Kumekuwapo na wimbi la Mafua yenye kuambatana na homa kali, maumivu ya mwili, kikohozi, kupoteza hamu ya kula, nk yasiyokuwa ya kawaida.
Zaidi sana leo hadi mechi ya wekundu wa Msimbazi na Kagera Sugar kule Kaitaba, imebidi kuahirishwa. Kisa na mkasa ugonjwa huu uliowang'ang'ania ghafla wengi wa wageni waliowasili kutokea Dar.
Taarifa ya ufafanuzi kutokea wizarani kuhusiana na hali hii ni kuwa huu ugonjwa ni wa kawaida. Kwamba hutokea mara kwa mara mwishoni mwa mwaka.
Kwa hakika taarifa hii ya wizara ni mfano wa majibu rahisi kwenye maswali magumu.
Hakuna mwaka wowote zaidi ya huu hali iliwahi kuwa hivi. Mwaka huu tumefikia hadi kufuta mechi wachezaji wanaumwa?!
Dalili za mvua ni mawingu. Mficha u*hi hazai. Pia mficha maradhi kifo humfichua.
Hala hala tusije kulaumiana.
Maisha ya watu ni muhimu zaidi kuliko kitu chochote.