SoC02 Tuimbe wimbo wa amani na upendo kabla hayajatokea mauaji ya kikatili

SoC02 Tuimbe wimbo wa amani na upendo kabla hayajatokea mauaji ya kikatili

Stories of Change - 2022 Competition

Adili Utotole

Member
Joined
Jul 20, 2022
Posts
14
Reaction score
14
Ukatili ni hali ya kusababisha kwa makusudi mateso na kukosesha raha dhidi ya mtu mwingine,ilihali lipo suluhisho la wazi linaweza kupatikana kwa urahisi

Unaweza kuwa ukatili wa kukatisha uhai wa mtu au mnyama, ukatili wa kingono , ukatili wa kunyima haki mtu ,kundi la watu au taasisi fulani,bila shaka mambo yote haya hufanywa kinyume cha Sheria au utaratibu wa eneo husika.

Kwa miaka ya hivi karibuni vitendo vya ukatili vimekuwa vikiongezeka siku hadi siku, ni wazi kwamba bado hatujapata suluhisho au njia mbadala za kutatua tatizo la ukatili ,ni matendo yanyofanyika na kuicha Jamii katika hali ya mshangao.

Tumeshuhudia wanawake ,wanaume ,watoto wakiuwawa ,kulawitiwa na kusulubishwa katika maeneo mbalimbali. Ni dhahiri kwamba matendo haya yanaendelea na yatazidi kuendelea kujitokeza Kama jamii au serikali haita simama kidete kukemea hali hii.

Bado hatujasahau mauaji ya watu watano wa familia moja yaliyotokea Januari 23 mwaka huu Dodoma. Tunayo kumbukumbu ya jaribio la mauaji kwa mwanasheria na mwanachama wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Tundu Lisu ,jaribio la Septemba Saba 2017.

Hatuwezi kusahau mauaji ya yaliyotokea jijini Mwanza kati ya wanandoa wawili Saidi na Swalha. Pia mauaji yalitotikisa nchi ya Askari watatu wa jeshi la polisi na mlinzi mmoja yaliyotekelezwa na kijana Hamza yaliyopelekea na yeye kuuwawa jijini Dar es Salaam.

Sababu kubwa katika matukio yote haya zimekuwa zikitajwa njama za kulipiza kisasi ama wivu wa mapenzi. Kulipiza kisasi kunatokana na mtu kudhulumiwa haki zake anazoziona kuwa ni za msingi,aidha pesa ,mali au hata kumpoteza mtu wake wa karibu hali kuwa mhusika anamfahamu.

Kwa kesi ya wivu wa mapenzi ,ni kweli kwamba kwa Sasa wapenzi au wanandoa hawaaminiani. Na Imani hutoweka pale ambapo mmoja hupata ushahidi wa kujiridhisha na wakati mwingine Jambo hilo hufanyika kwa makusudi .Kila binadamu kaumbwa na roho tofauti , mwingine huvumilia na kutafuta suluhu lakini mwingine atatafuta namna ya kulipa kisasi kwa muhusika ,na ndio hupelekea mauaji ya kikatili.


inbound6041447202523355050.jpg
Picha juu; Moja ya taarifa ya mauaji ya kikatili, chanzo (Mwananchi digital)

Sasa nini kinaweza kufanyika kupunguza vitendo hivi:

Kwanza ,kabla ya kumlaumu ,kumkamata mtuhumiwa na kumfikisha katika vyombo vya sheria ,ni lazima serikali kupitia jeshi la polisi na Jamii tuambiane na kukumbushana kuwa waaminifu kwa wenza wetu. Tuache kuwa na tamaa za kimwili,Kama huridhishwi na mwenendo wa mwenza wako ,tafuteni maridhiano au kuachana kabisa ,lazivyo matatizo yatatokea.

Pili , tuimbe wimbo wa amani na upendo. Hili ni jukumu la Jamii yote mpaka serikali. Tukumbushane kuwa na upendo. Panapostahili haki ,itolewe haki ya kweli bila upendeleo. Ukiwa mtawala waheshimu na kuwalinda watawaliwa, vivyo hivyo kwa watawaliwa.

Tuepuke tamaa za madaraka ,kwani Jambo hili huleta mtafaruku katika Jamii,watu huchukiana ,nafsi nazo hutibuka ,amani , upendo na umoja hotoweka.

Hata mimi nimewahi kudhulumiwa haki zangu ,tena zenye uwepo wa ushahisdi wa wazi. Lakini vyombo vya Sheria havijawahi kunisaidia hata nilipoahidi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ,niliambiwa upelelezi bado unaendelea mpaka nimekata tamaa ,ni mwaka mmoja Sasa. Hivyo rai yangu, vyombo vya Sheria vifuatilie mambo kwa wakati na haki ipatikane.

Tatu, tukishindwa vyote hivyo kuzuia ukatili na mauaji ,yatolewe hata matamko ya vitisho walau kupunguza hali hii. Endapo mtu atafanya kosa kinyume na Sheria au taratibu ,ataadhibiwa. Katika malezi ya watoto , wazazi hutumia adhabu mbalimbali ili mtoto akue katika maadili mema, tumelelewa hivyo. Wakati mwingine mbinu hizi husaidia.

Nakumbuka kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2015 , aliyekuwa Waziri mkuu wakati huo Mizengo Pinda aliwahi kutoa kauli ya vitisho Bungeni kwa watu waliopanga kufanya maandamano kipindi cha uchaguzi,nanukuu "Ukifanya fujo,umeambiwa usifanye hiki ukaamua wewe kukaidi utapigwa tu, maana hakuna namna nyingine, maana lazima wote tukubaliane kwamba nchi hii tunaendeshwa kwa misingi ya kisheria ,Sasa Kama wewe umekaidi, hutaki, unaona kwamba ni imara zaidi, wewe ni jeuri zaidi watakupiga tu, na Mimi nasema muwapige tu, kwa sababu hakuna namna nyingine,maana tumechoka Sasa" , mwisho wa kunukuu.

Ni kauli aliyoitoa moja ya kiongozi mkubwa wa nchi. Kwa bahati nzuri kila mmoja aliiheshimu kauli yake ,hakuna aliyedhubutu kuingia barabarani na kuleta fujo.Lengo halikuwa kuumiza mtu bali kukemea uovu na fujo.

Sasa kwanini wewe uibe? kwa nini uzini na mke wa mtu? ,kwanini unyime mtu haki ,tunajua nafsi yoyote hupata maumivu. Lakini yote kwa yote tuhimizane amani na upendo kuepuka mauaji ya kikatili, tusiibe ,tusinyimane haki tujenge taifa imara linalozingatia misingi ya kidemokrasia.

Naishukuru Jamii Forums kuanzisha jukwaa hili. Mbali na mshindi kupata zawadi pia ni njia nzuri ya kujifunza mambo mbalimbali,ikiwemo utawala Bora,afya ,siasa ,elimu na kilimo.

Pia unaweza kurejea kusoma makala zangu mbili za Story of change ambazo ni , WILAYA YA KITETO NA FURSA YA MASHAMBA KWA ZAO LA ALIZETI na HUWEZI KUFANIKIWA VIZURI KUJIAJIRI KAMA HUJAWAHI KUAJIRIWA, naomba maoni na ushauri katika maandiko yangu yote matatu.Mawasiliano yangu ni utotolemoja@gmail.com
 
Upvote 1
Back
Top Bottom