Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 7,899
- 10,415
Ni kweli kumekua na tatizo la upungufu wa maji uliosababishwa na ukame.
Swala hilo linapelekea maji ya kwenye mabwawa yanayotumika kufua umeme kupungua.
Lakini pamoja na hayo yote tunaweza kuongeza ufuaji wa umeme wa kutumia gesi.
Tunajua asilimia 62 ya umeme tunaotumia Tanzania ni wa gesi. Asilimia 38 inayobakia unatokana na vyanzo vingine kama maji n.k.
Katika swala la ukame hatuwezi kusubiri mabwawa yajae baada ya mvua kunyesha ndio uzalishaji wa umeme uongezeke hapo tutakua tunachelewa.
Hapo solution ni kuongeza uzalishaji wa umeme unaotokana na gesi.
Tuongeze uzalishaji wa gesi na pia tuongeze turbine zingine kwaajili ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi.