Tujadili uwepo wa idadi kubwa ya wenye nyumba ambao ni maskini hapa Tanzania hasa jijini Dar

Kama nchi bado tuna safari ndefu sana ya kufikia maendeleo ya kweli kwasababu bado watu wana mawazo kama yako. Kuna kazi kubwa ya kufanya. Wengi tunaweka akili kwenye matatizo tu... yaani kama vile shida ni jambo la kufurahia. Kwani huwezi kuwa na nyumba ikaungua? Tuuchukie umaskini. Haina maana unaishi kwenye nyumba nzuri ila ukiumwa tu unachangisha mchango wa matibabu au wengine hata kulipa tu ada za watoto ni shida
 
Ninasoma comments za watu hapa na kujikuta ninazidi kusikitika kuona wabongo wengi wanang'ang'ania umaskini utadhani ni sifa. Unapata faida gani kuwekeza kwenye nyumba kali huku ukiwa huna hata bima ya afya? Unaishi kwako ila hata ada za watoto ni mawazi kuzipata? Yaani watu hapa wanawaza kufukuzwa kazi, kufeli kwenye biashara, na matatizo mengine. Kama akili zetu tutakuwa tunazibebesha fikra hasi za kwamba ipo siku tutafukuzwa kazi au biashara itabuma basi kama nchi tuna safari ndefu mno kupata ukombozi wa kiuchumi. Ninawasihi vijana wekezeni kwenye vyanzo vya mapato. Kwa mfano kama wewe ni mwanariadha basi pesa zako za mwanzoni wekeza hata kwa kulipia training huko Kenya...
 
Umeshauri vizuri lkn itawawia wachache kutoa code. Code iloyopo kwenye ushauri wako ni kwamba watu wakipata mitaji yao ya kwanza wawekeze kwenye vitu vya kuzunguka haraka. Let us take risk. Nyumba kwa sababu ni less risk kama ilivyo kuweka pesa UTT Amis, basi haiwezi kukuletea mzunguko wa pesa unaoeleweka. Nyumba ziwe secondary investments. Nyumba hazina sifa ya kuwa primary investment. Unaweza ukajenga nyumba kwa milioni 50 halafu ukapangisha kwa milioni 2 kwa mwaka. Kuna taxes na operation costs.
 
Nashukuru. Wewe umeongea kitaalamu zaidi.
 
Binafsi ninakerwa mno nikiona baba au mama mwenye nyumba maskini kuliko mpangaji. Tubadilishe fikra zetu.


Umenikumbusha mama mwenye nyumba wangu.....una hoja usikilizwe
 
Ahsante kwa taarifa, tutaifanyia kazi.
 
Yani kupanga ni ujanja!! Kufilisika kwa mtu hakuji kwa kujenga nyumba, kuna wapangaji nao hufilisika na kurudi kijijini na kumuacha mwenye nyumba masikini mjini akitamba kwa kupokea kodi na kufurahia maisha mjini.
 
Wote mnaolazimisha Wenzenu wajenge Kuna mawili ama waoga wa maisha au hamujuimaisha ni nn Kuna angle watanzania hawajipata na ndo maana Kila mtu akipata Hela anaenda kuifungia kwenye Nyumba haizalishi na Ile Hela haitarudi tena.
 
Sijasoma matapishi yako yote hila ebu nikupe maarifa! Mwenyenyumba ataendelea kuwa juu sana kuliko mpangaji hata kama unamzidi kipato!
Ndugu Mtapishi kama uko Dar Njoo upande wa mbweni uone magofu ambayo hayajakamilika uone yamefungia Hela kiasi gani. Imagine watu wanachukua mikopo ya Nyumba 200 to500m unajenga Nyumba then maisha yako yote unalipia loan huna biashara. Mwajiriwa ukistaafi wanakuja Hadi Pension
 
Uko sahihi wamezika mitaji ya hela ndefu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…