Dunia hii unaweza kusema una kila kitu na una kila aina ya uwezo.Anajisemeaga mkuu Mpwimbe hii idara imejaa vilaza hakuna mfano
Ila matokeo ya uwezo wako, huwa siyo SIRI.
Kila mtu timamu anaona ni ZERO kabisa.
Dunia hii unaweza kusema una kila kitu na una kila aina ya uwezo.Anajisemeaga mkuu Mpwimbe hii idara imejaa vilaza hakuna mfano
Ahahahah wewe siku wakija kukukamata wananchi wenye hasira kali tutakunyoosha mbona😂😂😂 sasa hivi nafanya kazi kwa mkataba, ni jasusi wa kujitegemea.
Sifungamani na tiss yenu hiyo.
Yaaani wana kazi hadi za kuiba chaguzi za Serikali za Mitaa ili CCM ishinde. Hii ndo idara ya Ujasusi eti. kudadekiDunia hii unaweza kusema una kila kitu na una kila aina ya uwezo.
Ila matokeo ya uwezo wako, huwa siyo SIRI.
Kila mtu timamu anaona ni ZERO kabisa.
Yaaani wanaitumikia ccm na wako royal kwa ccm kuliko kwa Taifa na wananchi. Pathetic kabisaKwa sasa hakuna. Iundwe upyq, sheria zibadilishwe isiwe puppet wa ccm. Tiss iko chini ya rais ambaye ni mwenyekiti wa ccm unategemea nn
Kuiba kwenyewe hawajui.Yaaani wana kazi hadi za kuiba chaguzi za Serikali za Mitaa ili CCM ishinde. Hii ndo idara ya Ujasusi eti. kudadeki
Ukiwaona Mwambegele na Kailima walivyo alafu unaambiwa wale ndo senior officers wa TISS unajisemea tu kama nchi imefikia kuwa na watu kama wale ndo TISS na wanayofanya ndo yale kweli sie tumeshajifia kilichobaki ni kuzikwa tu.Kuiba kwenyewe hawajui.
Wamempa Samia kura milioninm 31.
Mpaka zuzu anawaona mazuzu.
Napiga watu 300 kwa pamoja bila kuchoka.Ahahahah wewe siku wakija kukukamata wananchi wenye hasira kali tutakunyoosha mbona
Kwa maslahi tu ya CCM yangu sawa, iwepoNchi inapaswa kuwa salama kwenye maeneo 3;
1. Kiuchumi
2. Kijamii
3. Kisiasa
Kisiasa Katiba ya Nchi yetu inatambua nchi yetu kuwa ya Kidemokrasia. Hii maana yake ni kwamba ili nchi iwe salama ni lazima mifumo ihakikishe siasa za nchi hii ni za kidemokrasia kweli. Vyama vya kisiasa vinashindana kwa usawa na vinakuwa na nafasi sawa ya kuunda serikali kwa kipindi fulani kwa mujibu wa Katiba. Vinakuwa na usawa kwenye kushindana kwenye uchaguzi na kupata nafasi ya kutangazwa kuwa washindi ili waunde Serikali.
Kinyume chake TISS imenajisi mfumo wa kisiasa kwa kukipendelea chama kimoja cha siasa ambacho ni CCM na kuruhusu Katiba kusiginwa na matakwa ya Wananchi kudhulumiwa. Hii ni hatari kwa usalama wa Taifa na Wananchi kwa sababu inaleta kinyongo na wananchi kuwaza njia mbadala za kutafuta demokrasia. Njia hizi zimeanza kuleta mauaji ya raia, kutekwa na kupotezwa kwa raia. Kiwango kikubwa cha utekaji na mauaji ya Wananchi kilichofanywa kuanzia mwaka 2017 hadi sasa ikiwemo kwenye uchaguzi mkuu wa 2025 inaonesha kabisa kuwa nchi yetu haipo salama kisiasa.
Kwa upande wa kiuchumi ili nchi iwe salama inapaswa kuwa na mifumo imara ya kifedha, uchumi imara usiotetereka, usioharibiwa na rushwa na ufisadi pamoja na maendeleo ya kweli kwa Wananchi.
Hapa Tanzania nchi yetu ina kila kitu cha kuifanya kuwa Taifa tajiri zaidi na lenye maendeleo zaidi Afrika. Hii ni kutokana na uwepo wake kijiographia na uwepo na mito, bahari na rasilimali nyingi zingiwemo gesi, dhahabu na madini mbalimbali.
Ila kinyume chake nchi yetu ni masikini sana. Kutokana na rushwa inayofanywa kwenye miradi mikubwa ya kulifanya Taifa liwe na uchumi imara, miradi mingi imekuwa ikitekelezwa kwa hasara kiasi cha kufanya Taifa liwe kwenye hatari ya kiusalama kiuchumi. Miradi ya barabara, ujenzi wa majengo, maji, reli na kila sehemu imekuwa ikitekelezwa chini ya kiwango huku ikitumia fedha nyingi za walipakodi ambazo mwisho zimefanya miradi husika kuwa ya hasara kwa Taifa.
Sio hivyo tu kipaumbele kwenye miradi na usimamizi wake unaonesha kuwa Taifa linaendeshwa na watu wasio na akili. Miradi ya mwendokasi, vivuko, ndege, masoko na sasa SGR inaonesha kabisa kuwa nchi hii imeshajifia kutokana na kukosa ubora wa muda mrefu. Kwa kifupi hii nchi sio salama kabisa kiuchumi maana iko kwenye blink of collapse.
Kijamii ili jamii iwe salama kunapaswa kuwa na kuelewana baina ya wananchi wa dini mbalimbali na makabila mbalimbali. Dini zinapaswa kuachwa kukemea dhambi na dhuluma. Walimu wa mashuleni na vyuoni wanapaswa kuachwa huru kufanya tafiti halisi za matatizo ya wananchi na kupendekeza kwa uhuru suluhisho la matatizo hayo. Walimu pia wanapaswa kuachwa kuwafundisha Wanafunzi ukweli katika masomo yao huku wakitoa mifano hai na ya ukweli. Wananchi pia wanapaswa kuachwa kuwa huru kutoa mawazo yao bila hofu ya kulawitiwa, kutekwa, kuuwawa au kufunguliwa kesi za uongo.
Kinyume chake hapa nchini sasa TISS kwa kushirikiana na CCM wanazuia wananchi kuwa huru kutoa mawazo yao kwa uhuru. Wanawatisha na hata kuwakamata na kuwapoteza.
Kwa sasa nchini, TISS na ccm wanaendesha propaganda za hatari za kufarakanisha dini na Viongozi wa dini ili tu kulinda maslahi ya wanasiasa kisiasa. Kwa sasa wanawapangia hadi wachungaji, masheikh na mapadre wahubiri nini na wakemee dhambi gani. Hii ni hatari kwa usalama wa Taifa.
Walimu mashuleni sasa wanapangiwa wafundishe nini wanafunzi wao na wawape mifano gani jambo ambalo linaenda kuua free thinking na kusababisha jamii iangamie maana bila fikra huru hapawezi kuwa na jamii imara. Historia ya dunia inaonesha matatizo ya wananchi duniani yalipatiwa ufumbuzi wa kudumu kupitia fikra huru.
Swali langu kwenu wanabodi Je kuna haja na faida tena ya kuendelea kuwepo kwa hiki chombo TISS nchini?
Kwa maslahi tu ya chama changu CCM sawa.Hii Tiss tuliyonayo imepigwa copy na mafisadi kwa maana ya kwamba ni kweli jina ni Usalama wa Taifa ila kiutendaji hawako kitaifa ni usalama wa viongozi walafi wa mali za taifa. Ni chombo ambacho hakiko kwa ajili ya maslahi ya taifa bali yapo kwa ajili ya kuhakikisha genge la wezi wa mali za umma haliguswi na ninaamini hata anapotokea mwanakitengo kusimamia ukweli na kutaka mambo yaende inavyopaswa anapotezwa haraka sana.
Kwahiyo mpaka aparikane mzalendo wa kweli ili afumue mifumo yote ya kiulinzi ikae kitaifa zaidi. Kamq mpaka kina mzee Warioba leo hii serikali iliyopo madarakani haiwaoni kama ni wazalendo tunatakiwa kujua definition ya uzalendo imebadilika sana uzalendo kwasasa unapimwa na wanachokitaka kina Mafwele kwa maslahi yao.
Hakuna kitu jeshi la wananchi lililikosea taifa kama ile tarehe 29th October hapo ndo mambo yote yaliharibika na sijui nani ataliokoa tena hili taifa maana limetekwa na manyang'au na yana nguvu ya kipesa na ulinzi hakuna mfano.