Tuhuma za Ukabila: Wasukuma si Miongoni mwa Makabila yenye Ukabila, tatizo ndio walio wengi!

Tuhuma za Ukabila: Wasukuma si Miongoni mwa Makabila yenye Ukabila, tatizo ndio walio wengi!

Wanabodi,

Mnyonge Mnyongeni, Haki Yake Mpeni!, Wasukuma sii miongoni mwa makabila yenye ukabila m-baya!, hivyo mtu akiwa ni Msukuma kweli, kamwe hawezi kuwa na ubaguzi wa kikabila, kidini na kikanda, labda jinsia, na hili sio kosa lao, ni mfumo dume wa jamii za kiasili za kiafrika.

Declaration of Interest.
Mimi Paskali Mayalla ni Msukuma, na jina la Mayalla ni jina la ukoo toka kwa mababu na maana yake ni mtu aliyezaliwa wakati wa baa la njaa ( ukame, famine, drought), na sio njaa ya tumbo, au njaa ya shibe kama wengi walivyoaminishwa!, mimi binafsi japo ni Msukuma lakini sio mkabila, na huu ni uthibitisho wa jinsi ninavyopinga ukabila, hata kama ni ukabila wa Wasukuma na 'Wasukuma'.
Wito Kwa Bunge Letu Tukufu: Mkithibisha Hii Nepotism ya Ajabu na ...

Wasukuma Sio Wakabila.
Sisi Wasukuma sio wakabila wa ule ukabila m-baya kwa kufanya ubaguzi wa kikabila au kindugu, yaani undugunaization wa nepotism, Wasukuma ni watu poa sana, ndilo kabila linaloongoza kwa watu wachapa kazi, ndilo kabila linaloongoza kwa upendo, ndilo kabila linaloongoza kwa ukarimu, ndilo kabila linaloongoza kwa unyenyekevu, ndilo kabila linaloongoza kwa viongozi ambao they are "men of the people", yaani watu wa watu na down to earth. Hivyo ninavyoandika hapa simtetei Magufuli kwa vile ni Msukuma, namtetea kwa vile mambo mengine, wanamsingizia bure tuu huyu Msukuma wa watu!.
Rais Magufuli ni Simple, Genuine & Down To Earth-He is Simply A of the People...
Magufuli Kama Nyerere: Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'unyi, Ni ...
Pongezi Rais Wetu Magufuli Kwa Kuwa Mkweli Daima, Tuanzishwa The ...

Jee Magufuli Kweli ni Mkanda, Mdini na Mkabila?.

Hili naomba nilisilijibu ili nisiingilie uhuru wa mahakama, kwa sababu tayari kuna kesi iliyofunguliwa kuhusiana na tuhuma hizi ila nawaomba tuu tusimlaumu Magufuli kutokana na kauli zake.
Kanda ya Ziwa na kuongea kwa ukali: Ukali wa Rais Magufuli ni ...

Conclusion.

Naendelea kusisitiza kwa dhati ya moyo wangu, ukanda, ukabila na udini ni sumu katika taifa letu, katika kupigana na vita hivi, ukweli usemwe, na katika kuusema ukweli huo, haki itendeke, hata kama kuna mnyonge, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni!.

Tanzania ni yetu sote, kila mmoja wetu, ana wajibu wa kuhakisha Tanzania inapa ustawi na maendeleo kwa kujengwa, kulindwa na kustawishwa na sisi Watanzania wenyewe, and it can be done if kila mmoja wetu, will play his part, this is my part
Mungu Ibariki Tanzania.
Asanteni.

Wasalaam.

Paskali
Mayalla acha upotoshaji. Wasukuma ni "wabaguzi" kama makabila mengine.Ushahidi upo.
1.Ubaguzi wenyewe kwa wenyewe.
Kati ya Wanyantuzu na wasukuma wengine. Wanyantuzu huwaona wengine "wajinga" kwa kuwaita "babuli bha ng'hweli" -wajinga wa magharibi(Bariadi ipo mashariki) na wasukuma wengine wapo magharibi.
2.Ni ngumu mtu wa kabila tofauti na Ntuzu kuendesha biashara na kufanikiwa Bariadi (miaka kadhaa nyuma). Hujuma na vikwazo ilikuwa kawaida.
3.Kuna msemo wa "likabila" ambao huitwa wasio wasukuma. Hadi miaka ya karibuni ilikuwa vigumu kujichanganya nao bila kuhisi "ugeni"
NB.Magufuli si msukuma bali kazaliwa na kulelewa usukumani. Ni mhamiaji haramu japo anaongea kisukuma.Ni mhutu! Ndo maana matendo na tabia ni za ki-Nkurunzinza!
 
Niongezee nikuwa naangalia data

  1. Brela: Biashara nyingi zilizopo wasukuama hawako hata karibu ya kuongoza kaangalie registration pale.
  2. CPA. Yaani certified Public Accounting wa Tanzania hadi wapare ni wengi kuliko wasukuma!
  3. Advocates: Hawa ni certified attorneys yaani hata watu wa Mara, wahaya ni wengi kuliko wasukuma
  4. Professors: Walimu wa vyuo wahaya na wachagga, na wanyaksusa wanaongoza
  5. wafanyabiashara wadodo wadogo au Machinga hadi watu wa pemba, watu wa kusini ni wengi kuliko wasukuma
  6. Viwanda: wahindi na wahamiaji wanaongoza
  7. Media: Vyombo miliki vya wahaya na wachagga ni vingi kuliko wasukuma
Kwenye siasa wasukuma ni wengi kidogo zaidi maana wana wabunge zaidi lakini huwezi kusema ni dominant!. Wasukuma au wahaya ni dominant kwenye lipi wame dominate wapi kwenye idara au sehemu gani ya uchumi. Hata kwenye kilimo ambako ndiyo wengi wapo nimeangalia kilimo cha Moshi, Tanga, Manyara kinazidi usukumani na mikoa yote, Mikoa ya Mbeya kule wanalima kuliko usukumani. Hivyo sio kweli kwamba tuna dominant kabila Tanzania hakuna. Kenya mfano kwenye siasa, biashara, utajiri kote huko ni wakikuyu kasoro elimu ni Luo
 
Kils kabila lina ikabila tu isipokuwa labda watu wa pwani

Nimezaliwa isukumani na nimekulia usukumani japo wasukuma hawana sana mambo ya kikabila sana tofauti na maeneo mengne zaidi huwa yanapandikizwa na viongozi wa juu

mfano unaweza gombea ubunge ukashangaa wanaeneza propaganda kwamba wewe ni kabila fulani so wasikupigie kura
Mmasai akigombea ubunge Newala atapata?.
 
Hivi wewe jamaa unaona fahari gani kuzungumzia ukabila ??? Yaani kabisa unajitutumua unaleta hoja za makabila Tanzania ya leo hii.

Mijadala kama hii huwa haishi vizuri, na wewe kama mtu mwenye ufahamu nilitegemea ungekuwa ushalifahamu hili mapema.

Yaani umefungua kabisa na uzi wa kikabila kisa tu kujenga hoja za kisiasa. Sijui wasomi wetu mna matatizo gani.
 
Wasukuma halisi ni kabila la watu watii sana na wanyenyekevu, wanaishi communal life mpaka kesho, they are not selfish, they're selfless hadi leo hadi kesho, vijijini wanakula sahani moja. Land ilikuwa ya wote the entire community hivyo it was easy kukubaliana na kila wazo la Mwalimu Nyerere after all, Wasukuma sio very industrious, pamoja na utajiri mkubwa wa n'gombe, hawakujijenga kisasa, vijumba vya hovyo hovyo, na hawana mazao ya kudumu hivyo it was easy ku abandon kila kitu na kuhamia kijiji cha ujamaa, sisi kwetu tuliisha jenga nyumba ya block ya bati, tukagoma kuhama, tukatengwa, babu alipochomoka, Bibi akahamia mjini kwa wanae tukahama bushi jumla.

Wachagga na Wahaya, ni selfish tribes, kila mtu anapakuliwa chakula sahani yake au bakuli lake hivyo no sharing. Kule hakuna communal land, kila ukoo na kihamba chake, na kufuatia zao la kahawa ndio the biggest cash crop, wale ni industrious, hivyo waliendelea wakajenga nyumba za maana, hivyo walikubali kuanzisha vijiji vya ujamaa Kwa lazima lakini walimgomea Mwalimu kuhama, kata kata, na kiukweli enzi za Mwalimu, Wachagga na Wahaya waliisoma sana number.

P
Mkuu sifikiri kama sababu ulizoweka hapa kuhusu kutoanzishwa vijiji vya ujamaa Kilimanjaro au Bukoba ni sahihi; labda kama unajibu ili ukubaliane na unayemjibu. Kuna mtu walifungua uzi kwenye hii kitu.

Hivi kweli kila mtu akitumia sahani yake wakati wa kula ni kuwa selfish?? Mbona ndo mijini majumbani wanafanya hivo? Kuhusu viamba mbona mjini kila mtu ana kiwanja chake na kuna maeneo ya wazi kwa watu wote? Ndo ilivyo huko vijijini kwenye jamii hizo kila mtu ana kihamba chake lakini yapo maeneo ya wazi (communal land) kwa watu wote mfano kuchungia ngombe. Kama yanayofanywa mjini unayaona sio kuwa selfish basi hizi jamii kwa muktadha wa hoja yako hapo juu sio selfish.
 
Wanabodi,

Mnyonge Mnyongeni, Haki Yake Mpeni!, Wasukuma sii miongoni mwa makabila yenye ukabila m-baya!, hivyo mtu akiwa ni Msukuma kweli, kamwe hawezi kuwa na ubaguzi wa kikabila, kidini na kikanda, labda jinsia, na hili sio kosa lao, ni mfumo dume wa jamii za kiasili za kiafrika.

Declaration of Interest.
Mimi Paskali Mayalla ni Msukuma, na jina la Mayalla ni jina la ukoo toka kwa mababu na maana yake ni mtu aliyezaliwa wakati wa baa la njaa ( ukame, famine, drought), na sio njaa ya tumbo, au njaa ya shibe kama wengi walivyoaminishwa!, mimi binafsi japo ni Msukuma lakini sio mkabila, na huu ni uthibitisho wa jinsi ninavyopinga ukabila, hata kama ni ukabila wa Wasukuma na 'Wasukuma'.
Wito Kwa Bunge Letu Tukufu: Mkithibisha Hii Nepotism ya Ajabu na ...

Wasukuma Sio Wakabila.
Sisi Wasukuma sio wakabila wa ule ukabila m-baya kwa kufanya ubaguzi wa kikabila au kindugu, yaani undugunaization wa nepotism, Wasukuma ni watu poa sana, ndilo kabila linaloongoza kwa watu wachapa kazi, ndilo kabila linaloongoza kwa upendo, ndilo kabila linaloongoza kwa ukarimu, ndilo kabila linaloongoza kwa unyenyekevu, ndilo kabila linaloongoza kwa viongozi ambao they are "men of the people", yaani watu wa watu na down to earth. Hivyo ninavyoandika hapa simtetei Magufuli kwa vile ni Msukuma, namtetea kwa vile mambo mengine, wanamsingizia bure tuu huyu Msukuma wa watu!.
Rais Magufuli ni Simple, Genuine & Down To Earth-He is Simply A of the People...
Magufuli Kama Nyerere: Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'unyi, Ni ...
Pongezi Rais Wetu Magufuli Kwa Kuwa Mkweli Daima, Tuanzishwa The ...

Jee Magufuli Kweli ni Mkanda, Mdini na Mkabila?.

Hili naomba nilisilijibu ili nisiingilie uhuru wa mahakama, kwa sababu tayari kuna kesi iliyofunguliwa kuhusiana na tuhuma hizi ila nawaomba tuu tusimlaumu Magufuli kutokana na kauli zake.
Kanda ya Ziwa na kuongea kwa ukali: Ukali wa Rais Magufuli ni ...

Conclusion.

Naendelea kusisitiza kwa dhati ya moyo wangu, ukanda, ukabila na udini ni sumu katika taifa letu, katika kupigana na vita hivi, ukweli usemwe, na katika kuusema ukweli huo, haki itendeke, hata kama kuna mnyonge, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni!.

Tanzania ni yetu sote, kila mmoja wetu, ana wajibu wa kuhakisha Tanzania inapa ustawi na maendeleo kwa kujengwa, kulindwa na kustawishwa na sisi Watanzania wenyewe, and it can be done if kila mmoja wetu, will play his part, this is my part
Mungu Ibariki Tanzania.
Asanteni.

Wasalaam.

Paskali

Pascal Mayalla,
Kwani Magufuli ni Msukuma asili au wa kuja? Kama ni Msukuma-asili niambie asili yake wapi? Halafu nitakwambia aina ya watu wanaojiita wasukuma hata kama si wa asili.

Wasukuma-asili wengi ukikutana nao faragha na kuwauliza kama Magufuli ni Msukuma utasikia majibu mbalimbali. Kuna kitu kimoja wote wanakubaliana: HAKUNA Msukuma wa aina ya ukali, ukatili, kiburi, na ujuaji kama Magufuli.

Ni kweli Wasukuma si wabaguzi kwa asili. Na wala Si wakatili na wenye kiburi. Wengi ni wapole, wanyenyekevu, wakarimu na wenye upendo kwa watu hata wasiowajua au kukubaliana nao. Wasukuma-asili hawanaga visasi.

Hata hivyo kutokana na ukubwa wa kabila hili, kuna vikabila vidogo vya kanda ya ziwa na baadhi toka nchi jirani vilivyomezwa na kujiita "wasukuma" ili kupata unafuu wa kujichanganya na kabila kubwa. Hawa asili yao yaweza kuwa mwingine japo wanaongea Kisukuma safi na hata kufuata mila na desturi zote za wasukuma-asili.

Siwezi kusema kwa hakika aina ya Msukuma aliyo nayo Magufuli, japo kwa anayewajua vizuri Wasukuma halisi, ni vigumu kumshawishi kama Magufuli ni Msukuma-asili.

Labda niseme hivi: Magufuli ama kawainua au kawahatibia kabisa Wasukuma-asili. Wengi wanaowajua vizuri kama wanyenyekevu wapole, na wakarimu, watakuwa wamebadilishwa kabisa kimtazamo na Magufuli huyu. Lakini pia wale waliodhani
 
Mkuu Paskali una-instigate uhutu na ututsi katika nchi hii. Please stop this. Haisaidii chochote, watanzania hatutakubali kuona watu wanajaribu kujikuza over others. Take it from me, hatutakuwa tayari kabila moja lijitukuze at the expense ya makabila mengine hapa Tanzania. Kabila la wasonjo ni dogo lakini likiona kuna ndivyo sivyo kwa minajili ya ukabila litafight hadi mwisho. Be composed when writing to mass.
Ndugu Jorojik, Thank you very much kwa ukweli ulituwekea hapa. Ndugu Pascal anaendelea kujivunjia hadhi na heshima, japokuwa ni mwandishi mzuri na mwenye maono mazuri ya kisiasa, lakini naona amejiunga na kundi linalosemekana lina mipango ya kutuletea siasa za kiKENYA nchini kwetu.

Ndugu Pascal yumo kwenye siasa za kidini na kikabila, hili jambo limenishtusha na kunisonesha sana, i was a great follower of his writings, but now am very disappointed.

Ninamuombea mungu amrudishe kwenye fikra za kizalendo na amuepushe na ukabila na udini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu Pascal, I truly hope unasome post zote katika uzi huu.

JEE huoni kama umetukosea sana Watanzania kwa kuutukuza ukabila na udini?

JEE huoni kama kuna wengi hapa JF walikuwa wapenzi wa michango yako mizuri na post zako nyingi zilizokuwa na mafunzo, ukweli na upendo.

I believe you need to sit down na kutafakari na ujirekebishe.

Ndugu Ukabila hauna maendeleo wala faida, nadhani hakuna anayefaidika kwa ukabila , it has never put any food in your plate nor supported your family.

Ndugu tuangalie yaliyotokea Somalia, hii ni nchi yenye watu wa Lugha Moja, dini moja tena madhehebu moja, lakini kilichoiteketeza somalia ni ukabila.

Tusisahau yaliyotokea Rwanda, Burindi, Kenya, Central Africa Republic, Myanmar na yanayo endelea leo India, bila kusahau Iraq na Syria.

Jee utafurahia hayo yakitokea Tanzania?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu Jorojik, Thank you very much kwa ukweli ulituwekea hapa. Ndugu Pascal anaendelea kujivunjia hadhi na heshima, japokuwa ni mwandishi mzuri na mwenye maono mazuri ya kisiasa, lakini naona amejiunga na kundi linalosemekana lina mipango ya kutuletea siasa za kiKENYA nchini kwetu.

Ndugu Pascal yumo kwenye siasa za kidini na kikabila, hili jambo limenishtusha na kunisonesha sana, i was a great follower of his writings, but now am very disappointed.

Ninamuombea mungu amrudishe kwenye fikra za kizalendo na amuepushe na ukabila na udini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kiukweli Pascal huwa ananisikitisha kwa posts zake za kikabila na ukanda. Sijui anajaribu kuleta ujumbe gani kwa Taifa?! Wacha tuangalie.
 
Pascal Mayalla,
Kwani Magufuli ni Msukuma asili au wa kuja? Kama ni Msukuma-asili niambie asili yake wapi? Halafu nitakwambia aina ya watu wanaojiita wasukuma hata kama si wa asili.

Wasukuma-asili wengi ukikutana nao faragha na kuwauliza kama Magufuli ni Msukuma utasikia majibu mbalimbali. Kuna kitu kimoja wote wanakubaliana: HAKUNA Msukuma wa aina ya ukali, ukatili, kiburi, na ujuaji kama Magufuli.

Ni kweli Wasukuma si wabaguzi kwa asili. Na wala Si wakatili na wenye kiburi. Wengi ni wapole, wanyenyekevu, wakarimu na wenye upendo kwa watu hata wasiowajua au kukubaliana nao. Wasukuma-asili hawanaga visasi.

Hata hivyo kutokana na ukubwa wa kabila hili, kuna vikabila vidogo vya kanda ya ziwa na baadhi toka nchi jirani vilivyomezwa na kujiita "wasukuma" ili kupata unafuu wa kujichanganya na kabila kubwa. Hawa asili yao yaweza kuwa mwingine japo wanaongea Kisukuma safi na hata kufuata mila na desturi zote za wasukuma-asili.

Siwezi kusema kwa hakika aina ya Msukuma aliyo nayo Magufuli, japo kwa anayewajua vizuri Wasukuma halisi, ni vigumu kumshawishi kama Magufuli ni Msukuma-asili.

Labda niseme hivi: Magufuli ama kawainua au kawahatibia kabisa Wasukuma-asili. Wengi wanaowajua vizuri kama wanyenyekevu wapole, na wakarimu, watakuwa wamebadilishwa kabisa kimtazamo na Magufuli huyu. Lakini pia wale waliodhani
Mkuu Facts First usemayo ni facts na hao Wasukuma unaowazungumzia wewe ndio Msukuma mimi, ila karibu pande hizi
P
 
Tanzania hakuna majority tribes . Wasukuma ndiyo wengi zaidi lakini ni 16% tu ya Watanzania.


Facts Kuhusu Dominant Tribes. Wasukuma The Biggest Tribe, The Best, The Kindest!
Wasukuma ndilo kabila kubwa kuliko makabila yote nchini Tanzania, na wamesambaa katika mikoa mingi kuliko kabila jingine lolote,

Hapo juu sio kweli Wachagga wamesambaa kuliko wasukuma kwasababu ya kuwa wengi ni wafanyabiashara. Nenda mikoa ya Mbeya, Iringa, Lindi utakuta wachagga wengi kuliko wasukuma. wasukuma wengi wanaenda mikoani kikazi zaidi. Ingawa kwa wingi wasukuma wanaongoza halafu wanyamwezi na wachagga wanafuata. Kiuchumi kwa familia wachaga namba moja kwa mbali wanafuata na groups nyingine wapare wako wachache lakini kwenye level ya familia wanamaendeleo pengine kuzidi hata wachagga ingawa hawaongelewi sana. Maendeleo ya upareni na uchagani ni sawa. lakini kiuchumi vilevile group ya kwanza ni wahamiaji hasa kutoka India miaka ya 1950's wameshikilia viwanda na biashara nyingi, wapemba ambao ni watu wa kisiwa cha pemba nao wapo juu sana kiuchumi.


Kusambaa kwa Wachaga ni kufanya biashara na si wengi kubali. Wasukuma wameenea kila mahala hadi Zambia. Wasukuma ni matajiri wa rasilimali mfano, ngòmbe, ardhi kwa maana ya kilimo, madini, uvuvi na chakula. Nenda Zanzibar ni wakulima wazuri wa mpunga. Wachaga mtu mmoja akiwa na uwezo familia nzima inaishia kwake. Wakati wasukuma kila mtoto katika familia uwezeshwa kuwa na mifugo na mashamba yake. Wasukuma si watu wa kujionesha na kujitangaza, pia majina yao ni mengi hayajirudii kama ya wachaga mfano Lyimo, Urassa, Chuwa na kadhalika. Hivyo majina haya kuwa common ni rahisi kujua hapa kuna mchaga ndo maana unahisi wachaga wengi. Wachaga wanakisiwa kuwa 1.2 Million wakati wasukuma ni kati ya Million 8 hadi 10. Familia za kisukuma si masikini kama unavyodhani bali wanapenda kuishi maisha ya kimila zaidi si modern life. Wakiamua kuuza mifugo yao nadhani utatambua ni kiasi gani wanauchumi mzuri. Wengi ni wafanya biashara za madini mikoa inayokaliwa na wasukuma wana madini mengi mbali na uvuvi. Ardhi kubwa. Ni tofauti na uchagani kuna shida ya ardhi familia moja wanakusanyika katika plot moja, hii ni tofauti na usukumani kila mtoto anapewa ardhi na mifugo yake.
 
Nimefanya kazi na wasukuma sehemu nyingi. Sijawahi kuona watu wenye ukabila kama wasukuma, wana upendeleo wa waziwazi na hawana hata aibu. Kuna idara moja naifahamu walijazana wenyewe, hata vikao wakawa wanaongoza kwa lugha ya kisukuma. Nakiri kuwa wapo wasukuma baadhi ambao ni smart kichwani, lakini majority ya hawa wanaopendelewa ni makinikia tu! Hadi mtu unajiuliza huyu kafikaje hapa?

Kwahiyo Pascal Mayalla hoja yako ya kutetea wasukuma wenzio haina mashiko, ninyi ni makaburu tu! Huwezi kuniambia katika nchi yenye watu karibu milioni 50 eti ni wasukuma tu ndio wanaoonekana, eti majority, kwa sensa ipi?

Na ni lini utaratibu ulibadilika ukawa ni kugawa kazi kwa 'proportionality'? Kwamba kazi watu hawapati kwa sifa tena, bali ni proportionality inayotokana na wingi wa watu kwenye makabila yao? Uongo kabisa huu! Acha ubaguzi!
kwenye hotuba moja ya Julius alisema nchi hii ukizingatia vigezo vya sifa juna hatari nafasi zote za serikali kushikwa na wachaga na wahaya, halafu uone moto wake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na kwa vipi Pasco kijiji kijengewe Airport??
Sio airdrome nasema airport ili zitue ndege gani, kwa bdgt ipi ikaidhinishwa lini na bunge lipi??
Mwl Nyerere hakufanya hivyo, nyumba tuu yakuishi alijengewa na jeshi tena wa lazima!!
That was a true Tanzanian, man of people.
Yako mengi watu wanaogopa watu waiojulikana!!
Mzee wa kiti moto back to your real sence!!
 
Kusema ukweli Mimi ni mkabila 100%,Ni mzalendo 100%.
Kukiwa na nafasi 10 za ndani ya nchi nitaanza na kabila langu,nitafuata wale wa ukanda wangu,ila nitakikisha wote wana sifa.
Kukiwa na nafasi 10 za kimataifa nitaanza na Watanzania Kisha watafuata wa nchi jirani.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niko mkutano wa CCM, nikianzia umati wa watu, ukilinganisha na Chadema, sio siri CCM cha Mtoto!.
Kama watu niliowana mkutano wa Chadema ni wapiga kura kweli, basi kwa mara ya kwanza nakiri kuwa CCM itapigwa chini mjini Busanda. Vijijini, sijajua.

Hakuna Ob yoyote ya TBC, hivyo hakuna live TBC-1 labda TBC-Taifa mlioko huko sikilizeni.

Kampeni za Mwisho za CCM mdororo!.
Tambwe Hiza kachemsha eti Rais Bush kamwalika Jk!.
Waziri Masha kagoma kupanda Jukwwaani.

Mgombea wa CCM Mama Bukwimba hana uwezo wa kujieleza.
Kama wanaBusanda wanachagua mtu na sio chama, basi Mbunge ni Magesa. Lakini kwa vile wanachagua vyama, hata mgombea wa chama awe bomu vipi, chama kitambeba.

Mhe. Magufuli amepanda jukwaani anamwaga kikabila Kisukuma mwanzo mwisho kujibu mapigo ya Shelembi. Magufuli anashangiliwa sana, sasa anamwaga sumu kali dhidi ya Chadema kwa lugha ya Kisukuma.
Anamnadi vizuri mkombea wa CCM.

Leo sijaona wazomeaji.

Kwa vile campain hizi za CCM zinaboa, sitadumu hapa kwa muda mrefu, nitaelekea kampeni za CUF na kumalizia na kampeni za UDP.
Nimesikia mahali Mchungaji Gwajima amehojiwa kwa kuhamasisha ukabila. Sheria yetu ya uchaguzi inakataza kabisa watu kuhutubia kwa kilugha katika mikutano ya kampeni za uchaguzi, hicho nilichoeleza hapo ni kitu ambacho nimekishuhudia kikifanyika, maofisa wa NEC wakiwepo, OCD na polisi wake wakiwepo, and nothing was done about this na kuna watu wanadhani baadhi ya watu kuhutubia kwa lugha za Kisukuma wameanza leo. Hili ni bandiko la mwezi May, 2009, miaka 11 iliyopita!. Sasa leo Gwajima anapoyasisitiza haya kosa lake ni lipi?.

Naendelea kusisitiza Wasukuma sii miongoni mwa makabila yenye ukabila m-baya

P
 
Back
Top Bottom