Nimejikuta naanza kuchangia kwa kupiga hesabu kwenye jukwaa la siasa na sio jambo la kawaida.
1,570,000 * 265=.......
Kwa mwaka wana "intakes" ngapi? kwa hiyo hilo jibu hapo unaweza kulizidisha mara mbili!.
Hivi kwa majibu ya hiyo hesabu hapo juu nikisema hao jamaa wapo kwa ajili ya kuwatapeli watanzania nitakuwa nakosea?
Kwa hiyo idadi ya wanafunzi wanaofeli sioni sababu ya wazazi kupeleka watoto wao huko "Law School", hiyo elimu sasa imegeuzwa kufaulu kuwa sawa na kushinda bahati nasibu, suala la uwezo wa mwanafunzi halipo tena.
Hili lisipoangaliwa, huko mbele tuendako naiona idadi ya wanafunzi wanaosoma sheria vyuoni itaanza kupungua, hasa kama wakizingatia mbele ya safari mambo ndio yanakuwa magumu kiasi hicho.
Bora hiyo ada ya Law School wazazi wawape watoto wao wafanye mtaji wa biashara, sio mahangaiko mengi na bado mwisho wa siku uhakika wa ajira haupo, ni kupoteza muda tu.