreement yeyote hiyo IGA aina nguvu tena kisheria.
 
Mkuu una akili timamu, mzalendo.
 
Kwanini usaini IGA na Memorandum?


Una akili timamu?
 
Wale nyumbu bado watakuja kusifia mama anafanya kazi nzuri sijui hiyo kazi nzuri ni ipi hata
 
mkuu naona nitarudia maneno yaleyale niliyoyatamka hapo juu, shida tunatofautiana kwenye understanding ya specific discipline on investment law,:
na tatizo kubwa ya investment laws is an archaic law but very recently discovered, kwa mfano bilateral investment ya kwanza ni kati ya German na pakistan, ya mwaka 1959. ni shida sana kwa nchi zetu na ndio maana tunapigwa sana kwenye mahakama za kimataifa, na hata kuingia mikataba hii, kwa mfano IGA na BIlateral ni shida kuelewa, hata bunge limehangaika, tunaambia makubaliano wengine mkataba, wengine mkataba, wengine ni makubalino, yaani ni shida sana.

mkataba wetu ni kichekesho mkuu, ni aibu sana kusema umeingiwa na wanasheria. am sure an investment lawyer can not enter into such agreement mkuu.

kwa faida ya rejea zako naomba tafuta vitabu hivi, these are legal puritan in investment laws, soma taratibu, chukua muda wako taratibu, ni self teaching books; they will teach step by step and all practical aspect za investment laws. utaona vizuri tofauti ya commercial law na investment laws, utagundua kama taifa tumekwama wapi, vinauzwa online you can buy mkuu,

1. Thomas machi (2021), vademecum of international investmet, University of West bohemia,
2. Cristina Elena Popa Tache (2020), Introduction to international investment law
3. Qiang Pen (2018), Public interest in international investment law: Balancing protection for investor and enrironment

ciao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…