Tuhuma za JWTZ kupiga raia huko Kawe: Tunaomba Waziri wa Ulinzi ajitokezee kukemea, kulaani, na kukataza jeshi kujichukulia sheria mkononi

So sad indeed
 
Na nyinyi raia wekeni utii kwa askari wenu. Kumfanyia baya askari ni kulishushia heshima jeshi. Kama kuna uonevu jeshi lina mamlaka zake, ukiripoti jambo linafanyiwa kazi.
Kwanza mwanajeshi ndie alienza ugomvi.
Pili hakuwa amevaa kijeshi hivyo kijana alijua anagombana na raia mwenzake.
Tatu jeshi alimchapa vibao kijana mbele ya watu, hivyo kupelekea kijana kuhamaki na kuamua kujihami kwa silaha iliyopelekea mauaji.

Hata hivyo tunacholaumu, ni kitendo cha jeshi kutembeza kipigo kwa watu zaidi ya mia moja (wakiwemo wakinamama ambao walikuwa wanajaribu kuwaokoa watoto wao) kwa sababu et ya kosa la mtu mmoja.

That it doesn't make sense.
 
Muuaji ni mtu mmoja, na tayari alikuwa ashakamatwa. Raia wanaopigwa hawakumuua mtu , wala kuwepo eneo la tukio, na wengine hata taarifa ya huyo mwanajeshi kuuwawa walikuwa hawana.

Hivyo hapakuwa sababu ya kuwapiga wasiohusika wala kufahamu kilichotokea. Pia na wewe hauna haki ya kutukana watu waliopigwa wakati wakitoka kwenye mishughuliko yao ya kujitafutia riziki zao bila kujua wala kufahamu kilichotokea eneo hilo.
 
mnaua luten kanali mchekewe?lazima mpate doso mbebe dunia.
 
mnaua luten kanali mchekewe?lazima mpate doso mbebe dunia.
Soma hapo chini, maana naona baadhi yenu hamjajua kwanini nimeandika hii thread.

Sitetei mauaji yaliofanywa na kijana. Nnachotetea ni ile ya kupiga watu hovyo bila sababu, huku wakifahamu kwamba wengi hao hawakuwa eneo la tukio.
Kiongozi kauwawa na mtu mmoja, lkn waliopigwa na kujeruhiwa ni zaidi ya watu mia moja, ambao hawakuwa eneo la tukio, na wala hawakuwa wanafahamu kilichotokea.
 
Mkuu yalikukuta nini?
Hapana mkuu, yalimkuta baba yangu mdogo (umri miaka 55) aliekuwa anatokea kwake Tabata kuelekea Kawe kumtizama mdogo wake (bamdogo) ambae ni mgonjwa.

Sasa angalia umri wa huyo baba yangu mdogo aliepigwa, tena haishi hapo Kawe na pia hakuwa anafahamu hata kilichotokea siku hiyo.
 
Kuna shida kwa wanajeshi wetu. Uwezo wao wa kuwaza na kung'amua mambo ni Mdogo sana na pia ni washamba. Hao raia wanaopigwa na surubishwa ndio waliomuua huyo mkuu wao ?? Hii ndio Shida ya kuchukua form four failure. Uwezo mdogo wa kufikiri kuanzia kwa Ma luetenants. Kulikuwa na shida gani kama angempisha huyo dogo au kumpotezea tu akaendelea na safari.
 
Mkuu ulichoandika hapa kinaonesha kuwa wewe ni mtu muungwa san, unaweza kuishi vizuri na watu mbali mbali tena kwa amani.

Naunga mkono hoja yako.
 
Mkuu raraa reree thank you so much mkuu.

Lakin ikikupendeza na wewe tia neno kidogo katika mada. Nina imani wewe ni muungwa na mwenye upendo kwa watu.

Hivyo neno lako litaweza kubadilisha mawazo ya watu mbali mbali, ambao humu wamekimbilia kuandika lawama bila kujua chanzo na sababu ya kuandika thread hii.
 
Jeshi lolote iwe jwtz, polisi, uhamiaji nk hawaruhusiwi kuvunja sheria.

Kuchukua sheria mkononi ni moja ya kosa la kuvunja sheria. Hivyo wahusika wote wwaliopiga raia washuulikiwewa sheria.

Na uyo alieua askari akamatwe na kufikishwa mahakamani akajibu sababu ya mauaji.

Kwishney!
 
Hakuna mtu mwenye akili anaekubaliana na matukio yote mawili. Kuua mtu au kupiga raia.

Kwa vile mtuhumiwa alikuwa ameshakamatwa na polisi, hivyo hapakuwa sababu ya wanajeshi kuingia mtaani kupiga watu wasiokuwa na hatia hovyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…