Naona mmekuja kupiga siasa, na binafsi nadhani wengi mnahubiri msichokifahamu. Mtu yoyote makini huwezi kulinganisha kati ya shule ya sheria ya Tanzania iliyoanzishwa mwaka 2007 na ile ya Kenya iliyoanzishwa mwaka 1963. Utofauti, upo na mkubwa sana, kuanzia mbinu za ufundishaji (Pedagogical Methods), mbinu za kumpima mwanafunzi (Mode of Assessment) na Masomo yanayofundishwa.
The Law School of Kenya, mwanafunzi anapimwa kwa mfumo wa 20/20/60/. Ambapo Group Project Work anapewa alama 20, Oral Examination anapewa alama 20, na mitihani ya kuandika anapewa alama 60. The Law School of Tanzania, mwanafunzi anapimwa kwa mfumo wa 100, ambapo ni kuandika tu, mwanzo mwisho huku mwishoni akimaliza na Oral Examination. LST ni vurugu tupu na uhuni, siyo elimu ile.
Kama mtoto anafeli, basi afeli kiuhalali, lakini siyo kuhuni-huni tu. Lile la watu kulamba pesa na kugeuza watoto wetu miradi, hatulitaki kabisa.