Mwanantogakulya
Senior Member
- Mar 18, 2025
- 157
- 155
Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Maswa, Joseph Timothy Kaare, anakabiliwa na malalamiko yanayodai kuwa amekuwa akiendesha shughuli za baraza hilo kwa kutumia maamuzi binafsi yanayokiuka taratibu na miongozo ya Serikali.
Baraza hilo, ambalo lipo chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, lina jukumu la kusikiliza na kuamua migogoro ya ardhi katika wilaya hiyo.
Kwa mujibu wa malalamiko yaliyowasilishwa na baadhi ya wadau, Mwenyekiti huyo anadaiwa kumuondoa katika majukumu ya ukarani Karani wa Baraza, Salome Zacharia, bila kufuata utaratibu unaotakiwa na baadaye kumkabidhi majukumu hayo Rachel Felician Kihinga, ambaye awali alikuwa akifanya kazi za usafi katika baraza hilo.
Walalamikaji wanadai Rachel amekuwa akifanya kazi zinazodaiwa kuwa nje ya majukumu yake, ikiwemo kuingia katika ukumbi wa usikilizwaji wa mashauri wakati kesi zikiendelea, kuandaa nyaraka mbalimbali za baraza, kutoa wito kwa wahusika wa mashauri na kutumia muhuri rasmi wa baraza.
Malalamiko hayo pia yanadai kuwa muhuri wa baraza umekuwa ukihifadhiwa na Rachel badala ya mtumishi mwenye dhamana hiyo, jambo ambalo walalamikaji wanasema linaibua maswali kuhusu usalama wa nyaraka na uhalali wa baadhi ya taratibu zinazofanyika.
Aidha, walalamikaji wanadai kuwa Mwenyekiti huyo amekuwa akiendesha baadhi ya mashauri nje ya ukumbi rasmi wa kusikilizia kesi na badala yake kutumia eneo la korido ndani ya jengo la baraza, jambo wanalodai halizingatii utaratibu wa uendeshaji wa mashauri.
Katika malalamiko hayo, imeelezwa kuwa licha ya suala hilo kufikishwa Wizara ya Ardhi na mamlaka nyingine za Serikali, hatua zinazodaiwa kutarajiwa na walalamikaji bado hazijachukuliwa, huku wakieleza hofu kwamba hali hiyo inaweza kuathiri utoaji wa haki kwa wananchi, hususan wenye uwezo mdogo wa kifedha.
Walalamikaji wamezitaka Wizara ya Ardhi pamoja na mamlaka nyingine za Serikali kufanya uchunguzi wa kina kuhusu madai hayo na kuchukua hatua stahiki endapo yatabainika kuwa na ukweli.