Bwana Misitu,
malembeka18 na
dos.2020 nawaonea huruma sana kwa sababu naielewa sana hali mnayopitia.
Mimi sitaongelea hayo mavumbi na dawa zozote, sijawahi kutumia na sizielewi kabisa. Na awali ya yote niseme wadau wanaosema kula vyakula (walivyotaja na kunywa maji ya kutosha) na kutuliza akili wako sahihi kabisa, ingawa nafahamu ugumu wa hili la pili (la kutuliza akili). Kwa mtu ambaye hajapitia haya ni vihumu sana kuelewa ugumu wa dhana ya kutuliza akili (ni rahisi kumueleza mtu, kuliko mtu husika kulifanikisha). Nilielezee kidogo hili: Wengi tunaokuwa kwenye hili tatizo huwa tunakuwa tayari tushaathirika kisaikolojia.
Utasema mbona akili iko sawa, sina papara, nk, lakini ndani ya nafsi upo wasiwasi na sehemu ya hofu inayojiuliza "nitaweza?". Ni ngumu sana kuwa "normal" kama ambavyo ulikuwa unapoingia katika mechi wakati hupitii haya matatizo. Sasa ni nini nilichojifunza? NAFASI YA M/KE. Kiukweli ikiwa mwanamke uliyenanye anakupa "presha" na kuonesha anawalakini nawe ndiyo anakudhoofisha kabisa wakati wa pambano. Ikumbukwe, kwa wapitiaji wa hali yetu, ukishamaliza round ya kwanza (ambayo hutokea haraka kuliko kawaida) huwa tunahitaji muda wa kutosha kuanza upya.
Hapa ndipo kipimo cha saikolojia kilipo, na ndipo ambapo m/ke anaweza kukuondoa kabisa mchezoni ama kuisaidia saikolojia yako. Maneno huwa hayahitajiki hapa kutoka kwa m/ke maana lolote linaweza kukuondolea ujasiri. M/ke makini haoneshi kushtukia hali yako, atajua tu ushachemsha round ya kwanza na kusubiri round(s) zijazo, atakulia timing tu....ikisimama hata kidogo atairudisha ndani fasta (uzuri jamaa akianza kusimama akarudishwa ndani wewe ukiwa katika hali nzuri ya kimawazo anaamka zaidi hukohuko). Lakini bahati mbaya w/ke huwa wanatuvuruga hapa.
Hivyo usipokuwa na m/ke makini unahitaji uwe na uwezo mkubwa sana mwenyewe wa kujipa ujasiri (ni kazi kubwa kama nilivyoelezea awali lakini inayowezekana). Na uzuri ukiweza hata mara moja kufanya rounds zaidi ya moja, unakuwa ushaondoa dhana kuwa unashida...ni powerful statement going forward!
Nimeandika kirefu kwa vile ninaelewa sana mnayopitia, nilitamani hata tungekutana tupeane uzoefu. Binafsi nawaelewa sana waliotaja vyakula, maji, mazoezi na hali nzuri ya akili.