Tuelimishane: mazishi ya Membe yamebeba sura ya msiba wa kiongozi mkubwa Kiitifaki. Nini maana yake

Tuelimishane: mazishi ya Membe yamebeba sura ya msiba wa kiongozi mkubwa Kiitifaki. Nini maana yake

Mnaofatilia msiba huu wanasoma wasifu wa marehemu.

Membe ni mwana idara wa Usalama wa Taifa. Na amepigana vita vya Kagera kama jasusi na amesimamia uundaji wa serikali mpya ya Uganda baada ya vita.

Msoma wasifu, amesema wazi mwaka ambao Membe ameanza kazi ndani ya Idara ila hajasema kama alistaafu.
 
Je ni sahihi kutaja wssifu wa mfanyakazi wa idara?

Hawajawahi kufa? Maana hatykuwahi kusikia kabla hili jambo la marehemu kutajwa kama.mfanyakazi wa idara
 
Poleni watanzania mlioguswa na msiba huu mzito wa Bernard Kamilius Membe.

Ninaangalia live capture ya sherehe ya kumuaga Marehemu Membe hapo Karimjee. Naona kuna itifaki imeandaliwa kwa namna ambayo inanipa dukuduku kufahamu undani wake.

View attachment 2621216
Protokali za Mkuu wa Nchi kushiriki msiba wa mtumishi ama mstaafu zinafahamika. Na ikumbukwe marehemu Membe alikuwa amestaafu na sheo chake cha juu cha mwisho kilikuwa ni Waziri wa Mambo ya Nje.

Nimeona Serikali nzima imejaa pale Karimjee, na hata wakuu wa mihimili ya dola nao wameshiriki kupata mimbari ya kutoa salaam kwa protokali za serikali.

Nafahamu humu JF kuna wataalam wengi, naomba tuelimishane inakuwaje huu msiba kuwa na protokali za juu kuliko misiba hata ya mawaziri waliowahi kufariki wakiwa madarakani.
Tunamkumbuka aliyekuwa Waziri wa Ulinzi alipofariki hatukuona ukuu wa protokali namna hii.

R.I.P. Membe

Kuna sababu kadhaa,
Ni Waziri mstaafu, kada na mwana mtandao…

90% ya waliopo Serikalini ni watu amefanya nao kazi kwa muda mrefu, wengine walioko kwenye system ni ndugu na rafiki zake.

Pia ukumbuke huu msiba unaigusa Msoga, sasa unapozungumzia msoga si ndo serikali yenyewe?
 
Kwa hiyo kama ukifahamika serikalini ndo Hazina iingie gharama hizo kubwa?
 
Back
Top Bottom