Faana
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 38,657
- 44,759
Nipo kwenye bus la ABC, kimsingi mabasi ni mazuri, huduma ni nzuri mwendo ni mzuri. Ila changamoto niliyoona ni upande wa choo ambapo bus likifika kwenye matuta mambo yanakuwa siyo shwari ukizingatia matuta nayo hayafanani, usipofanya timing vizuri uka synchronise mwendo wako na mwendo wa dereva basi huduma ya dharura inakuhusu na mbaya zaidi sijaona mahali pa kumfikishia mhudumu taarifa ya dharura.