Tuhuma za Ukabila: Wasukuma si Miongoni mwa Makabila yenye Ukabila, tatizo ndio walio wengi!

Tuhuma za Ukabila: Wasukuma si Miongoni mwa Makabila yenye Ukabila, tatizo ndio walio wengi!



Wanabodi,

Mnyonge Mnyongeni, Haki Yake Mpeni!, Wasukuma sii miongoni mwa makabila yenye ukabila m-baya!, hivyo mtu akiwa ni Msukuma kweli, kamwe hawezi kuwa na ubaguzi wa kikabila, kidini na kikanda, labda jinsia, na hili sio kosa lao, ni mfumo dume wa jamii za kiasili za kiafrika.

Declaration of Interest.
Mimi Paskali Mayalla ni Msukuma, na jina la Mayalla ni jina la ukoo toka kwa mababu na maana yake ni mtu aliyezaliwa wakati wa baa la njaa ( ukame, famine, drought), na sio njaa ya tumbo, au njaa ya shibe kama wengi walivyoaminishwa!, mimi binafsi japo ni Msukuma lakini sio mkabila, na huu ni uthibitisho wa jinsi ninavyopinga ukabila, hata kama ni ukabila wa Wasukuma na 'Wasukuma'.
Wito Kwa Bunge Letu Tukufu: Mkithibisha Hii Nepotism ya Ajabu na ...

Wasukuma Sio Wakabila.
Sisi Wasukuma sio wakabila wa ule ukabila m-baya kwa kufanya ubaguzi wa kikabila au kindugu, yaani undugunaization wa nepotism, Wasukuma ni watu poa sana, ndilo kabila linaloongoza kwa watu wachapa kazi, ndilo kabila linaloongoza kwa upendo, ndilo kabila linaloongoza kwa ukarimu, ndilo kabila linaloongoza kwa unyenyekevu, ndilo kabila linaloongoza kwa viongozi ambao they are "men of the people", yaani watu wa watu na down to earth. Hivyo ninavyoandika hapa simtetei Magufuli kwa vile ni Msukuma, namtetea kwa vile mambo mengine, wanamsingizia bure tuu huyu Msukuma wa watu!.
Rais Magufuli ni Simple, Genuine & Down To Earth-He is Simply A of the People...
Magufuli Kama Nyerere: Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'unyi, Ni ...
Pongezi Rais Wetu Magufuli Kwa Kuwa Mkweli Daima, Tuanzishwa The ...


Jee Magufuli Kweli ni Mkanda, Mdini na Mkabila?.
Hili naomba nilisilijibu ili nisiingilie uhuru wa mahakama, kwa sababu tayari kuna kesi iliyofunguliwa kuhusiana na tuhuma hizi ila nawaomba tuu tusimlaumu Magufuli kutokana na kauli zake.
Kanda ya Ziwa na kuongea kwa ukali: Ukali wa Rais Magufuli ni ...

Conclusion.
Naendelea kusisitiza kwa dhati ya moyo wangu, ukanda, ukabila na udini ni sumu katika taifa letu, katika kupigana na vita hivi, ukweli usemwe, na katika kuusema ukweli huo, haki itendeke, hata kama kuna mnyonge, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni!.

Tanzania ni yetu sote, kila mmoja wetu, ana wajibu wa kuhakisha Tanzania inapa ustawi na maendeleo kwa kujengwa, kulindwa na kustawishwa na sisi Watanzania wenyewe, and it can be done if kila mmoja wetu, will play his part, this is my part
Mungu Ibariki Tanzania.
Asanteni.

Wasalaam.

Paskali
 
Unatumia nguvu nyingi kumtetea MTU ambaye hawezi kujitetea. Kila tamko lina ukakasi. Kumpaka kwako rangi yeupe wakati yeye mweusi hakukusaidii.
 
Unatumia nguvu nyingi kumtetea MTU ambaye hawezi kujitetea. Kila tamko lina ukakasi. Kumpaka kwako rangi yeupe wakati yeye mweusi hakukusaidii.
Narudia tena n'a tena!paskali anautafuta udc kwa nguvu zote!inabidi rais amuonee butins amteu tu maana hakuna jinsi

Ova
 
wachaga mnajitaidi sana kupandisha nyuzi za kuwasema wasukuma wakati Tanzania nzima inajua ni kwa jinsi gani mliigawana nchi na kupeana kwa undugu sasa ni zamu ya wengine ni bora muwe wapole
 
Vyuma vimekaza Mkuu mwache huyu naye achakarike ili akumbukwe. Njaa mbaya sana Mkuu. Teuzi lazima uzisotee kwa kumsifia dikteta uchwara kwa nguvu zote.

Narudia tena n'a tena!paskali anautafuta udc kwa nguvu zote!inabidi rais amuonee butins amteu tu maana hakuna jinsi

Ova
 
Msukuma kuamua kesi dhidi ya wasukuma ni sawa na kesi ya nyani kumpelekea ngedere.

Hakujawi kutokea ukabila mzuri hata uupake rangi nzuri kiasi gani. Hata kipindi cha Nyerere kuwa na wanajeshi wengi kutoka Mara haikuwa sawa na haikuwa na maana kuwa watu wa Mara ndio wanafaa zaidi kuwa wanajeshi. Kila mtanzania awe na haki sawa bila upendeleo.Mbona leo hii kuna wanajeshi kibao kutoka kila kona ya nchi na wanafanya vizuri?

Mifano yako mingi uliyotoa haina tija kabisa. Kwa mfano umetolea mfano wa kuendeleza wamakonde na wanariadha kutoka jamii za wafugaji na wawindaji wa milimani eti kisa wengi wao wana historia ya kufanya vizuri kwenye maeneo hayo.

Mifano hii ni old fashioned ,kwa dhama hizi ambazo tunaamini any one can be anything he/she want as long as he/she works on it. Siku hizi kipaji sio kila kitu, watu wanaamini sana katika bidii na kujifunza, mengine yote yatakuja kama maji yanavyotiririka mtoni.

Hiyo mifano yako haifanyi kuwepo kwa ukabila/ukanda mzuri ilimradi kila mtu akipewa fursa akitia bidii anaweza kufanya lolote bila kujali anatokea wapi.

Nenda kajipange na wasukuma wenzio ndio urudi tena.
Kila mkutano wake wa kisiasa ni kusukuma mwanzo mwisho
 
Rais huyu anaiangamiza hii nchi,anaichafua nchi hii,anakiuka haki za binaadamu kwa kiwango kikubwa kuliko Rais yoyote katika historia ya nchi ni mkabila,mdini,ni Rais wa visasi kwa wapinzani wake wa kisiasa,anaingiza nchi hii katika umasikini mkubwa,Ni Rais ambaye upeo wake wa kufahamu uhalisia,uko mbali sana na ustaarabu wa binaadamu,nakupa mfano mdogo tu anaachilia kila kona ya Dar/Tanga watu kuvunjiwa nyumba zao,ati sababu wanajenga mabondeni,ukitizama sehemu hizo zote ni ngome za upinzani,hivyo mbona hatusikii mwanza ,shinyanga,Geita,chato nk watu kuvunjiwa wanaojenga mabondeni?na katika sehemu hizi kuna sehemu nyingi watu wamejenga mabondeni,tena tuna ushahidi mkubwa wa haya tunayoyasema,asilimia kubwa ya serikali yake anachukua jamaa zake,hajapatapo kutokea rais wa namna hii Tanzania,anatetea uvunjifu wa sheria,kwenye veti,katiba,sheria zabunge,usalama wa raia nk,raia wanauwawa kila leo bill hatia,ukisema unawekwa ndani,tujiulize tukienda namna hii tutafika?.

Rais Magufuli kamwe hana ukabila wala udini au ukanda. Nusu ya Watanzania ni Wasukuma(note Mnyamwezi ni Msukuma kwani lugha ni moja), 1963 idadi ya watu Tanzania walikuwa million tisa(9,000,000) na kati ya hawa million tatu walikuwa ni Wasukuma kwa hiyo kwa sasa wa Sukuma ni kama million ishirini (20,000,000) and this is the reality, ni wengi lakini hawasikiki kama Wanyakyusa Wahaya Wachagga Wakuria!! Go through our history books. Mungu Ibariki Tanzania.
 
Rais Magufuli kamwe hana ukabila wala udini au ukanda. Nusu ya Watanzania ni Wasukuma(note Mnyamwezi ni Msukuma kwani lugha ni moja), 1963 idadi ya watu Tanzania walikuwa million tisa(9,000,000) na kati ya hawa million tatu walikuwa ni Wasukuma kwa hiyo kwa sasa wa Sukuma ni kama million ishirini (20,000,000) and this is the reality, ni wengi lakini hawasikiki kama Wanyakyusa Wahaya Wachagga Wakuria!! Go through our history books. Mungu Ibariki Tanzania.

Wakati walipopewa na wasukuma viti vya ubunge, Maswa mashariki na magharibi, Kisesa, Bukombe, Biharamuro ,ukerewe, Ilemela na nyamagana, kote usukumani ukabila wa wasukuma ndani ya Chadema hawakuuona.Leo ccm kafanya hivyo kwa kupewa viti vya ubunge.poor Chadema.wasukuma tuna hasira na nyie Kama njaa subirini 2020
 
Haitokei hivi hivi tu hata kama wasukuma ni wengi. Kwasababu si lazima apitishwe na chama? Kumbuka mgombea binafsi bado haikubaliwi kikatiba.

Sasa wewe unadhani muda wote huo ni kwasababu walikuwa hawataki au walishikiwa chini na sera za mwalimu kuhusu makabila makubwa? Kwa miaka yote toka uhuru , unadhani hawa kuwepo ndani ya ccm wenye uwezo wa kuongoza nchi?

Think think. Usitafute easy solution out!
Mkuu hawa ni wengi,wala si kosa lao kuwa wengi.Mambo ya watu wachache kuwaamlia wengi sio demokrasia ya kweli,lakini hao wengi haikatazi kutafuta nani nje yao.
Mwalimu Nyerere yeye hakuwahi kuwa mwanademokrasia yeye alikuwa mkombozi wa kuondoa wazungu na kutawala mweusi.Kumleta Nyerere kwa hili hali yeye alitawala miaka 27 lakini waliomfuata akawapangia miaka kumi ule ulikuwa ubinafsi.
 
Wakati walipopewa na wasukuma viti vya ubunge, Maswa mashariki na magharibi, Kisesa, Bukombe, Biharamuro ,ukerewe, Ilemela na nyamagana, kote usukumani ukabila wa wasukuma ndani ya Chadema hawakuuona.Leo ccm kafanya hivyo kwa kupewa viti vya ubunge.poor Chadema.wasukuma tuna hasira na nyie Kama njaa subirini 2020

Hasira hasara! Achana na mawazo kama hayo, Mungu tu ndiye afanye kazi kwani ukisema hivyo na ukiwa na nia mbaya na taifa, Mungu ana mijeleji yake and He uses them at will and at the right time. Jifunze kutoka kwa Goliati na David na hapo uombe huruma ya Mungu kwa mawazo yako ya chuki kwa makabila mengine 125. Tunajua Wasukuma kabisa hawana ukabila.
 
Back
Top Bottom