Tuelimishane hapa kuhusu hii bahati na sibu ya BIKO

Nimeshiriki mchezo huu, na niliposhiriki wamekuwa wakinitumia msg zao za kunihamasisha nishiriki au msg za kutangaza washindi wao, Cha ajabu ni hizi msg mbili za kutangaza washindi hebu angalieni namba za simu za washindi! View attachment 533320

Kwani wamekulazimisha ucheze bahati nasibu yao Mkuu? Hivi kama ingetokea ume ' beti ' halafu kweli ukashinda hiyo 20 M yao ungekuja ' kuwapovukia ' hivi humu JF kama ulivyofanya sasa baada ya kupatwa na hasira ya ' Kubeti ' kila siku lakini mpaka sasa bado hujaambulia ' Senti ' yoyote?

Na bado ' Kudadadeki '.
 
Hivi watu huwa mnacheza hiyo jamboz???
Nipeni mie ela zenu hizo basi niwatunzie
 
wadanganye na kutapeli kijanja sasa sio kiboya namna hiyo

 
mi kinachonishangaza ni hawa wanaotoa buku buku zao kucheza huu upuuzi ni wajinga kiasi gani?? kweli maarifa ukiyakosa unaangamia kirahis sana
 
Mtu na akili zako timamu unacheza hiyo michezo.

Mbona njia halali za kutafuta pesa zipo.

Hii michezo ni ya wavivu wavivu wanaotaka pesa huku wamelala vitandani na mtaendelea kupigwa sana maana wenzenu wameshajua udhaifu wenu
 
Wengi mnaponda humu ila nina uhakika asilimia kubwa mmecheza, mmepigwa! Majinga kama nyie ndo yaliwayo, mjini mnataka watu wakale wapate pesa vipi wakati kuna wajinga ambao ni mtaji?? Acha mpigwe tu!!
 
Sisemi kitu sio kama sina cha kisema ,bali nashangaa na kuzaliwa mjini mapigwa na mburulaz kama biko wanaoshindwa kudesign uongo wao!
Maskini 10 000 yangu si ningeenda nayo kwa changu kubadili ladha za papuchi?
 
Jamaa ni matapeli wa wazi wazi kabisa wanatudanganya kwakuwa hatuonagi wanavyofanya uo usanii wao.

bora ubeti tuu mpira nk matokeo ndio yanaamua ule au uliwe.hii biko wahuni wahuni wamejikalia wanaamua nani ashinde wanagawana tuu ela zetu.acha fasta utafilisika.
 
Hapo ndo na shindwa kujua kazi za maboard kama Tanzania Gaming Board. DCI na Usalama jamani hawa wakifanya kazi zao vizuri huwezi pata upuuzi huu
 
Asante. Wengi Umetutoa matongotongo! Nilikuwa nakaribia kushawishika nianze kushiriki, kumbe matapeli!?
Lakini nimebaki najiuliza, hadi hali hii inajitokeza, Wawakilishi wa Bahati Nasibu ya Taifa wako wapi? Maana mara zote matangazo ya matokeo ya michezo ya kubahatisha hutolewa utambulisho wa kuwepo kwa Mwakilishi wake! Imekuwaje kwa hilo? Ama ano ni washiriki katika utapeli huu?!
Haya no "MAJIPU", yatumbuliwe haraka.
 
Kama vipi waripotiwe hawa wapuuzi wezi wakubwa...wafungiwe na wafunguliwe mashtaka kama wenzao hawa ni wezi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…