Umesoma bandiko hili mwanzo?.
Kulisaidia
"
Ukabila Mzuri Katika Uteuzi.
Kufuatia kabila la Wasukuma kuwa ndilo kabila kubwa kabisa nchini Tanzania, ndilo kabila lenye watu wengi zaidi, hivyo automatically, tukifuata principals of proportionality, Wasukuma ni lazima wawe wengi kila mahali, hii ni halali yao na sio upendeleo!.
Ukitokea wewe ni mteuzi, ukaletewa majina matatu wote wenye sifa sawa na mmoja wao ni Msukuma, jee utaogopa kumteua huyo Msukuma kwa sababu ya kuchelea utaonekana ni mkabila?, zikitokea nafasi, halafu kati ya walioomba wote, wenye sifa zaidi ni Wasukuma, then let it be, hata Wasukuma wakijazana sana, as long as ndio wenye sifa, then huu ni ukabila mzuri, hivyo natoa wito kwa JPM, endelea kuteua Wasukuma, wajaze kila mahali as long as ni watu wenye sifa na ni wachapa kazi, then wewe teua tuu, wanaosema waache waseme, watasema mchana msiku watalala.
Na ikitokea wewe ni Msukuma, ukakuta kuna home boy wako alishateuliwa na mtangulizi wako, inapotokea anazingiziwa au kutuhumiwa, kuna ubaya kumsaidia kama hapa?
Kumbe ni Uongo, Uzushi, Fitna, Majungu, Wivu na Kijicho Dhidi ya ...
Ukabila Mbaya Katika Uteuzi.
Ikitokea kuna nafasi za uteuzi, then ukaamua kwa makusudi kutafuta mtu wa kabila lako, ambaye hana sifa, lakini kwa vile ni kabila lako, unampandisha haraka haraka ili kumjengea sifa, kisha unamteua. Huu ni ukabila mbaya!.
Au kunatokea nafasi ya uteuzi, wewe unatafuta mtu wa kabila lako, ukimkosa, unakasirika, unaamua nafasi hiyo huteui mtu, bali unaikaimisha na kusubiria hadi mtu wa kabila lako atokee!. Huu ni ukabila mbaya.
Facts Kuhusu Dominant Tribes. Wasukuma The Biggest Tribe, The Best, The Kindest!
Pamoja na kuwepo kwa ukabila mzuri na ukabila mbaya, kuna kitu kinaitwa dorminabt tribes, hii ni fact, hatuwezi kuipuuzia, Wasukuma ndilo kabila kubwa kuliko makabila yote nchini Tanzania, na wamesambaa katika mikoa mingi kuliko kabila jingine lolote, na ukiwemo Mkoa mmoja tuu Tanzania nzima, ambao mkoa wote ni kabila moja tuu, Mkoa wa Shinyanga, hakuna mkoa mwingine wowote ambao ni mkoa mzima una watu wa kabila moja!.
Sababu ya Wasukuma Kuwa Wengi Zaidi Kuliko Makabila Yote.
Wingi wa watu unatokana na kitu kinachoitwa population growth, Wasukuma ndio wanaoongoza kwa highest population growth, sisi nyumbani kwetu kwa mama yangu tumezaliwa 8!, hivyo mwanamke wa Kisukuma kuzaa watoto 10-12 its normal, na hapa mama hakuwa peke yake!. Sababu ya uwepo wa chakula bora, kingi na cha kutosha, ndio maana unaiona miili ya Wasukuma sio miili ya njaa njaa, wanaume wa Kisukuma wana nguvu sana za ku service zaidi ya mwanamke mmoja, elimu duni maeneo mengi, kuoa wanawake wengi, kuzaa watoto wengi bado ni sifa kwa Wasukuma, mimi mwenyewe ninao watoto 8 na sio mwisho!, na kufuatia kuwepo kwa lishe bora, rate ya procreation iko juu, watoto wanazaliwa sana, infant mortality rate iko chini, watoto hawa hawafi, deathrate Usukumani iko low, na kuishi maisha marefu kutokana na kula vyakula vya asili, kunafanya Wasukuma kuishi maisha marefu sana. Ingefanywa sensa ya wazee Tanzania, tungekuta ni Wasukuma pia ndio wanaoongoza kwa maisha marefu!
Kati ya watu milioni 50 walio Tanzania, Wasukuma ni milioni 10, hivyo hii ni asilimia 20% ya Watanzania wote, hivyo tungefuata haki bin haki kwenye kila ofisi yenye watu watano, mmoja ilipaswa lazima awe Msukuma, hivyo piga hesabu ya kila sekta ulinganishe na idadi ya Wasukuma waliopaswa kuwepo, mkimuita jamaa ni mkabila kwa sababu tuu ya kuteua Wasukuma wawili watatu, huko kutakuwa ni kumuonea".
P