Tuhuma za wizi wa Hayati Magufuli haziniumizi, kinachoniumiza kwanini alizaliwa kwenye nchi hii?

Tuhuma za wizi wa Hayati Magufuli haziniumizi, kinachoniumiza kwanini alizaliwa kwenye nchi hii?

Trable

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2023
Posts
1,781
Reaction score
3,288
Ndiyo,

Kinaniuma kwa sababu hasa ya waliostahili kuzaliwa hapa! Waliozaliwa kihalali katika nchi hii ndio hao walionipa kutaka nijue ni kivipi JPM azaliwe katikati yao?

Na iliwezekanaje yeye JPM akubali kuzaliwa katika nchi hii ngumu ukilinganisha na aliyoifanyia hii nchi, badala yake, kwa upekee wake, eti anaogeshwa matusi ya ajabu na wenye nchi yao ngumu!

Ninajaribu kujiuliza na kuhoji uwezo wake mkubwa ambao haujawahi kuoneshwa na kiongozi yeyote hapa!

Alikuwa na uwezo wa kipekee, aliiona Tanzania ikiwa ni nchi wezeshi kwa nchi zingine na nchi yenye uwezo mkubwa kimaendeleo,

Kwa kauli zake hizo, wenyeji ziliwachanganya na wasielewe kwa sababu ndio uwezo wao pekee na huwezi kuwalaumu!

Jambo la kwanza ili kuendana na kauli zake, aliitangaza kuwa, nchi hii ni lazima iwe na viwanda vingi na ili tu wazaliwa wa nchi hii wapate ajira, serikali ikusanye kodi na nchi kuuza bidhaa nyingi nje! Kwa wenyeji, jambo hili kwao ni tusi kwa sababu ndio akili zao zinaishia

Haikutosha, kwa sababu aliiona Tanzania ikiwa ni nchi ya viwanda vingi vikubwa kwa vidogo; akaona mizigo mingi sana ikitoka kila kona ya nchi, akazihurumia barabara na kuona hasara kwa serikali kukaa inakarabati barabara zake zitakazosababishiwa na malori na katika kuhakikisha viwanda vidogovidogo vinafika hadi kijijini, alibuni namna nzuri kuhakikisha umeme umemfikia mwananchi kokote kule kwa bei ya Karibu na bule ya Tsh 27000 tu

Akaamua ajenge Reli mpya ya mizigo SGR ili kukabiliana na jambo hilo, wenyeji wa nchi Hii, jambo hili ni upumbavu!

Akakumbuka tena kwamba, viwanda anavyotamani kuviona katika nchi isiyo yake, shida itakuwa umeme, na ili nchi iwe na ushindani wa kibiashara, lazima kuwepo na umeme wa uhakika na wa bei ndogo, akaona JKNHP ni suluhisho la jambo hilo, angalia vita iliyoibuka juu yake na wenyeji wa nchi Hii ngumu, kila mtu ni shahidi kwa alivyoshambuliwa kila kona! Unajiuliza, ilikuwaje azaliwe kwenye nchi ya watu aina hii tulivyo?

Hakuishia hapo tu, akatazama akaiona Tanzania kuwa ndio kituo kikuu cha biashara ya Madini ndani na nje ya nchi, wageni waje kununua na kuuza dhahabu, serikali ipate kodi na wananchi wafanye biashara, akafungua masoko ya Dhahabu kila kona ya nchi, kwa wenyeji eti hiyo ni kero?

Kwa nini JPM ulikubali uzaliwe katika nchi Hii! Mama mzazi wa JPM utusamehe sana,

Hakuishia hapo, alipoitazama Tanzanite yetu, akagundua kuwa, ni Madini yetu lakini hayatupi faida yoyote zaidi ya mataifa Jirani! Alichokifanya kila raia ni shuhuda, na hii yote ni kwa ajili ya wenyeji wazaliwa! Lakini wapi!

Akaiona Daresalaam kuwa ni jiji linaloshughurika na biashara za kimataifa na kitaifa, akaona kuwa hiyo itakuwa kero kwa viongozi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa kujichanganya katika jiji lenye kuvuta watu wa kila aina, akahamisha makao mkuu kwa kasi na nguvu zote kuupisha mji huo mkubwa nchini ili uwe wa kibiashara tupu, lakini wenyeji mpaka leo hawana uelewa juu ya jambo hilo!

Asante JPM kwa maisha yako katika nchi usiyoistahili uzaliwe! Asante kwa uliyotuachia!

Huko uliko Hayati Magufuli utusamehe sana wenyeji wa nchi hii
 
Joseph Pombe alizaliwa Burundi kwa Baba asiyefahamika. Alivuka mpaka wa Burundi ña mama yake na mama akaja kuolewa na mtu aliyeitwa Magufuli.

Tuwalaumu TISS na CCM ya Kikwette kumpitisha mkimbizi kugombea Urais wa Tanzania na kuwa Rais wetu.

Alichokuwa anafanya Joseph Pombe ni kui vuruga nchi yetu ya amani iwe kama nchi zao za Burundi, Rwanda au Somali.

Wote kwa dakika moja hapo tulipo tuseme ASANTE MUNGU kwa kutuondolea yule Shetani
 
Unajua barabara zilizojengwa na JK??
Nazijua vizuri tu, JK alimwaga pesa zakutosha kwaajili ya njia kuu za kimkakati zilizo unganisha nchi nzima.
Na huyo John Pombe Joseph Magufuli ndio alikuwa site kama waziri wa ujenzi, kusimamia huwo mpango uliofanikiwa vizuri.
 
Back
Top Bottom