Tuhuma nzito ya ufisadi wa kupora ardhi mpaka sasa haijajibiwa

Hahhahahha... Tangu lini CHADEMA mmeanza kupinga ufisadi? Agenda hiyo ilishakufa tangu 2015 pale mlipogeuka madodoki ya kusafisha watu.
Kwahiyo huko kwenu ni pachafu ?
 
Katika bandiko lako uliandika kuwa kagera hakuna migogoro ya ardhi, lakini katika utetezi ukasema iko migogoro, Rekebisha kauli yako halafu tuendelee.

Nimekwambia ya Ngoswe mwachie Ngoswe! Kama hiyo ardhi inayoitwa orweya ingekuwa inaweza kupatikana kirahisi hivyo si watu wangeenda kulima huko! Angalia pale Bigoro, wananchi walianza kulima kwa kupewa hata eka moja tu; walitoka huko vijijini wakaja kulima hapo porini - ni kwa sababu huko waliko hakuna ardhi ya kutosha. Wamelima wanakaribia kuvuna wakatolewa eti ni eneo la wafugaji. Wamerudi wapi? Huko walikokuwa wamekimbia kwa ukosefu wa ardhi! Hivi wangepewa hapo pa mheshimiwa si wangeshukuru sana. Ndugu yangu kumbuka watu wanaongezeka lakini ardhi haiongezeki kihivyo; mtu mmoja anapochukua eneo kubwa peke yake hilo ongezeko la watu litaenda wapi?
Umesema JPM alimilikishwa, sawa, ila mimi nikauziwe - kwa nini
 
Jamaa hata asipotangazwa na NEC lakini tutampigia kura za heshima kwa kutufungua mambo mengi sana watanzania
 
Mataga wanasema Magu hatakuwa rais wa kwanza kujimilikisha eneo kubwa hivyo hapa Tz, yeye anafuata nyayo za watangulizi wake. Kama Mwinyi, Mkapa na Kikwete wanamiliki maeneo hayo makubwa, kipi cha ajabu kwa Magu?!
Si nilisikia Waziri mkuu wa zamani walimnyang'anya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…