Wamiliki wengi wa silaha zimegeuka mzigo kwao wapo waliojiua, walioua wenzi wao, ndugu, watoto, nk. Jiulize unao ulazima wa kumiliki silaha. Kama una tabia ya silaha achana na wazo la kumiliki silaha, bora uwe na bodigadi. Halafu ukitaka silaha nunua mpya achana na hizi used nyingi zina maagano yaani tayari zishaua so ukiwa nayo ni lazima tu utaua sababu tayari imebeba damu ilishasababisha mauaji,. Ni salama zaidi kuwa na bodigadi na walinzi binafsi nyumbani kuliko kumiliki silaha. Labda uwe na utulivu wa kutosha wa akili, lakini kama huna hasira au mke au mme ana hasira achana na hio kitu. Maana Hasira ni mlango wa sebuleni wa shetani mda wowote atakuvaa utaua. Utatoka jela kwa sababu unayo pesa lakini je hatia ya kuua utaifutaje damu ni muhuri wa moto aufutiki hadi kaburini.