Tufanyeje ili wanasiasa wenye agenda zao wasiingilie michezo? Ni wavugaji wanaoua michezo

Tufanyeje ili wanasiasa wenye agenda zao wasiingilie michezo? Ni wavugaji wanaoua michezo

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Leo ilikuwa mechi ya watani wa jadi SIMBA na Yanga. Maarufu kama Deby ya Kariakoo.

Michezo pia ni siasa.. Lakini pale inapokuwa ni siasa safi bila agenda za siri nyuma yake.. Kinyume chake ni uchuro wenye nuksi mbaya na laana!

Mimi ni mwana SIMBA original kabisa.. Na Nilikuwa na imani kubwa timu yangu itanifuta machozi leo. Lakini kitendo cha kuona tambara jekundu lenye nakshi ya picha ya mwanasiasa kilinikata stimu kabisa na kujua mwanzoni kabisa tutafungwa.

Hayo matambara hayajatengenezwa na pesa za SIMBA.. Kwanini kampeni mpaka huku? Kwanini tusiachwe tufurahie maisha kidogo.

Haki ya nani nilipoona ile picha na ule wekundu nikakumbuka damu nyingi iliyomwagika isiyo na hatia kwasababu tu ya siasa

Haya mahela yote yanayotumika kutengeneza matangazo yote haya kwenye kila tukio nchi nzima yanatoka wapi?

Huyu mwanasiasa kama anadhani anaji brand kapotea njia vibaya mno.. Branding yenye baraka ni kuulinda, kuutunza na kuuhudumia uumbaji wa Mwenyezi Mungu na tunu zake na rasilimali zake zote

Mapambo yakizidi badala ya kupendeza huchukiza. Manukato yakizidi badala ya kuvutia hukarahisha.. Kuna baadhi badala ya kunukia hunuka!

Sasa hivi hakuna kunukia tena bali ni kunuka! Tambara la leo limetunukia harufu mbaya.. Tumetengwa na kukimbiwa na nguvu chanya. ! Badala ya kufungwa tukajifunga.. Tujitenge na hawa wanasiasa na siasa zao..hii ya leo ni warning
IMG-20241019-WA0115.jpg
 
Hizo timu zimepoteza utamu wake Mimi niliacha kuzifatilia tangu 2007 nikiwa darasa tano .

Wangebaki na siasa zao then mpira ukabaki unajitegemea.

Ukiachana na yote hii yanga ya sasa ni unstoppable
 
Yanga kuna lijinga limoja lilikuwa pale chini, kashika picha ya Samia. Alipotugeuzia tukaiona tulimuonyesha kwa ishara ya toka hapa na lipicha lako. Akakoma kugeuza mpaka mpira ukaisha. Watuache tuenjoy mpira jamani. Kwani shida nini? Mbona nguvu nyingi sana inatumika?
 
Back
Top Bottom