Mkuu ulizia wenyeji wa Kagera na hasa hasa wilaya za Muleba, Bukoba, Karagwe na kadhalika...Wenyeji wa kule migogoro ya ardhi huwa ni ya "EKIBANJA" mashamba ya ukoo yenye migomba na mibuni...hiyo ndiyo migogoro ambayo kesi zake huwa zinafika hadi makama za rufaa! mtu anaweka hadi wakili kwa kesi ya kipande kidogo cha mita 75 za mraba! Ardhi aliyomilikishwa JPM kule inafahamika kama "ORWEYA" kwa maana ya mbuga na mapoli nyingi zipo chini ya serikali za vijiji ambao hata wewe unaweza kwennda kununua kwa ajili ya kuwekeza!