imhotep
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 55,997
- 88,219
Niwekee Link Mkuu.Basi,kujifunza hakuishi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Niwekee Link Mkuu.Basi,kujifunza hakuishi.
Una matatizo ya kiakili nenda mirembeNyerere alifanya jambo moja tu zuri ktk taifa hili, nalo ni kuondoa ukabila na ukanda, hivyo kuwafanya watanzania kuwa wamoja. Lakini mengine yote alikosea.
Hivyo kuendelea kumuenzi mwalimu Nyerere ni sawa na kusema tuendelee kuyakumbatia mabaya yake yote. Ambayo ni:-
1. Muungano.
Lengo lilikuwa zuri lakini aina ya muungano ndiyo tatizo. Huu muungano wetu umejaa utata mtupu. Haueleweki, hauelezeki na hautekelezeki lakini tumeukumbatia tu ili kumuenzi mwalimu.
2. Katiba yetu.
Katiba yetu ya Sasa iliundwa enzi za Nyerere 1977. Ktk katiba hii Nyerere alijitwika mamlaka na madaraka yote ya nchi. Kwa katiba hii rais yuko juu ya katiba. Sasa tukiendelea kumuenzi Nyerere maana yake tuendelee na hii katiba. Kwasabb tukiibalisha hata muungano utabadilka.
3. Mwenge.
Hiki kitu hakuna mwenye majibu ya nia, malengo, na umuhimu wake. Lakini kila mwaka mabilioni ya shilingi yanateketezwa ili kuuzungusha nchi nzima. Tunamuenzi Nyerere.
4. Ujamaa.
Wajuvi wanasema watanzania hawajitumi na hawana uthubutu ktk utafutaji kwasabb ya haka kaugonjwa ka ujamaa. Watu wengi wamebweteka kwasabb wanajua watasaidiwa na majirani , ndugu na jamaa. Mifano:-
*Huandai fedha ya harusi/sendoff kwasababu unajua utachangiwa.
*Huandai fedha ya jeneza na mahala pa kuzikiwa kwasbb unajua utachangiwa.
*Watu wengi wamejiunga na vikundi vya kijamii (vikoba, kwaya, jumuiya, soka legends, makanisa, jogging, misikiti, n.k) vinavyowapotezea muda
mwingi ili tu wakipatwa na shida wasaidiwe na vikundi hivyo.
My take: Hii siku ifutwe. Kumbukumbu za Nyerere ziwekwe makumbusho ya taifa huko. Ili tuweze kutekeleza fikra mbadala.
Nchi inaongozwa na waliokuwepo wakati wa uongozi wa Nyerere ama walikuwa sehemu ya uongozi wa Nyerere:- Mwinyi (1925), Mkapa (1938), Kikwete (1950, Magufuli (1959), Samia (1960,). Kwahiyo vichwani mwao kumejaa fikra na mitazamo ya Nyerere tu.Huu ni mtazamo finyu kutoka kwako mtoa mada japo una uhuru wa kutoa maoni.
Sijawahi kumkubali mtu yeyeote anaye link matatizo yetu ya sasa na J K Nyerere. Nyerere hadi 1985 katawala miaka 24.
1985 mpaka leo ni miaka 38, halafu vichwa 5 baada ya Nyerere bado tuendelee kumlaumu yeye ? Not fair at all.
Yaani 60% ya Watanzania wamezaliwa baada ya yeye kuacha madaraka, bado kweli tuendelee kumlaumu?
Na 40% wamezaliwa 2000 kuja huku mbele wamekuta amekufa, nao wanamlaumu Nyerere.
Nyerere aliondoka hajachimba madini instead aliacha ameyahifadhi kwa ajili ya kizazi hiki na cha baadaye. Na utajiri uko kwenye madini, bado TAKATAKA kama Sexless zinamlaumu
Hivi unajua kwamba siasa ni Imani kama ilivyo Imani ya dini? Unadhani ni nini kinazuia katiba kubadilisha?Kuendelea kumlaumu JKN mtu aliyeondoka madarakani zaidi ya miaka 35 iliyopita ni proof watanganyika wanan uwezo finyu wa kufikiri na kutafuta matatizo yao. Mlitaka JKN asolve matatizo yenu ya miaka yote ya mbeleni ili nyie mfanye nini? Waliomfuata walifanya nini? Tuseme alikosea sana hao wengine wameshindwa kurekebisha? This speaks volume about us than him.
Hivi unajua kwamba siasa ni Imani kama ilivyo Imani ya dini? Unadhani ni nini kinazuia katiba kubadilisha?
Hao walioko madarakani wanaona kuibadili katiba ni sawa na kwenda kinyume na Imani zao!
Kisahili kakikuta hata yeye alipoytoka kwao Kiswahili alikuwa anakijuwa, au alikuja Dar Kiswahili hakijuwi?
Hakuna makabila yaliyounganishwa wala kulikuwa hakuna matatizo ya makabila Tanganyika wala Zanzibar.
Tusijitungie vitu ambavyo havikuwepo.
Kuna aliyoyafanya Nyerere lakini hayo mawili hapana. Labda alibadilisha shule zisiwe zinafundisha Kingereza kuanzia shule za msingi, Kingereza kianzia sekondari.
Matokeo, kazalisha taifa la kusomea ujinga.
Kwani wameacha lini?Bibi acha ulimbukeni,wasukuma na wamasai walikua na uadui mkubwa sana wa kuibiana mifugo na kuuana huo ni mfano tu. Huwezi dharau juhudi za JKN kuliunganisha taifa hili. Utakua ni mpumbafu na mwenye chuki binafsi.
Well saidNchi inaongozwa na waliokuwepo wakati wa uongozi wa Nyerere ama walikuwa sehemu ya uongozi wa Nyerere:- Mwinyi (1925), Mkapa (1938), Kikwete (1950, Magufuli (1959), Samia (1960,). Kwahiyo vichwani mwao kumejaa fikra na mitazamo ya Nyerere tu.
Hata baadhi ya wasaidizi wa Nyerere bado wako ofisini hadi leo:- Mkuchika yupo, Wasira amekuwemo mpk awamu ya Kikwete. Unategemea nn?
Hao vijana unaowasema hawana sauti wala maamuzi. Kazi yao ni kuendesha bodaboda na bajaji tu. Hata taarifa za habari hawaangalii kwasabb ya kukosa muda ama kukosa TV.