Nakumbuka pasaka moja enzi hizo, mama kaenda kanisani, kaniachia mboga nipike, akirudi aendelee na mapishi mengine.
Bata mtamu nyie, nikachukua kipande kimoja ili nionje, chumvi ilikuwa imekolea vyema, kawekwa tangawizi, vitunguu swaumu na pilipili manga, viungo vimemkolea.
Nikaongeza kipande cha pili, aisee kikawa kitamu kuliko cha kwanza, ninachokumbuka nilibakiza vipande vitatu tu.
Mama akarudi akiwa ameongozana na Mchungaji, Mwinjilisti na
Mzee wa kanisa.
Uzuri kulikuwa na kuku bandani, akawachinjia fasta. Kichapo nilichopokea aisee, usipime, manundu mWili mzima kama nimepigwa na radi.