Tuishi na wanyama vizuri: paka wangu kaua nyoka jioni ya leo, bila yeye nyoka angekuwa ndani ya nyumba na lolote lingeweza kutokea

Dah! Mtafutie hata supu na yeye ajilambe, jamaa kafanya kazi nzuri.

Paka ni mnyama hatari, sema mwili wake ni mdogo, angekuwa na umbile kubwa kama la mbwa hata mbwa ziwe sita zisingeweza mkabili paka mmoja.
Kwahiyo Simba, chui, duma, mountain lion, jaguar, Black panther, tiger, puma, wote hawa kwako sio paka wakubwa mzee au unadhani paka ni kitu gani?
 
Kwahiyo Simba, chui, duma, mountain lion, jaguar, Black panther, tiger, puma, wote hawa kwako sio paka wakubwa mzee au unadhani paka ni kitu gani?
Ni jamii ya paka ila wana tofauti pia.
Mfano cheetah anakimbia kuliko wote, simba ana nguvu kuliko wengine wote n.k wana sifa tofauti.

Kuwa jamii moja haimaanishi wanafanana kila jambo.

Paka wa nyumbani anayefugwa ni mwepesi sana, yuko makini sana.
 
Paka anaongoza kwa hunting skills kuliko wanyama wote wa jamii ya paka
 
Sababu ya kumkata mkia ilikuwa nini haswa?
Ilikuwa kijijini kipindi cha njaa, mwenyenyumba alienda shamba kurudi akakuta paka amekula mboga alioitegemea na hakukuwa na mboga nyingine.
 
Ilikuwa kijijini kipindi cha njaa, mwenyenyumba alienda shamba kurudi akakuta paka amekula mboga alioitegemea na hakukuwa na mboga nyingine.
Paka mwizi dawa yake ni kumtia kwenye gunia na kwenda kumtupa mbali sana akaishi huko na siyo kumdhuru
 
yani paka ana kasi kubwa mno ya kukwepa kiasi cha kunishangaza.

Sikujua kwamba paka wana uwezo mkubwa kiasi hiki.

Paka ni familia moja na simba, chui, duma, simbamarara n.k, ni jamii ya wanyama wenye uwezo wa kuua viumbe wengine kwa kutumia meno na makucha...
 
Bila picha ya shujaa paka uzi haujatimia


Tunaomba na picha ya shujaa paka tafadhali
 
Paka anaweza kukuua hata wewe mkuu, kama unabisha funga mlango na madirisha yaani kusiwe na mahali pa yeye kutoka halafu mkate mkia.
Ukimkata mkia hana nguvu hata ya kukimbia nanstamina yote inaisha
 
Kala kibano cha maana sana
 
Hata mwa ukimfungia na paka lazima mbwa aumizwe
Humjui mbwa vizuri chief, nilipata tabu sana kufuga mbwa na paka, walikua Kila paka unayemleta wanamuua usiku.... Mpaka ikafika mahali nikiwa nawatrain mchana nakaa nao na paka wakimbwekia tu nawafokea na kuwatishia kuwapiga ndo wakamzoea

Hawa mbwa walishaua paka zaidi ya 6,paka Wana balaa lao lakini kwa mbwa anauliwa chap sana usijidanganye
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…