Tufanye nini na hizi clip zinazopotosha Historia ya Tanzania?

Unaangalia kila kitu kwa miwani ya dini inakua ngumu kuKuchukulia seriously.

Kiarabu ni official language TZ? Kama ni official language Znz, kwanini hujalalamika huyo mtu kusema ni official language hadi TZ mainland?
Bufa,
Kweli maneno yako mimi nimetafiti sana katika historia ya Uislam Tanzania.

Ikiwa wewe huchukulii "serious," hilo si ajabu ni wewe una hakika na ukitakacho.

Lakini nimealikwa kuzungumza vyuo vingi katika somo hilo.

Naamini unakijua kitabu changu, "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika," (1998).
 
Bwana Mohamed Said, natamani kukutunukia shahada maalum juu ya utetezi wa Imani yako na waumini wenzako. Upo vizuri one day yes
 
Bwana Mohamed Said, natamani kukutunukia shahada maalum juu ya utetezi wa Imani yako na waumini wenzako. Upo vizuri one day yes
Big...
Sitetei imani nikiwa na maana Uislam kama dini.

Elimu hii sina kiasi cha kuweza kuhubiri.

Ninachotetea ni historia ya uhuru wa Tanganyika ambayo ni historia ya Waislam wa Tanganyika kwa umoja wao.

Historia hii ni historia ya wazee wangu babu na baba zangu.

Ilifutwa ikawa historia inayofundishwa ni ya Julius Nyerere peke yake.


''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968)
The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika,''
Minerva Press, London 1998​
 
Kleist hatokei sana kwenye historia ya Tanganyika kwa sababu hakuwa Mzawa wa hapa Tanganyika. Huyu alikuwa Mzulu wa Afrika ya Kusini.

Nafananisha historia ya Kleist hapa Tanganyika na ile ya Okello kule Zanzibar. Naye hatajwi sana kwa vile siyo Mzanzibar. Inaonekana tabia ya kudharau wageni waliochangia pakubwa uhuru wetu ni ya watu wa bara na visiwani

😅😅
 
Kinyungu,
Wanahistoria hawakuandika mchango wake kwa kuwa baba yake alitoka Mozambique.

Sikuwa najua hili kuwa kuna uandishi wa historia wa namna hii.

Vyuo gani vinafundisha hivi?

Hivyo kusema ndiyo maana historia ya Abdul Sykes na nduguye katika kuunda TANU ilifutwa kwa kuwa babu yao hakuwa kutoka Tanganyika?

Sasa kipi kilibadilika Abdul na Ally Sykes wakapewa medali ya Mwenge wa Uhuru katika kuadhimisha miaka 50 ya uhuru?

Mbona leo vyombo vingi vya habari pamoja na vya CCM na serikali wanakuja kunihoji kuhusu mchango wa akina Sykes kwa TANU, Nyerere na kupigania uhuru wa Tanganyika?

Kuna mabadiliko?
 
Unatuambia kuwa wakristu, wapagani, wahindu wasio na dini hawana nafasi katika historia yako ya uhuru wa Tanganyika. Historia ya uhuru Tanganyika ni historia ya wazee wako na rafiki zao! Kwa mtazamo wako hata waislamu ambao hawakutoka Tabora na Gerezani nao hawana nafasi katika historia ya hiyo Tanganyika.

Kwa mtazamo huu una tofauti gani na wale ambao waliigeuza historia ya Nyerere kuwa ndio historia ya uhuru wa Tanganyika? Hautofautiani nao kwa sababu kwako wewe historia sahihi ya uhuru wa Tanganyika ni ya wakina Sykes.

Amandla....
 
Fundi...
Hapana siwezi kusema hivyo.

Kitabu cha Abdul Sykes nimejitahidi kueleza mengi.

Muhimu hapa ni ikiwa wewe unaona wapo ambao mimi sikuwataja ukachukua fursa hii kuwataja wakajulikana.
 
Fundi...
Hapana siwezi kusema hivyo.

Kitabu cha Abdul Sykes nimejitahidi kueleza mengi.

Muhimu hapa ni ikiwa wewe unaona wapo ambao mimi sikuwataja ukachukua fursa hii kuwataja wakajulikana.
Mohamed, mbona unakana ulicho andika? Nimekuwekea ulichoandika lakini bado unaruka! Mimi ninaowajua ndio hao unasema historia ya Tanganyika sio yao kwa sababu wao sio waislamu.

Amandla...
 
mudi unaonaje umpelekee samia mswada afute historia ya nyerere mashuleni na vyuoni ili ifundishwe ya wazee wako wacheza bao ?
 
The Messenger of Allah [SAW] said: 'Whoever changes his religion, kill him.'

Whoever changes his Islamic religion, kill him' Hadith - Sahih Al-Bukhari (9:57)

Kwamba Uislamu unaruhusiwa kusilimu na kujiunga ila kuhama uislamu hurusiwi adhabu yake ni unakatwa kichwa

mudi aliogopa watu wakiwa huru watamkimbia kwenye dini yako ndo maana anaitetea na jambia.
 
Mohamed, mbona unakana ulicho andika? Nimekuwekea ulichoandika lakini bado unaruka! Mimi ninaowajua ndio hao unasema historia ya Tanganyika sio yao kwa sababu wao sio waislamu.

Amandla...
Fundi...
Mimi si mtu wa mabishano.

Huenda tatizo kwako ni jinsi unavyotafsiri niliyoandika.

Historia hii nimeiandika kitabu kina miaka 25 tunakwenda chapa ya 4.

Kitabu kimesahihisha historia iliyokuwako.

Mimi sina sababu ya kurejea tena kwenye kitabu hiki.
 
Mimi sizungumzii kitabu chako ambacho kwa kweli sina mpango wa kukisoma.

Nazungumzia ulichoandika humu leo katika kurasa za JF.

Amandla....
 
Mohamed, hivi ndivyo ulivyoandika leo.
Nilicho "quote" kabla ni hicho nilicho bold. Umesema kuwa historia ya Tanganyika ni historia ya waislamu na historia hiyo ni ya wazee wako babu na baba zako. Kwa maneno haya, si unamaanisha kuwa wasio waislamu historia ya Tanganyika haiwahusu? Au kuwa mchango wao ni mdogo mno kulinganisha wa waislamu hasa wale ambao una undugu nao? Haya ni maneno yako, sio yangu. Kama tafsiri yangu ina walakini nielimishe ulikuwa una maana gani ulipoandika haya maneno.

Amandla....
 
mudi unaonaje umpelekee samia mswada afute historia ya nyerere mashuleni na vyuoni ili ifundishwe ya wazee wako wacheza bao ?
Luku...
Nakusihi niite kwa jina langu Mohamed au Mzee Mohamed.

Usinikate jina.
Mimi sasa ni mzee.

Haipendezi si kwangu wala kwako.

Unanitukania wazee wangu.
Kwa nini kaka iwe hivi?

Nimekuudhi kwa mimi kuchangia katika historia ya nchi yetu?

Kwa nini historia ya Nyerere ifutwe?

Historia ya Nyerere ipo kama ilivyoandikwa na historia ya wazee wangu imekuja na kupata umaarufu baada ya zaidi ya miaka 50 toka uhuru upatikane.

Wasomi wakubwa wa Tanzania wakiongozwa na Prof. Issa Shivji wameandika "Nyerere Biography," (2020).

Huu ni mchango mkubwa katika kuitunza historia ya nchi yetu.
 
Fundi...
Hakika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika ni historia ya Waislam na kitabu changu kimesema hivyo: "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika."

Mimi sitaabishwi na vipi utatafsiri maneno yangu.

Naweza nikipenda nikakunyamazia kama baadhi ya watu wanavyonishauri.

Hii ni historia ya wazee wangu na nimeiandika kwa msaada wao wengine wameushi na kukiona kitabu na wengine wametangulia mbele ya haki kabla ya kazi kukamilika.

Ninachoshukuru ni kuwa Mwalimu Nyerere kakidiriki kitabu na kakisoma.

Kutokana na kitabu hiki ndipo alipomkubalia Prof. Haroub Othman atengeneze jopo waandike maisha yake.

Mazungumzo ya Mwalimu Nyerere na Prof. Haroub Othman ninayo nimeyahifadhi kama nilivyoyapokea kutoka kwake.

Nilikuwa mmoja wa watu waliochangia kitabu hicho katika kueleza historia ya Mwalimu Nyerere alivyopokelewa na wazee wangu alipofika Dar es Salaam mwaka wa 1952.

Nalishukuru jopo hili kwa kueleza kuwa Maktaba yangu ni katika maktaba tatu bora zilizohifadhi kumbukumbu nyingi za Babu wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Maktaba nyingine ni ya Salim Ahmed Salim na ya Brig.General Hashim Mbita.
Picha hiyo hapo chini TBC 1 wakinihoji kuhusu Nyerere Biography


Kulia ni Bi. Chiku bint Said Kisusa (mke wa Shariff Abdallah Attas), Bi. Titi MOhamed na kushoto ni Bi. Tatu bint Mzee, Julius Nyerere ni huyo hapo wakimuaga safari ya kwanza UNO 1955.
 
Mohamed, mbona awali ulikana maneno hayo? Maneno ambayo yanaweka wazi kuwa kwako wewe Nyerere na wakristu wenzake walikuwa "supporting act" ya ndugu na jamaa zako. Unajua kusema kuwa uliambiwa na Profesa Othman kuwa kitabu chako ndicho kilichomfanya Mwalimu akubali historia yake iandikwe. Mimi binafsi sijawahi kukupinga kwenye suala la kuandika historia ya ndugu zako. Ninachokupinga ni wewe kufanya historia yao ndio historia ya nchi yangu. Naamini kuwa historia ya Tanganyika sio ya waislamu peke yao, bali ni historia ya wale wote ambao bila kujali dini, kabila, rangi, utaifa ( kuna wakenya, waingereza, wamarekani, waghana, waganda,na wanyasaland wengi tu waliochangia historia ya hii nchi) na jinsia zao. Wakina Abdul Wahid hawakushirikiana na wakina Julius kwa sababu walitaka waislamu waongoze nchi hii. Ni wewe ndio unaowavisha hilo joho la udini. Hao wakina mama waliomsindikiza mkatoliki airport (na unajua hawakuwa peke yao) hawakufanya hivyo kwa sababu ya uislamu wao bali kwa utanganyika wao. Hapo airport walikuwepo watu wa dini zote.

Kwenye hili la udini nitakupinga siku zote. Kunijibu au kuninyamazia ni uamuzi wako. Mimi kila ninapoweza nitakujibu.

Amandla...
 
Fundi...
Hakuna tatizo.
Sikuzuii kupinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…