Tujadili pamoja: Kuna haja na faida tena ya kuwa na TISS nchini?

Umuhimu wa nchi ndo nini? Au ndo kama mnavyofanya kuharibu miradi kwa rushwa
Mradi gani umeharibiwa kwa rushwa?una ushahidi?
, kufanya nchi isiwe na mifumo imara ya utawala
Uliza waliofanya vurugu 29/10 kama hakuna mifumo imara ya utawala
huku wananchi wakizidi kuwa masikini?
1990s barabarani(za vumbi) vyombo vya moto vilikua vya waasia, serikali,mashirika leo barabarani(lami) kuna vyombo vya watanzania na kila nyumba tano tatu Zina vyombo vya moto,nyumba za nyasi zimeisha,shule binafsi tele na ada juu lakini watz wanalipa,hakuna njaa
 
Teeth ni UHASAMA wa TAIFA na USALAMA WA WANASIASA.

UHASAMA WA TAIFA kwa kuteka na kuua wazalendo ,mafisadi yanaiba mali wao wapo tu wanakenua MENO.

USALAMA WA WANASIASA kwasababu wanalinda maslahi yao na ndiyo maana abdul anatoa order tu.
Taasisi inaingiza hadi Mercenaries kutoka Zanzibar, Msumbiji, Uganda na Burundi kuuwa Watanganyika?

Hapa hatuna Taasisi kwa kweli bali kikundi cha wahuni na wapumbavu wa ccm wanaotumika na ccm kuwatawala watanzania kwa nguvu huku kuwaharibia maisha yao kwa faida ya wachache.
 
Nchi inapaswa kuwa salama kwenye maeneo 3;
1. Kiuchumi
2. Kijamii
3. Kisiasa

Kisiasa Katiba ya Nchi yetu inatambua nchi yetu kuwa ya Kidemokrasia. Hii maana yake ni kwamba ili nchi iwe salama ni lazima mifumo ihakikishe siasa za nchi hii ni za kidemokrasia kweli. Vyama vya kisiasa vinashindana kwa usawa na vinakuwa na nafasi sawa ya kuunda serikali kwa kipindi fulani kwa mujibu wa Katiba. Vinakuwa na usawa kwenye kushindana kwenye uchaguzi na kupata nafasi ya kutangazwa kuwa washindi ili waunde Serikali.

Kinyume chake TISS imenajisi mfumo wa kisiasa kwa kukipendelea chama kimoja cha siasa ambacho ni CCM na kuruhusu Katiba kusiginwa na matakwa ya Wananchi kudhulumiwa. Hii ni hatari kwa usalama wa Taifa na Wananchi kwa sababu inaleta kinyongo na wananchi kuwaza njia mbadala za kutafuta demokrasia. Njia hizi zimeanza kuleta mauaji ya raia, kutekwa na kupotezwa kwa raia. Kiwango kikubwa cha utekaji na mauaji ya Wananchi kilichofanywa kuanzia mwaka 2017 hadi sasa ikiwemo kwenye uchaguzi mkuu wa 2025 inaonesha kabisa kuwa nchi yetu haipo salama kisiasa.

Kwa upande wa kiuchumi ili nchi iwe salama inapaswa kuwa na mifumo imara ya kifedha, uchumi imara usiotetereka, usioharibiwa na rushwa na ufisadi pamoja na maendeleo ya kweli kwa Wananchi.

Hapa Tanzania nchi yetu ina kila kitu cha kuifanya kuwa Taifa tajiri zaidi na lenye maendeleo zaidi Afrika. Hii ni kutokana na uwepo wake kijiographia na uwepo na mito, bahari na rasilimali nyingi zingiwemo gesi, dhahabu na madini mbalimbali.

Ila kinyume chake nchi yetu ni masikini sana. Kutokana na rushwa inayofanywa kwenye miradi mikubwa ya kulifanya Taifa liwe na uchumi imara, miradi mingi imekuwa ikitekelezwa kwa hasara kiasi cha kufanya Taifa liwe kwenye hatari ya kiusalama kiuchumi. Miradi ya barabara, ujenzi wa majengo, maji, reli na kila sehemu imekuwa ikitekelezwa chini ya kiwango huku ikitumia fedha nyingi za walipakodi ambazo mwisho zimefanya miradi husika kuwa ya hasara kwa Taifa.

Sio hivyo tu kipaumbele kwenye miradi na usimamizi wake unaonesha kuwa Taifa linaendeshwa na watu wasio na akili. Miradi ya mwendokasi, vivuko, ndege, masoko na sasa SGR inaonesha kabisa kuwa nchi hii imeshajifia kutokana na kukosa ubora wa muda mrefu. Kwa kifupi hii nchi sio salama kabisa kiuchumi maana iko kwenye blink of collapse.

Kijamii ili jamii iwe salama kunapaswa kuwa na kuelewana baina ya wananchi wa dini mbalimbali na makabila mbalimbali. Dini zinapaswa kuachwa kukemea dhambi na dhuluma. Walimu wa mashuleni na vyuoni wanapaswa kuachwa huru kufanya tafiti halisi za matatizo ya wananchi na kupendekeza kwa uhuru suluhisho la matatizo hayo. Walimu pia wanapaswa kuachwa kuwafundisha Wanafunzi ukweli katika masomo yao huku wakitoa mifano hai na ya ukweli. Wananchi pia wanapaswa kuachwa kuwa huru kutoa mawazo yao bila hofu ya kulawitiwa, kutekwa, kuuwawa au kufunguliwa kesi za uongo.

Kinyume chake hapa nchini sasa TISS kwa kushirikiana na CCM wanazuia wananchi kuwa huru kutoa mawazo yao kwa uhuru. Wanawatisha na hata kuwakamata na kuwapoteza.

Kwa sasa nchini, TISS na ccm wanaendesha propaganda za hatari za kufarakanisha dini na Viongozi wa dini ili tu kulinda maslahi ya wanasiasa kisiasa. Kwa sasa wanawapangia hadi wachungaji, masheikh na mapadre wahubiri nini na wakemee dhambi gani. Hii ni hatari kwa usalama wa Taifa.k

Walimu mashuleni sasa wanapangiwa wafundishe nini wanafunzi wao na wawape mifano gani jambo ambalo linaenda kuua free thinking na kusababisha jamii iangamie maana bila fikra huru hapawezi kuwa na jamii imara. Historia ya dunia inaonesha matatizo ya wananchi duniani yalipatiwa ufumbuzi wa kudumu kupitia fikra huru.

Swali langu kwenu wanabodi Je kuna haja na faida tena ya kuendelea kuwepo kwa hiki chombo TISS nchini?
Kwakuwa chinjachinja iliaminiwa zaidi,hiyo ifutwe wachukue majukumu yao.
 
Mradi gani umeharibiwa kwa rushwa?una ushahidi?

Uliza waliofanya vurugu 29/10 kama hakuna mifumo imara ya utawala

1990s barabarani(za vumbi) vyombo vya moto vilikua vya waasia, serikali,mashirika leo barabarani(lami) kuna vyombo vya watanzania na kila nyumba tano tatu Zina vyombo vya moto,nyumba za nyasi zimeisha,shule binafsi tele na ada juu lakini watz wanalipa,hakuna njaa
Miradi yote

Huoni mwendokasi? Nani alisema ijengwe vile? Nani alisema ijengwe yard Jangwani?

Huoni SGR? Huoni mvua kidogo tu imesitisha safari kwa madaraja kuathiriwa na mvua?

Huoni vivuko vinavyojengwa kwa bei mbaya vinavyoharibika na kuendeshwa hovyo?

Huoni Bandari? Huoni barabara zinavyojengqa chini ya kiwango? Umepita barabara ya Dar- Dodoma - Mwanza? Dar- Lindi - Mtwara?

Umepita barabara ya Dodoma- Iringa? Umeona barabara za mitaani zilivyo chini ya kiwango?
 
Hizo shule unazosema ulishawahi kumuona mtoto wa afisa elimu,mkuu wilaya,waziri anasoma?Hizo shule ni Kwa ajili ya TABAKA la kutumiwa na watawala kama dekio ili wao waendelee kuneemeka na wewe kubaki mpiga mdomo tu wa mapambio
 
Hana akili huyu. Achana nae.
 
Nchi inapaswa kuwa salama kwenye maeneo 3;
1. Kiuchumi
2. Kijamii
3. Kisiasa

Kisiasa Katiba ya Nchi yetu inatambua nchi yetu kuwa ya Kidemokrasia. Hii maana yake ni kwamba ili nchi iwe salama ni lazima mifumo ihakikishe siasa za nchi hii ni za kidemokrasia kweli. Vyama vya kisiasa vinashindana kwa usawa na vinakuwa na nafasi sawa ya kuunda serikali kwa kipindi fulani kwa mujibu wa Katiba. Vinakuwa na usawa kwenye kushindana kwenye uchaguzi na kupata nafasi ya kutangazwa kuwa washindi ili waunde Serikali.

Kinyume chake TISS imenajisi mfumo wa kisiasa kwa kukipendelea chama kimoja cha siasa ambacho ni CCM na kuruhusu Katiba kusiginwa na matakwa ya Wananchi kudhulumiwa. Hii ni hatari kwa usalama wa Taifa na Wananchi kwa sababu inaleta kinyongo na wananchi kuwaza njia mbadala za kutafuta demokrasia. Njia hizi zimeanza kuleta mauaji ya raia, kutekwa na kupotezwa kwa raia. Kiwango kikubwa cha utekaji na mauaji ya Wananchi kilichofanywa kuanzia mwaka 2017 hadi sasa ikiwemo kwenye uchaguzi mkuu wa 2025 inaonesha kabisa kuwa nchi yetu haipo salama kisiasa.

Kwa upande wa kiuchumi ili nchi iwe salama inapaswa kuwa na mifumo imara ya kifedha, uchumi imara usiotetereka, usioharibiwa na rushwa na ufisadi pamoja na maendeleo ya kweli kwa Wananchi.

Hapa Tanzania nchi yetu ina kila kitu cha kuifanya kuwa Taifa tajiri zaidi na lenye maendeleo zaidi Afrika. Hii ni kutokana na uwepo wake kijiographia na uwepo na mito, bahari na rasilimali nyingi zingiwemo gesi, dhahabu na madini mbalimbali.

Ila kinyume chake nchi yetu ni masikini sana. Kutokana na rushwa inayofanywa kwenye miradi mikubwa ya kulifanya Taifa liwe na uchumi imara, miradi mingi imekuwa ikitekelezwa kwa hasara kiasi cha kufanya Taifa liwe kwenye hatari ya kiusalama kiuchumi. Miradi ya barabara, ujenzi wa majengo, maji, reli na kila sehemu imekuwa ikitekelezwa chini ya kiwango huku ikitumia fedha nyingi za walipakodi ambazo mwisho zimefanya miradi husika kuwa ya hasara kwa Taifa.

Sio hivyo tu kipaumbele kwenye miradi na usimamizi wake unaonesha kuwa Taifa linaendeshwa na watu wasio na akili. Miradi ya mwendokasi, vivuko, ndege, masoko na sasa SGR inaonesha kabisa kuwa nchi hii imeshajifia kutokana na kukosa ubora wa muda mrefu. Kwa kifupi hii nchi sio salama kabisa kiuchumi maana iko kwenye blink of collapse.

Kijamii ili jamii iwe salama kunapaswa kuwa na kuelewana baina ya wananchi wa dini mbalimbali na makabila mbalimbali. Dini zinapaswa kuachwa kukemea dhambi na dhuluma. Walimu wa mashuleni na vyuoni wanapaswa kuachwa huru kufanya tafiti halisi za matatizo ya wananchi na kupendekeza kwa uhuru suluhisho la matatizo hayo. Walimu pia wanapaswa kuachwa kuwafundisha Wanafunzi ukweli katika masomo yao huku wakitoa mifano hai na ya ukweli. Wananchi pia wanapaswa kuachwa kuwa huru kutoa mawazo yao bila hofu ya kulawitiwa, kutekwa, kuuwawa au kufunguliwa kesi za uongo.

Kinyume chake hapa nchini sasa TISS kwa kushirikiana na CCM wanazuia wananchi kuwa huru kutoa mawazo yao kwa uhuru. Wanawatisha na hata kuwakamata na kuwapoteza.

Kwa sasa nchini, TISS na ccm wanaendesha propaganda za hatari za kufarakanisha dini na Viongozi wa dini ili tu kulinda maslahi ya wanasiasa kisiasa. Kwa sasa wanawapangia hadi wachungaji, masheikh na mapadre wahubiri nini na wakemee dhambi gani. Hii ni hatari kwa usalama wa Taifa.

Walimu mashuleni sasa wanapangiwa wafundishe nini wanafunzi wao na wawape mifano gani jambo ambalo linaenda kuua free thinking na kusababisha jamii iangamie maana bila fikra huru hapawezi kuwa na jamii imara. Historia ya dunia inaonesha matatizo ya wananchi duniani yalipatiwa ufumbuzi wa kudumu kupitia fikra huru.

Swali langu kwenu wanabodi Je kuna haja na faida tena ya kuendelea kuwepo kwa hiki chombo TISS nchini?
Mkuu vipi tena? Si uliomba Jeshi la Marekani lije likusaidie kupindua serikali? Vipi wamekataa?

Chadema ni chama kinachoongozwa kutoka Uberligiji hivyo kisahau kuongoza nchi ya TZ fullstop!!
 
Hatutaacha kuomba msaada marekani. Uzuri safari hii tumewaomba msaada na wametusikiliza kweli. Tulia muone kibano.
 
Miradi yote

Huoni mwendokasi? Nani alisema ijengwe vile? Nani alisema ijengwe yard Jangwani?

Huoni SGR? Huoni mvua kidogo tu imesitisha safari kwa madaraja kuathiriwa na mvua?

Huoni vivuko vinavyojengwa kwa bei mbaya vinavyoharibika na kuendeshwa hovyo?

Huoni Bandari? Huoni barabara zinavyojengqa chini ya kiwango? Umepita barabara ya Dar- Dodoma - Mwanza? Dar- Lindi - Mtwara?

Umepita barabara ya Dodoma- Iringa? Umeona barabara za mitaani zilivyo chini ya kiwango?
Ukiona hivyo mnufaika ama nyumbani ni pale Kazurambimba,chekechea hadi darasa la saba na baada ya hapo hajatoka nje ya hapo.
 
Kabla hujawajadili kwa ujumla ....jadili kwanza sheria iliyowapeleka ikulu na kuwa chini ya rais
 
Hatutaacha kuomba msaada marekani. Uzuri safari hii tumewaomba msaada na wametusikiliza kweli. Tulia muone kibano.
Mmefeli pakubwa sana safari hii na vurugu zenu za kupindua Serikali. Vipi bado Maria anakulipa perdiem hapo Nairobi au ndio imekwisha hiyo!!?
 
Nani anataka kupindua Serikali. Nani yupo Nairobi? We endeleza tu upunguani wako tu. Akili yako haina akili ndo mana unawaza ujinga na upumbavu muda wote.
 
Hii serikali inatakiwa itoke yoote
kila kitu kianze upya
REFORMS.

KISS imejaza mapimbi ya uvccm ni taasisi imejaa machawa wa mbogomboga
wapo pale kulinda chama cha magaidi!
 
Mpumbavu ni wewe uliyekuwa unahamasisha watz kuchoma moto mali za umma na binafsi vyombo vya ulinzi na usalama lazima wakushughulikie ukirudi tu TZ. Umesababisha mali za umma na binafsi kuchomwa moto na wahuni wenzako hatutaacha kukusema mhuni wewe.
 
Hii serikali inatakiwa itoke yoote
kila kitu kianze upya
REFORMS.

KISS imejaza mapimbi ya uvccm ni taasisi imejaa machawa wa mbogomboga
wapo pale kulinda chama cha magaidi!
Ni kikundi cha wahuni, vilaza, wapumbavu na wasio na akili.
 
Halafu wewe ndio unafaa unayetaka wazungu waje kuongoza nchi hii!!? Slavery mentality inakusumbua sisi tunaojitambua hatutakubali kama ambavyo tumekataa uhuni wenu wa kutaka kupingua Serikali tarehe 29 October 2025
 
Sijasoma mada ila mimi ni mtu namba moja nae pinga uwepo wa tiss kwenye hii nchi hawa jamaa amn kitu wanafanya toka wachague chama badala ya Taifa bora ifutwee tu wanakula kodi zetu bureee takataka hawa, sasa ngoja nisome mada
 
Wewe utakuwa zaidi ya takataka!😀
 
Back
Top Bottom