Tuhuma za Kabendera dhidi ya Magufuli na ukimya wa Kikwete. Je, tuamini ni kweli?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Tuhuma za Erick Kabendera dhidi ya Marehemu Magufuli, ni nzito mno ikiwa ni pamoja na madai ya Kabendera kuwa Magufuli alitaka kumkamata Kikwete kwa tuhuma za kuhongwa fedha na mfanyabiashara mmoja ambae hakumtaja japo yupo anaehisiwa.

Katika hali ya kawaida, tulitarjie Kikwete ajitokeze hata kupitia mitandao na kusema jambo: sikuwa na ugomvi na Magufuli au vinginevyo.

Sasa ukimya huu wa JK tafsiri yake nini?

Je, ndio anamanisha silence means yes?

Binafsi naona huu ni mwanzo tu na kuna mengine yanakuja.

Tusubiri.
 
Tunatarajia Mfanyabiashara huyo atajitokeza hadharani kuthibitisha madai ya Kabendera
 
Kikwete aje kujibu nini..? Vyombo vya ulinzi vichunguze kupata ukweli hizo ni tuhuma kubwa kwa maana kama alikua hajui ndipo na yeye anapata mshangao sasa hivi. Yote yana wezekana kuwa kweli au isiwe kweli. Wenye mamlaka wafanye uchunguzi yakinifu
 
Mwendazake hata Shetani bado amemuweka pending kule jehanam. Kila akiangalia CV yake anamuogopa kuwa anaweza kumgeuzia kibao hata yeye mwenyewe.

Shetani anaogopa kuuliwa na Magufuli
 
Unasema hivyo kwa kuwa inadaiwa kuwa eti wewe ndiyo ulimchomea Erick Kabendera kwa Mwendazake. Naanaza kukubaliana na tuhuma hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…