Tuhuma za JWTZ kupiga raia huko Kawe: Tunaomba Waziri wa Ulinzi ajitokezee kukemea, kulaani, na kukataza jeshi kujichukulia sheria mkononi

Wewe umefurahia nini yeye kupoteza maisha?
Mkuu sifurahii, na pia kulikuwa na sababu ya mauaji. Sio kwamba dogo alitoka huko akaja tu kumvamia na kumuua.

Kulikuwa na sababu iliyopelekea dogo kuu. Lkn pia kuna sheria na mahakama ambavyo vipo kwa ajili ya kuendesha kesi za namna hiyo na baadae kutoa hukumu.

Wewe unahalalisha watu wasiohusika na ambao hawakuwepo hata eneo la tukio kuvamiwa na kupigwa hovyo, et kwa sababu ofisa wao ameuliwa na mtu wasiomfahamu!!
 
Siyo kaushamba,hawa ni washamba kabisa, nakumbuka miaka ya nyuma pale Mwenge kwenye magorofa waliyokuwa wanakaa hawa washamba walikuwa wanaweka mapazia ya viroba. Hawa walitakiwa wakae porini tu kwenye makambi yao.
Nimecheka sana 🤣🤣🤣
 
Habari zenu wanaJF wenzangu,

Ndugu wanaJF wenzangu, nafikiri wengi wetu hapa JF tumesikia, tumesoma na wengine kuona kile kinachosemekana kufanywa na jeshi letu, ambalo tumelipa jina la "Jeshi la Wananchi wa Tanzania.

Jeshi hilo tulilipa jina hilo kwa kuamini kwamba, jeshi hilo limeundwa kwa ajili ya kumlinda, na kumpigania mwananchi wa Tanzania.

Lakini pia liliundwa kwa ajili ya kuilinda mipaka ya Tanzania, pamoja na viongozi wa Tanzania akiwemo raisi wa nchi (ambae ni amiri jeshi wao mkuu) mawaziri, wakuu wa mikoa na viongozi wengine mbali mbali. Hilo ndio lilikuwa lengo la kuundwa kwa jeshi hilo, lkn pia kupewa jina hilo (JWTZ)

Sasa inashangaza sana jeshi ambalo lingewalinda na kuwapigania wananchi, ndio linageuka kuwa jeshi la kuwapiga hovyo wananchi, kuwatesa wananchi na hata wengine kuwauwa wananchi bila sababu za msingi.

Yes tunajua kwamba kila binadamu ana mapungufu yake, hivyo wapo wananchi wanaofanya makosa, au mambo mabaya kwa jeshi letu. Lakini kuna sheria na mahakama ambavyo vinaweza kutumika kuwaadhifu wale wanaofanya mambo mabaya kwa jeshi letu, na sio jeshi hilo kukimbilia tu kujichukulia sheria mkononi mpaka kupelekea maafa kama yaliotokea Kawe na kwengineko.

Malalamiko ya wananchi au raia dhidi ya jeshi hayakuanza leo, ila cha kushangaza badala ya kumalizwa kwa njia ya amani, ndio yanazidi kuongezeka kwa njia za kuchochewa na jeshi hilo hilo lililopewa dhamana ya kutulinda.

Kwa kilichotokea juzi huko Kawe, nafikiri viongozi wengi wa kiserikali wanalifahamu, lkn kwa vile pengine sio wahusika wakuu wa maswala ya kiusalama ndio maana hawahitaji kuliingilia swala hili.

Hivyo sisi wananchi tunamuomba waziri husika wa ulinzi mama yetu Stergomena Tax, pamoja na waziri wa mambo ya ndani brother Masauni waingilie kati swala hili kwa kuonya, kulaani na kutolea maelezo swala husika.

Msingoje mpaka raisi aje kulizungumzia mwenyewe, na wakati nyinyi kama mawaziri mmepewa dhamana ya kutulinda.

Kwa niaba ya wananchi wanyonge, ni mimi mpigania haki zao Mr Dudumizi wa somewhere in Kawe.
Walivyo wapumbavu wanasubiri habari hii ichapishwe Instagram, Facebook, na twitter ndio wajitokeze TANZANIA kuna upumbavu mwingi sana
 
Hakuna kiongozi yoyote anaweza kuwakemea ama kuwachukulia hatua yoyote hao wanajeshi, maana viongozi hawa wako madarakani kwa wizi ww kura, na hisani ya jeshi ndio inawafanya waendelee kukaa madarakani. Ingekuwa ni viongozi walioko madarakani kwa kura halali wangeweza kukemea, ama hata kuchukua hatua.

Hao wanajeshi tutawaona wa maana kama watapindua serekali hii isiyo na uhalali wa umma, na kuhakikisha tunapata katiba mpya na serekali halali.
 
Back
Top Bottom