Tufanye nini kama taifa ili vijana wetu wawe na moyo wa kujitolea (kufanya jambo hata kama hatolipwa pesa) ndani ya jamii??

Nina Akili Ndogo Sana

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2026
Posts
865
Reaction score
1,125
NB: Nina Akili Ndogo Sana.

Just imagine gari yako imekwama kwenye mchanga maeneo ya Mbagala Chamazi kisha vijana watatu (3) wanakusaidia kuisukuma mpaka inafanikiwa kutoka.

Baada ya hapo, badala ya vijana kusema "kaka tunakutakia safari njema" wao wanasema "kaka tuachie hata ya soda basi"

Au, unamuita mtoto wa jirani unataka kumtuma dukani akakununulie majani ya chai na mkate mkubwa, mtoto wa darasa la 6 anakuuliza, utanipa shing' ngapi?? Au chenchi ikibaki yangu??

Unakuta vijana wanashindwa hata kwenda katika kituo cha kulelea watoto yatima na kufanya usafi kwa kufagia hata lisaa limoja tu basi.

Wakuu, tuna kizazi cha namna gani jamani?? Tufanyeje sisi kama taifa tuondokane na mentality hii ya "pesa ndio kila kitu"??

NB: Zingatia sana jina langu.
 
Kujitolea Hadi uwe unacho. Mtu huna pesa, chakula, mavazi, malazi etc unajitoleaje ?
 
Hivi kwani mnaishi wapi wakuu, mbona hivi vitu asilimia kubwa ya vijana wanafanya sana bila kuhitaji malipo yoyote yaani kwa moyo mmoja
 
NB: Nina Akili Ndogo Sana.

Just imagine gari yako imekwama kwenye mchanga maeneo ya Mbagala Chamazi kisha vijana wanakusaidia kuisukuma mpaka inafanikiwa kutoka.

Baada ya hapo, badala ya vijana kusema "kaka tunakutakia safari njema" wao wanasema "kaka tuachie hata ya soda basi"

Au, unamuita mtoto wa jirani unataka kumtuma dukani akakununulie majani ya chai na mkate mkubwa, mtoto wa darasa la 6 anakuuliza, utanipa shing' ngapi?? Au chenchi ikibaki yangu??

Unakuta vijana wanashindwa hata kwenda katika kituo cha kulelea watoto yatima na kufanya usafi kwa kufagia hata lisaa limoja tu basi.

Wakuu, tuna kizazi cha namna gani jamani?? Tufanyeje sisi kama taifa tuondokane na mentality hii ya "pesa ndio kila kitu"??

NB: Zingatia sana jina langu.
Katiba ibadilishwe ili haki itendeke. Hapo vijana watakuwa na ari ya kujituma.
 
Nenda halmashauri mwajiriwa hakufanyii kazi yako hata ya kutia saini document mpaka uumpe chochote wakati analipwa mshahara na hiyo ndio kazi yake

Athari za ubepari hizo ujamaa ushajifia mbele
 
Asije akajaribu huo ujinga kwangu. Ataacha ndala.
 
Tulisukume bure uondoke ukakae mbele ya kamera mitandaoni uwaambie vijana wafanye kaz waache kulalamika
 
Back
Top Bottom