Tuhuma za Ukabila: Wasukuma si Miongoni mwa Makabila yenye Ukabila, tatizo ndio walio wengi!

Tuhuma za Ukabila: Wasukuma si Miongoni mwa Makabila yenye Ukabila, tatizo ndio walio wengi!

Baada ya hayo yote uliyosema.
Mh. Magufuli hana ukabila.

ISIPOKUWA aliona baada ya hao Wasukuma kudharaulika na kuwekwa pembeni kwa Muda mrefu tangu wakati wa Mwalimui kiwemo systemc strategy ya kuwanyima Elimu wasije wakshika IONGOZI maana alikuwa na HOFU na WASUKUMA.

Magufuli anachofanya sasa Si UKABILA bali ni EQUALIZATION format/ Yaani anabalansi.
Ndo maana nao sasa wanasikika.
.
Kwanini wabaki nyuma kisa tuni WaSUKUMA ?
Jamani tuwe wakweli!
mhn!Makubwa.
 
Nyerere aliwanyimaje wasukuma elimu kama kweli wewe ni mtanzania.
Ulitaka wakijenga shule kisha waje na kuwafunga kamba kwa nguvu.Acheni lawama zisizo na ukweli. Kuna watu toka mikoa mbalimbali walisombwa kwenda shinyanga mwanza na Tabora ili wakajaze nafasi ktk shule ambazo wenyeji waligomea kusoma.

Mlijibagua wenyewe kwa ujinga wenu nadhani hata ibilisi shetani akiambiwa achague kabila ambalo aungane nalo basi angejiita msukuma.
Siandiki kama Msukuma wala Mbena naadika kama Mtanzania niliyo na historia ya hao watu.
Neno "NYIE" halina maana kuwa kila mtu akitoa mchango wake wa kifikira ni
'MSUKUMA".
Hawa jamaa kusema ukweli walionewa sana.

1.Vyama vyao VIKUU vya USHIRIKA vilihakikishwa kuwa vimekufa ili kusiwe na elements ya kuwaunganisha
.
2'MAJARIBIO9 experiments} za UJAMAA zilianzia kwa hawa jamaa maana hawakuwa na la kufanya.

3.MAJARIBIO{ EXPERIMENTS} za UJAMAA hazikufanyika
BUKOBA/KAGERA, Ama Mikoa kama KILIMANJARO.Jiulize ni KWA NINI??????

Ni kweli hawa ni wati wa kuhurumia sana!!
Japokuwa TATIZO lao nao walipenda Ngombe sana.
Na kama nasema uongo unaweza kuni challenge
 
Wanabodi,

Mnyonge Mnyongeni, Haki Yake Mpeni!, Wasukuma sii miongoni mwa makabila yenye ukabila m-baya!, hivyo mtu akiwa ni Msukuma kweli, kamwe hawezi kuwa na ubaguzi wa kikabila, kidini na kikanda, labda jinsia, na hili sio kosa lao, ni mfumo dume wa jamii za kiasili za kiafrika.

Declaration of Interest.
Mimi Paskali Mayalla ni Msukuma, na jina la Mayalla ni jina la ukoo toka kwa mababu na maana yake ni mtu aliyezaliwa wakati wa baa la njaa ( ukame, famine, drought), na sio njaa ya tumbo, au njaa ya shibe kama wengi walivyoaminishwa!, mimi binafsi japo ni Msukuma lakini sio mkabila, na huu ni uthibitisho wa jinsi ninavyopinga ukabila, hata kama ni ukabila wa Wasukuma na 'Wasukuma'.
Wito Kwa Bunge Letu Tukufu: Mkithibisha Hii Nepotism ya Ajabu na ...

Wasukuma Sio Wakabila.
Sisi Wasukuma sio wakabila wa ule ukabila m-baya kwa kufanya ubaguzi wa kikabila au kindugu, yaani undugunaization wa nepotism, Wasukuma ni watu poa sana, ndilo kabila linaloongoza kwa watu wachapa kazi, ndilo kabila linaloongoza kwa upendo, ndilo kabila linaloongoza kwa ukarimu, ndilo kabila linaloongoza kwa unyenyekevu, ndilo kabila linaloongoza kwa viongozi ambao they are "men of the people", yaani watu wa watu na down to earth. Hivyo ninavyoandika hapa simtetei Magufuli kwa vile ni Msukuma, namtetea kwa vile mambo mengine, wanamsingizia bure tuu huyu Msukuma wa watu!.
Rais Magufuli ni Simple, Genuine & Down To Earth-He is Simply A of the People...
Magufuli Kama Nyerere: Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'unyi, Ni ...
Pongezi Rais Wetu Magufuli Kwa Kuwa Mkweli Daima, Tuanzishwa The ...

Jee Magufuli Kweli ni Mkanda, Mdini na Mkabila?.
Hili naomba nilisilijibu ili nisiingilie uhuru wa mahakama, kwa sababu tayari kuna kesi iliyofunguliwa kuhusiana na tuhuma hizi ila nawaomba tuu tusimlaumu Magufuli kutokana na kauli zake.
Kanda ya Ziwa na kuongea kwa ukali: Ukali wa Rais Magufuli ni ...

Conclusion.
Naendelea kusisitiza kwa dhati ya moyo wangu, ukanda, ukabila na udini ni sumu katika taifa letu, katika kupigana na vita hivi, ukweli usemwe, na katika kuusema ukweli huo, haki itendeke, hata kama kuna mnyonge, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni!.

Tanzania ni yetu sote, kila mmoja wetu, ana wajibu wa kuhakisha Tanzania inapa ustawi na maendeleo kwa kujengwa, kulindwa na kustawishwa na sisi Watanzania wenyewe, and it can be done if kila mmoja wetu, will play his part, this is my part
Mungu Ibariki Tanzania.
Asanteni.

Wasalaam.

Paskali
kumbe walewale sa tutegemee nini?? ndomana nyerere nasikia alikataaga makabila yenye watu wengu kushika nchi
 
Mayalla umesahau pia kuwa Wasukuma ndio kabila linloongoza kwa kuharibu manzigira kukata miti ovyo, kuingiza mifugo kwenye hifadhi za taifa na reserve pia hawachimbi vyoo.
Wasukuma ni kweli ni waharibifu wa mazingira aisee. Ila wamasai wanaongiza kwa kuchungia ng'ombe kwenye hifadhi za taifa wala siyo wasukuma. Msukuma hana uwezo wa kupambana na simba ila masai anao. Anachungia Ngorongoro national park na simba akisikia kengele ya ng'ombe anatimua mbio mwenyewe. Jamaa ni noma sana hao.
 
Tusipokuwa makini hii nchi tutakuja kugawana vipande. Maana wasukuma wakishanogewa wanaweza wasiachie madaraka moja kwa moja. Na hivi wako wengi kama kataifa kao wenyewe huko kanda ya ziwa.
 
kumbe walewale sa tutegemee nini?? ndomana nyerere nasikia alikataaga makabila yenye watu wengu kushika nchi
Ni kweli, hata mleta mada kasema "tatizo ni kabila lenye watu wengi", na kweli ni tatizo. Tena endapo watauendeleza ukabila, basi ni wasukuma hadi kiyama. Labda nchi imegeke. Na dalili ziko huko mbeleni kwa utaratibu huu wa "kiwanja cha kimataifa cha ndege chato", na bandari.
 
Siandiki kama Msukuma wala Mbena naadika kama Mtanzania niliyo na historia ya hao watu.
Neno "NYIE" halina maana kuwa kila mtu akitoa mchango wake wa kifikira ni
'MSUKUMA".
Hawa jamaa kusema ukweli walionewa sana.

1.Vyama vyao VIKUU vya USHIRIKA vilihakikishwa kuwa vimekufa ili kusiwe na elements ya kuwaunganisha
.
2'MAJARIBIO9 experiments} za UJAMAA zilianzia kwa hawa jamaa maana hawakuwa na la kufanya.

3.MAJARIBIO{ EXPERIMENTS} za UJAMAA hazikufanyika
BUKOBA/KAGERA, Ama Mikoa kama KILIMANJARO.Jiulize ni KWA NINI??????

Ni kweli hawa ni wati wa kuhurumia sana!!
Japokuwa TATIZO lao nao walipenda Ngombe sana.
Na kama nasema uongo unaweza kuni challenge
Wasukuma halisi ni kabila la watu watii sana na wanyenyekevu, wanaishi communal life mpaka kesho, they are not selfish, they're selfless hadi leo hadi kesho, vijijini wanakula sahani moja. Land ilikuwa ya wote the entire community hivyo it was easy kukubaliana na kila wazo la Mwalimu Nyerere after all, Wasukuma sio very industrious, pamoja na utajiri mkubwa wa n'gombe, hawakujijenga kisasa, vijumba vya hovyo hovyo, na hawana mazao ya kudumu hivyo it was easy ku abandon kila kitu na kuhamia kijiji cha ujamaa, sisi kwetu tuliisha jenga nyumba ya block ya bati, tukagoma kuhama, tukatengwa, babu alipochomoka, Bibi akahamia mjini kwa wanae tukahama bushi jumla.

Wachagga na Wahaya, ni selfish tribes, kila mtu anapakuliwa chakula sahani yake au bakuli lake hivyo no sharing. Kule hakuna communal land, kila ukoo na kihamba chake, na kufuatia zao la kahawa ndio the biggest cash crop, wale ni industrious, hivyo waliendelea wakajenga nyumba za maana, hivyo walikubali kuanzisha vijiji vya ujamaa Kwa lazima lakini walimgomea Mwalimu kuhama, kata kata, na kiukweli enzi za Mwalimu, Wachagga na Wahaya waliisoma sana number.

P
 
Mkuu Karne hiii unakuwa na guts za ku spell Ukabira kwenye mind na kuutafsiri kwenye ink. Good luck japo huwa nasoma posts zako
 
Wasukuma halisi ni kabila la watu watii sana na wanyenyekevu, wanaishi communal life mpaka kesho, they are not selfish, they're selfless hadi leo hadi kesho, vijijini wanakula sahani moja. Land ilikuwa ya wote the entire community hivyo it was easy kukubaliana na kila wazo la Mwalimu Nyerere after all, Wasukuma sio very industrious, pamoja na utajiri mkubwa wa n'gombe, hawakujijenga kisasa, vijumba vya hovyo hovyo, na hawana mazao ya kudumu hivyo it was easy ku abandon kila kitu na kuhamia kijiji cha ujamaa, sisi kwetu tuliisha jenga nyumba ya block ya bati, tukagoma kuhama, tukatengwa, babu alipochomoka, Bibi akahamia mjini na wanae tukahama bushi jumla.

Wachagga na Wahaya, ni selfish tribes, kila mtu anapakuliwa chakula sahani yake au bakuli lake hivyo no sharing. Kule hakuna communal land, kila ukoo na kihamba chake, na kufuatia zao la kahawa ndio the biggest cash crop, wale ni industrious, hivyo waliendelea wakajenga nyumba za maana, hivyo walikubali kuanzisha vijiji vya ujamaa Kwa lazima lakini walimgomea Mwalimu kuhama, kata kata, na kiukweli enzi za Mwalimu, Wachagga na Wahaya waliisoma sana number.

P
Ni kweli mwalimu amesomesha wachagga namba mbaya kabisa! Lakini sikubaliani kusema eti nyie wasukuma mkila chakula wenyewe kwa wenyewe ndiyo siyo ukabila. Huo pengine ni utamaduni tu, hata uchggani upo. Mbona watu wana "ria mbege", chubuku moja inapitishwa kila mtu anakunywa? Mbona hata wakichinja ng'ombe ama mbuzi, nyama zinawekwa kati na ndizi watu wanapiga?

Mkuu hauna taarifa za kutosha, pengine ni kwasababu ya ubinafsi hutaki kufahamu. Ama umekuwa "blindsided due to bias", kwahiyo vya wengine either huvioni, na hata ukiviona, hauoni kwamba ni bora nk.
 
Mkuu Roman, kwanza sorry and don't be offended, kabla ya ujio wa wakoloni, Wachagga pia walikuwa communal, hiyo ya Ku "ria hapo kidogo mbee' ndio kidogo iliyobakia, the spirit ya accumulation of capital is inside Wachagga wengi, na ndio maana wanaijua hela na ndio wanaongoza kwa maendeleo and fixed assets lakini kubali kataa, tribals preferential ipo kwenye ofisi zote top boss ni Mchagga au Muhaya na usitake kupinga tukafumua humu makaburi.
 
Mimi ni msukuma sihitaji kutetea wasukuma hata kidogo natamani watu waseme wale walioenda usukuma nadhani ushuhuda wao utakuwa na nguvu kuliko utetezi wangu. Niliwahi tu kumwambia rafiki yangu kuwa Mungu acha aitwe Mungu maana hili kabila kama lingepewa karma ya ndugunazation wakivyo wengi wangeleta machafuko. Allhamudillah mola akaepusha. Hakuna cha Mwadila ofisin wala ginehe nkoi. Ila kama ipo ni ya mtu mmoja mmoja maana ubaya hauna kwao
 
Mkuu Roman, kwanza sorry and don't be offended, kabla ya ujio wa wakoloni, Wachagga pia walikuwa communal, hiyo ya Ku "ria hapo kidogo mbee' ndio kidogo iliyobakia, the spirit ya accumulation of capital is inside Wachagga wengi, na ndio maana wanaijua hela na ndio wanaongoza kwa maendeleo and fixed assets lakini kubali kataa, tribals preferential ipo kwenye ofisi zote top boss ni Mchagga au Muhaya na usitake kupiga tukafumua humu makaburi.
Ukabila upo kwa makabila mengi tu mkuu. Niwekee hizo links hapa unazodai ni makaburi utafukua, weka hapa.

Shida kubwa ni assimilation! Hata hayo makabila ya wachagga na wahaya, kama waliajiri watu ambao wanasikilizana, kikubwa kinachangiwa na assimilation. Mfano kuna baadhi ya makabila yako hivyo hayawezi ku assimilate ama kujichanganya. Nimeshuhudia sana hili. Bado ile identity ya utaifa inafunikwa na ukabila. Mtu utakuta yuko happy kufanya kazi na mtu wa kabila lake kwasababu wanaelewana zaidi, ama wanakula the same food, wanaogea the same language, na tamaduni zao hawaziachi nk.

Utakuta msukuma ameishi uchaggani akifanya vibarua nk, lakini piga ua, hawezi kula ndizi, atasema siyo chakula, na hiyo ni stereotype. Ndizi ni chakula bora sana. Yeye amekariri ugali nk.

Hayo mambo na hizo tabia, ni visababishi vikubwa vilivyopelekea sisi kutawaliwa na mzungu. Mzungu yeye kwa kujichanganya! Utakuta anaongea hadi kimasai na rubega kapiga!
 
Maandishi yako yanakaukweli, Mimi nina zaidi ya mwaka uhayani lakini sijawahi wala kutamani kuonja senene, naona ni wadudu. Inakuwaje nile wadudu? Ila wengi wanaisifu chakula hiki, sisi kwetu nyama hasa ya ngombe na mbuzi ndiyo kila kitu.
 
Naunga mkono hoja, hata mimi sijaweza kabila kula senene, tatizo ni psychological na connotation kuwa senene ni chakula cha Kihaya, kwa vile mimi sio Mhaya, then siwezi kula senene. Huu pia ni ubaguzi wa kikabila, kwa sababu hao senene sijawahi hata kuwajaribu nikashindwa, ile thinking tuu ni wadudu, siwezi kula, lakini mimi huyo huyo, nimeletewa prone nikajaribu, na ninawala!.
P.
 
Pashal...nimelipenda andiko lako ni zuri..ila sikupendezwa na jambo moja: kutaja taja 'wasukuma'...ushauri wangu ni kuwa jiepushe na hii tabia ya kutaja taja makabila...najua umeandika kwa nia nzuri tu na kwa utani...lakini mambo siku hizi yamebadilika...wako ambao wana elements za ukabila...na wanachukulia kutaja taja makabila kuwa ni agenda yao....watanzania hatuna ukabila na hili tunashukuru kwa jitihada za viongozi wetu waasisi wa taifa hili na hasa Mwalimu Nyerere....lakini watu wengi na hasa vijana wengi hawajui kuwa inawezekaana pengine in Africa ni Tanzania pekee isiyo na ukabila...sasa mitandao au sociaal media ni nzuri lakini zina ubaya wake ..zinaweza kutumika pia kuleta mabaya yakiwemo ya ukabila...tusije taje makabila humu sijui wasukuma, wagogo wachaga na kadhalika....tunadike tu watanzania wanajaza ndege na siyo sijui wasukuma, wachaga na kadhalika...
Hili la ukabila wa Wasukuma, nimelizungumza hapa.
P.
 
paskal ktk awamu ya nne kuna mambo ya kijinga sana yalitokea ikiwemo ubaguzi wabaguzi ndo wanaobaguliwa sasa na kelele ziko nyingi ila kimyakimya next presdent akitoka kwa waliobaguliwa nae ataanza kujenga ngome ya kuwabagua wengine, na hii ita multply forever. Paskali tumia kalamu kuelimisha madhara ya ubaguzi hasa wa kidini na kikabila, utapewa tuzo ya nobel(kama ukipenya salama kwa wasojulikana) na utakumbukwa daima.
Karibu mitaa hii
P
 
Watu kama Pascally Mayalla ni watu wa kupuuzwa,
Hawa ni aina ya watu wanaofikiria kwamba wana akili kuliko watanzania wengine.

Hawa ndio wanaojiita GT wa JF shame.
Pascally mayalla aka njaa wewe nina uhakika unamtetea jiwe sababu ni amekulia usukumani kwenu lkn si mzaliwa wa usukumani,ukabila na ukanda hasa nyinyi watu wa kanda ya ziwa unawala sana,mmeanza kujiona nyinyi ni bora kuliko kanda au kabila zingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
Soma bandiko hili
Sisi sio wakabila bana.
P
 
Mh.Paskali Mayalla umekosea kidogo kuendeleza harakati za ukabila ndani ya CCM kwa Lengo la kushinda uchaguzi tu lakini ni jambo baya sana na kwa kiasi kikubwa limeleta utengano wa wazi sana mpaka sasa. Hilo hata mtoto mdogo anajua limeanza kuota mizizi.
Lilianza kama utani wakati wa Uchaguzi Mwaka 2015.

Ni rahisi sana kuzungumzia Kanda ya Ziwa kwa pamoja kwa ujumla kwa ajili ya kupata kura kutokana na population kubwa ya ukanda huo lakini wakiweza kufanikiwa watagundua kuwa kuna kuna makabila mengine humo ndani wataanza kuwabagua pia mana watagundua hata hao wanaoitwa wasukuma sio wote wasukuma Kuna wengine wamezaliwa tu usukumani au wamejipa tu majina ya kisukuma ili kupata makazi.

Nadhani mbinu hizi za kusifiana kwa sababu ya ukabila zitakwama na zitazidi kuwagawa badala ya kuwaunganisha hata wao wenyewe.

Ukanda huo ni kati ya ukanda uliotumia fedha nyingi sana za umma kwa kuanzia awamu ya kwanza na umetoa Mawaziri na wakubwa wengi sana kwenye serikali zote tangu awamu ya kwanza ya Mkoloni na ya kwanza ya Mkoloni Mweusi lakini hatujasikia wakileta Poroja za kikabila japo mambo mengi sana waliyafanya tofauti na mategemeo ya serikali mana Ni ukanda uliokua na vyama vingi sana vya ushirika lakini wajanja wachache wanaojua kujipendekeza na kusifia watawala walikwapua mapesa za Vyama vya ushirika na kujitajirisha.

Ni ukanda wenye matajiri wengi sana ambao ni wanasiasa waliowahi kushika wizara na mashirika makubwa na nafasi kubwa serikalini . Kwa maana kuwa wengi wametajirika kutokana na ofisi za umma.

Nadhani hata agenda ya kusifiana ni moja tu ya kujipendekeza ile wapate ulaji mana nje ya madaraka ya umma inabidi wakafuge mbuzi na ng"ombe.

Ni vyema sasa kutumia utajiri wao na uchapakazi wao wa asili kujiletea maendeleo bila kutegemea kila kitu toka serikalini. Kila mradi ni Pesa za umma badala ya kuuza ng' ombe na Pamba,Samaki na madini na kujiletea maendeleo kwa kuchanga kama makabila mengine wanaofanya harambee na kujenga mashule na mahospitali na mpaka barabara.

Kuna watu ukanda huo wana miliki mpaka Ng'ombe elfu hamsini lakini wanasubiri kujengewa mpaka kisima cha maji na matundu ya vyoo vya shule.

Uchapa kazi wanao lakini ni wakati sasa wakuwaunganisha kiuchumi sio kuleta siasa za kulaghai watu kwa sifa zisizo kichwa wala miguu.

Watu wanajadili masuala ya nchi yetu ni maskini lakini wengine wanatizama uongozi Kwa jicho la mahaba ya kikabila na kikanda .
Khatari sana!!!

Tusiweke ukabila mbele mana wengine hatuwezi kuvumilia mambo yanayopotosha bila kuyaweka wazi ili kila mtu aone kwa undani zaidi.
Mkuu Digiti Elfu, kwanza samahani kukujibia huku, kwa sababu ni kawaida yangu, nikipandusha baadhi ya mada, huwa sichangii lolote wala kujibu hoja yoyote zaidi ya kutoa likes tuu, lakini objectivity ya mchango wako, umenigusa.

Mimi sio mkabila, na Wasukuma sio wakabila na hawajawahi kuwa wakabila, kwa vile Tanzania tumeisha ongozwa na marais wa makabila matano tofauti, na kila kabila lina strenghs zake na weaknesses zake, kuna ubaya kusifia strenghts za kabila fulani kama uchapakazi bila kuonekana mkabila?.

Tumepata rais chapa ng'ombe anapiga kazi kama maksai, mtu hadi analala na mafaili chumbani, kuna ubaya kumsifia bila kuonekana mkabila?.
P
 
Mimi ni msukuma sihitaji kutetea wasukuma hata kidogo natamani watu waseme wale walioenda usukuma nadhani ushuhuda wao utakuwa na nguvu kuliko utetezi wangu. Niliwahi tu kumwambia rafiki yangu kuwa Mungu acha aitwe Mungu maana hili kabila kama lingepewa karma ya ndugunazation wakivyo wengi wangeleta machafuko. Allhamudillah mola akaepusha. Hakuna cha Mwadila ofisin wala ginehe nkoi. Ila kama ipo ni ya mtu mmoja mmoja maana ubaya hauna kwao

Nakubaliana na wewe kabisa kuwa Wasukuma hawana ubagusi tangu zamani. Nakumbuka enzi zetu za Middle school ile miaka ya sitini(kuwa specific 1963) tulifundishwa darasani kuwa idadi ya Wa Tanganyika(population in Tanganyika) ilikuwa million 9 kati ya hao Wasukuma walikuwa million tatu(three million)(from this figure current Wasukuma lazima wawe at least 20 million) na upande wa nchi ya Zanzibar population ilikuwa laki tatu(three hundred thousand) Wachagga na Wahaya wastani kila moja laki 6!!!! Ila waliosoma kuliko wote ni Wachagga, Wahaya na Wanyakyusa! Sababu - wamissionari waniingia sehemu hizo na kujenga mashule na Mahosipital. Waarabu walisisitiza zaidi ujenzi wa misikiti! Ukweli ndiyo huo! Pili Wachagga/Pare na Wahaya wengi walisoma Uganda na Kenya wakati sekondari zilikuwa chache Tanganyika - Sarafu ilikuwa ni moja Africa Mashariki. Ukiona Wahaya, Wanyakyusa na Wachagga/Pare maofisini siyo kwa upendeleo ila ni shule!!! I stand to be corrected ila kwa sasa sekondari ziko kila kata!
 
Back
Top Bottom