DOKEZO Tuhuma za Siasa chafu "Law School of Tanzania" wahusika wajitokeze kuzijibu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Mkuu hiyo pesa hapo ni ada tu. Kumbuka wanafunzi hawa wanatoka all over Tanzania. Dar wanajitegemea kwa Kila kitu ikiwamo makazi na chakula. Ikumbukwe hiki chuo hakina hostel.

Vipi kuhusu vitabu na stationeries?

Vipi usafiri na field attachments?

Halafu yote hii inazimwa ni watu waliogeuka kuwa miungu.

Angalia Uzi huu pia kuihusu LST:

Napinga uteuzi wa Prof. Sifuni Mchome kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu
 
Law School ni eneo linalokwaza sana ktk taaluma.

Unahitajika kuwa kondoo haswaa ili uweze kupenya hapo.

Badala ya kuzalisha wanasheria, wao wanazima ndoto za wanasheria wa kesho

Shime waungwana kama hiki ni chuo cha umma, manyanyaso yao hayapaswi kufumbiwa macho.
 
Iwapo mwalimu aliingia darasani akafundisha na wanafunzi walikuwa darasani, kwanini paper iwe ngumu? Kuwa ngumu maana yake nini?
-kuingia darasani kwa mwalimu,na kufundisha haimaanishi lazima utafaulu mtihani, kwani hujawahi kusikia mitihani mgumu, iko juu ya kiwango?, read the law and understand the law, wengi hawasomi sheria na kuzielewa, mtu anajibu swali kwa kukopi section nzima? wakati lecturer anataka statutory interpretation, maswali ya Law school unakuta ni scenario ndefu uisome,uichambue,na uielewe na utoa legal opinion on that particular aspect, wengi hawaelewi maswali ya scenario
- kwa hiyo mwalimu akiingia darasani na wanafunzi walikuwepo darasani sio hoja justification ya kufaulu
 
Law School ni eneo linalokwaza sana ktk taaluma.

Unahitajika kuwa kondoo haswaa ili uweze kupenya hapo.

Badala ya kuzalisha wanasheria, wao wanazima ndoto za wanasheria wa kesho
umewahi kutazama matokeo ya nbaa?
 
Hayo ni madhara ya vyuo kuendekeza siasa. Mitihani hazina viwango, Walimu hawaja bobea sheria. Wanafunzi ni mapenzi tu. Mkifika Law School jamaa wana kaza.
Komaeni tu wakuu mta toboa.
 

Zingatia hakuna lalamiko la mtihani mgumu.

Zipo tashwishi hata za ukimwi kuendelea kusambazwa.



Ukondoo unaosemwa na mjumbe huyu unauelewa sawa sawa?
 
Sii kweli!, kwa kuanzia kuna kusoma kutafuta cheti cha kuhitimu ili upate ajira na kuna kusoma kutafuta elimu ili tuu kuelimika, kuna mamia ya watu wamesoma sheria na wanafanya shughuli nyingine tuu, wako very successiful bila kuhitaji kuwa wakili. Sio lazima kila mwenye LL.B awe wakili, wengine tumesoma LL.B ili tuu kuelimika na sio kusaka ajira. Ila kama unataka kuwa wakili ni lazima upite LST na ufaulu.
Kama walimu ni miungu watu kiasi hiki, ukimwi utakwisha kweli Tanzania hii?
What has this got to do with LST?. Pale wanaingia graduates only, mtu msomi utamvuliaje mtu na kumruhusu akuingilie kavu kavu hadi upate ukimwi?, unless useme miungu watu hawa pia ni wabakaji?.
"Hiki ni chuo cha umma, wenye dhamana hawawezi kuchagua kukaa kimya."
Naunga mkono hoja.
P
 
Hii ingewekwa kama certification ya ziada yani ukifanikiwa kuipata inakua na added advantage kama ilivyo kada za computer.

Iko CCNA, CEH, CISA na nyingine nyingi lakini mtu asipokua nazo haimyimi haki ya kutafuta na kupata ajira.

Kuieka ni lazima kua nayo ili upate ajira ndio shida ilianzia hapo kwa waswahili hii ni lazima igeuke kuwa urasimu na ukiritimba.

Umesoma una degree ya sheria lakini sasa inakuaje usiweze kuajiriwa hadi law school? Sio ni ushenzi huu.
 

Mkuu una maana kazi kama za kulima nyanya?

Napinga uteuzi wa Prof. Sifuni Mchome kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu

Bila cheti cha LST kama lawyer ni bure. Wapi utatambuliwa? Ndiyo zengwe lilipowekwa na wajuvi.
 
Ngoja nimwite Wakili msomi Pascal Mayalla aje atoe neno
Mkuu Selikavu , kwanza mimi sio Wakili Msomi, mimi ni Wakili Mtangazaji ambaye nimejikita kwenye human rights natetea bure kesi za ukiukwaji wa haki za binaadamu.

Kwa vile mimi nimeupata uwakili juzi kati wengi wanadhani LL.B yangu ni ya juzi hivyo mimi ni product ya LST!. Mimi ni wa longi nilihitimu sheria kabla ya sheria ya LST.
P
 
Binafsi naomba nisema yafuatayo kuhusu shule ya sheria Tanzania:

Mosi,
kutokana na uhitaji wa elimu ya kusoma kwa vitendo (Post-Graduate Diploma in Legal Practice) haikutakiwa kuwe na shule moja nchi nzima tena ambayo iko kwenye mji kama Dar es salaam. Walau hizi shule zingekuwepo kikanda ili kuwaepusha na kadhia wale wanafunzi wanaotoka mikoa ya mbali kuja kurudia mitihani Dar es Salaam. Mtoto anasafiri kutoka Tarime, hana hata mkopo halafu anakuja Dar es salaam kufanya mtihani akiwa na 50/50 kwamba hilo somo analorirudia atafuaulu au lah.

Pili, mbinu ya kumpima mwanafunzi (Mode of Assessment) siyo rafiki kabisa na haizingatia utaalamu wa kisaikolojia kwamba wanafunzi wana uelewa tofauti. Mtoto anasoma mwaka mzima halafu anapewa mitihani 24 ndani ya mwaka ambayo kama akifeli hata mmoja basi anaweza kupoteza zaidi hata ya miaka 2 anarudia tu kozi hiyo hiyo. Kikawaida tulitegemea kwenye elimu ya vitendo wanafunzi wapimwe kupitia kazi nyingine muhimu ambazo lazima ziwe na alama, kama PRESENTATIONS, GROUP ASSIGNMENTS, CLINICS + WORKSHOPS and INTERNSHIP WITH MARKS.

Sasa wanaitwa DIPLOMA IN LEGAL PRACTICE huku wakichukua ada ya zaidi ya milioni moja, ilhali vipimo vyote vinatolewa kupitia mitihani. Hii siyo sahihi, kwasababu hata mahakamani kwenyewe wanasheria huwa hatuviziani ila tunapewa muda wa kujiandaa. Sasa mtoto anakaa INTERNSHIP miezi zaidi ya sita huku akija kukaguliwa kihunihuni tu mara moja, bila kupewa alama yoyote ile ya muhimu. Kwanini hawa wanafunzi wasipangiwe hata miezi miwili-miwili kufanya kazi za lazima zenye alamu mahakama za mwanzo, mabaraza ya ardhi, mabaraza ya usuluhishi, dawati la jinsia ???

Jingine, ambalo nimeliona ni jambo la kipumbavu kufanywa na watu wanaojiita wasomi ni kitendo cha kutoa matokeo ya mitihani yote ya mwaka mzima ndani ya siku moja, baada ya mwaka mzima na miezi mitatu kupita. Kwanini matokeo ya ICA (Individual Continous Assessment), WPE (WRITTEN PRACTICAL EXAMINATION) na FINALS NON-CORE hayatolewi mapema, ili mwanafunzi ajue mbivu na mbichi na aweze kujipanga vizuri kwenye mitihani ya mwisho ??? Pia wawekewe utaratibu maalumu kabisa wa kuyarudia haya masomo wakati hata wako shule, hasa wiki moja baada ya kumaliza WPE. Wanafunzi wakipewa nafasi ya kurudia ICA wakiwa ndani ya mwaka wa masomo, basi DISCONTINUATION zitapungua mno.

Lingine muhimu ni kwamba LST, kuna mitihani ya WPE (Written Practical Examination) ambayo kwingineko duniani mwanafunzi huifanya kwa kufanya tafiti pamoja na majadiliano na wanafunzi wenzake, kisha baadae huenda kufanya huo mtihani. Ilhali sasa pale LST, wanafunzi wanafungiwa masaa manne (4) wakisoma mavitabu, bila kuruhusiwa kuzungumza halafu wanapewa saa moja kupumzika, ili warudi kufanya mtihani huohuo kwa masaa matatu. (It's just emotional debilitating)

Tatu, hili la kulazimisha kila anayesoma sheria awe wakili nadhani ni jambo la kishenzi ambalo lilifanywa kwa mihemko bila kufikiriwa. Miaka yote huko nyuma watu tuliajiriwa kama STATE ATTORNEYS bila hata kuwa wanasheria. Tulitakiwa tu tufanye INTERNSHIP miezi tisa kwa ATTORNEY GENERAL halafu tunaenda kufanya BAR-EXAMINATION kule Arusha. Kinachoshangaza ni kwamba wengi ambao hawakupita Law School wako vizuri kuliko hata hawa watoto wenu wa Mawasiliano nyuma kule.

Kubwa zaidi, wanasheria tuko kwenye nyanja kuu mbili ambazo ni LEGAL PRACTITIONER (ADVOCATES) na JURIST (LEGAL SCHOLARS/LEGAL RESEARCHERS). Hawa ni watu wawili tofauti na wanafanya kazi tofauti kabisa, sasa ukitaka kuwalazimisha wawe kitu kimoja utakuwa unapuyanga mno. Leo hii ushauri wa sheria wa JURIST unaweza kuwa una uzito kuliko hata ule wa ORDINARY LEGAL PRACTITIONER, kutokana na tafiti na ufahamu. Sasa kwenye nchi fulani ya kusadikika, wenyewe kwasababu hawana SPECIALIZATION basi wanalazimisha kila mtu awe wakili, kwamba hata JURIST haweza kutoa ushauri kama hana muhuri. Just Lackadaissical and Nonsensical....

Nne, mtaala wa shule ya sheria ni wa kizamani sana na hauwezi kumfanya mwanafunzi awe vizuri kwenye soko la kimataifa. Kuna baadhi ya masomo tulitegemea yafundishwe pale LST, lakini hayapo kwenye mtaala. Mfano, INTERNATIONAL COMMERCIAL ARBITRATION, INVESTMENT LAW, BASICS OF INTERNATIONAL ECONOMICS LAW/ INTERNATIONAL TRADE AND FINANCE LAW. Nchi haina wataalamu wa haya masomo, sisi tunakomaa kufundisha PROPABATE & ADMINISTRATION OF ESTATES, COMMERCIAL LAW, LEGAL ETHICS, HUMAN RIGHTS and ACCOUNTS FOR LAWYERS masomo ambayo vyuo vingi vinayafundisha na vinaweza kuyafundisha vizuri.

Kesi kubwa kama zile za makinikia, DOWANS, ESCROW n.k zinahitaji mwanasheria walau awe anajua masomo ya INTERNATIONAL COMMERCIAL ARBITRATION, ambapo anatakiwa aifahamu mikataba mikubwa BIT (Bilateral Investment Treaties), pamoja na taasisi muhumu kama ICSID, PIC, ICC. Lakini sisi tunakomaa kuwafelisha watoto masomo kama ACCOUNTS. Sijui hii nchi haina watu wenye akili kabisa. Mambo ya ajabu yanafanyika na hakuna hata anayestuka.

Tano, mradi wa LST tangu mwaka 2006 marehemu Prof. Mukoyogo aliupinga kweli kwasababu aliona hauna maana zaidi ya kuwatengenezea ulaji baadhi ya wataalamu wa pale University of Dar es Salaam. Hivi kweli, tuna uhakika kwamba haya masomo ya LST hayawezi kufundishwa vizuri kwenye vyuo ambavyo wanafunzi wanasoma wakiwa wanatafuta Shahada ya kwanza kweli ???

Jambo jingine ni kwamba wataalamu wengi wa pale LST wameamua kufanya biashara ya vitabu. Wanatunga mitihani ambayo majibu yake utayapata kama tu umenunua vitabu vyao. Hili nilishawahi kuambiwa nikathibitisha mwenyewe kwenye baadhi ya vitabu. Hii ni tabia ya kishezi ambayo inaumiza na kukwamisha wengine huku wengine wakipata ukwasi mkubwa. Mwanafunzi anataoa pesa nyingi za Ada lakini hivyo vitabu havipo maktaba, utavipata mpaka umfuate mwandishi mwenyewe na umlipe 50,000. Kwanini msiweke vitabu vingi kule maktaba wanafunzi wakavisoma ???

Sita, hivi inawezekanaje mwanafunzi ambaye amefauli vizuri shahada yake afeli vibaya kwa kiwango cha DISCONTINUE pale LST ??? Ina maana huyu mwanafunzi hafahamu kitu chochote kabisa ??? Lakini, kubwa zaidi ni hili la wanafunzi 600 kuanza pamoja, lakini wanaofaulu ni watu 30, huku nusu ingine ikiwa inafanya SUPPLEMENTARY au DISCONTINUED. Sijui kwanini hili haliwastui Majaji na Wizara. Watu hufeli, lakini siyo kwa kiwango hicho ambacho kinafanyika pale Law School.

Pia, pale pana rushwa sana ya ngono, kukomoana na kubadilishiana matokeo. Kuna jamaa niliwahi kuwa naye mahakamani aliwahi niambia kwamba kuna rafiki zake wanafundisha pale walimuahidi kwamba watamfaulisha, na kweli alifaulu vizuri hadi tukashangaa. Alikuwa na maswali hata kabla mitihani haijaanza. Nikasema HIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII...


TANZANIA HAKUNA KITU KINACHOFANYA KAZI VIZURI KUSEMA TUNAWEZA JIVUNIA...
 
Mkuu una maana kazi kama za kulima nyanya? Bila cheti cha LST kama lawyer ni bure. Wapi utatambuliwa? Ndiyo zengwe lilipowekwa na wajuvi.
Sii kweli, sii kila anayesoma sheria, anasoma ili awe wakili, kuna wanasheria kibao wamesoma sheria na sasa wanafanya shughuli nyingine sio za uwakili.

Mfano mzuri ni mimi, nimefanya LL.B ikaishia kabatini na sasa ni wakili na wala sikupita LST na wala silimi nyanya!.
P
 
Hivi wewe PASCO unaweza kumwandikia mtu ushauri wa kisheria na ukalipwa kama wakili bila muhuri ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…