Daimler
JF-Expert Member
- Sep 11, 2018
- 556
- 974
Wewe ndiye mkabila, acha kududanganya.Wakuu asalaam!
Naomba niende kwenye mada moja kwa moja
Huwa najiuliza sana kwa misingi aliyoipigania na kuijennga baba wa taifa Mwl JK Nyerere kama
umoja
Mshikamano
Udugu na zaidi
Kukataa vikali ukabila na udini
Juhudi hizi zinaenziwa kwa vitendo?
Mh rais alipokwenda Kenya na kupewa fursa ya kuongea nakumbuka alisema
"mnaenda vizuri sana tatizo lenu wakenya ni ukabila baasi!"
Nikaona tena alipokwenda kumsalima mjane wa Mwl kwa kinywa chake akisema kuwa yeye ni mfuasi wa Mwl Nyerere.
Kama ndivyo kweli,,,,,
kwanini viongozi wakuu karibu wote 95% wanatoka/teuliwa kutoka kanda ya ziwa
Rais
Jaji mkuu
Mkuu wa majeshi
Mkuu wa polisi
Mwanasheria mkuu
DPP
Mawaziri zaidi ya 60%(kuanzia waziri wa nishati, mifugo na uvuvi, viwanda na biashara, mambo ya ndani, kilimo nk
Na bado kila teuzi mpya inayofanywa ina harufu ya kanda ya ziwa (Ukanda na ukabila)
Hii inamaanisha nini hasa?
Huu ndio tunaita umoja wa kitaifa?
Huku ndiko kumuenzi baba wa taifa?
Tunapata wapi jeuri ya kuwakosoa wakenya?
Ukisema Kanda ya Ziwa unamaanisha nini?
Ungeanza kututajia hiyo Mikoa halafu utuambie wakazi wake kwa kulinganisha na Kanda nyingine ungesaidia sana.
Lakini swali la muhimu sana kwenye uongozi lazima utambue kila mtu anafanya kazi na mtu anayeweza kumsaidia kwenye kazi zake. Hakuna Kiongozi mjinga atafurahia kuteua mtu ili kuwaridhisha watu fulani wakati huyo mteuliwa yupo tu kama pambo. Wakati wa kutafuta kura hawatakusaidia chochote.