Tuhuma nzito ya ufisadi wa kupora ardhi mpaka sasa haijajibiwa

Mataga wanasema Magu hatakuwa rais wa kwanza kujimilikisha eneo kubwa hivyo hapa Tz, yeye anafuata nyayo za watangulizi wake. Kama Mwinyi, Mkapa na Kikwete wanamiliki maeneo hayo makubwa, kipi cha ajabu kwa Magu?!
Magufuli ni muumini wa kikristu mzuri, hawezi kufuata nyayo za Mafisadi kama Kikwete, mkapa na Mwinyi

Kamwe msimfananishe Magufuli na utopolo
 
Jiwe ni kabaila, bwanyenye, mnyonyaji, kupe, Mnyarubanja Halafu anajidai kumuenzi baba wa Taifa. Miaka mitano tu umeshajichukulia ardhi kubwa namna hiyo je ukikaa 10?

Baba wa Taifa alikaa madarakani miaka 23 lakini alishindwa kujenga nyumba yoyote ya maana kijijini kwake mpaka alipojengewa na Jeshi!, wewe miaka 5 una hector 25000!

Acheni kuita CCM chama cha kijamaa, hakuna ujamaa wa kutumia cheo chako kwa maslahi binafsi!. CCM ya leo ni makupe!, Wanyonyaji wakubwa!

Wanajifanya eti wanakata mirija, kumbe wao wanasimika mirija mikubwamikubwa tena ya chuma. Wanyonyaji wakubwa!
 
HAWEZI KUIJIBU HOJA HII , NI NZITO KWAKE ATABAKI NAYO MOYONI TU MPAKA ANATOKA MADARAKANI.
 
Ekari 25000 sio mchezo tufanye kila hekari moja ni 1M

1,000,000 × 25000 = 25,000,000,000/=

Sasa jiulize magufuli anao uwezo huo?
Na kama anao huo uwezo atuambie alinunua kwa nani na kwa utaratibu upi?
Aliekuambia hekari maoja no 1M ni Nani?
 
Kuna maeneo huku tupo jamaa yangu moja anamiliki hekari 1500 na si mfanyakazi, wakati huohuo Kuna watu kinijini hapo hata hekari 1hawana. Hebu punguzeni ujinga
 
Ahh eka elfu 25!

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Hahhahahha... Tangu lini CHADEMA mmeanza kupinga ufisadi? Agenda hiyo ilishakufa tangu 2015 pale mlipogeuka madodoki ya kusafisha watu.
Hebu tuonyeshe mahakama ya mafisadi aliyoihubiri John
 
Ukiona kimya ujue ni kweli
 
Ya Ngoswe mwachie Ngoswe, Soma hapa ‘Migogoro ya ardhi husababisha mauaji na hapa Migogoro ya ardhi Kagera yachangia ongezeko la mauaji - TimesMaijira
 
Mkuu ulizia wenyeji wa Kagera na hasa hasa wilaya za Muleba, Bukoba, Karagwe na kadhalika...Wenyeji wa kule migogoro ya ardhi huwa ni ya "EKIBANJA" mashamba ya ukoo yenye migomba na mibuni...hiyo ndiyo migogoro ambayo kesi zake huwa zinafika hadi makama za rufaa! mtu anaweka hadi wakili kwa kesi ya kipande kidogo cha mita 75 za mraba! Ardhi aliyomilikishwa JPM kule inafahamika kama "ORWEYA" kwa maana ya mbuga na mapoli nyingi zipo chini ya serikali za vijiji ambao hata wewe unaweza kwennda kununua kwa ajili ya kuwekeza!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…