SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Kuna haka kautamaduni tunako waswahili ka kuwachukulia poa sana wachezaji wazawa. Inafikia wakati wanalipwa mishahara duni, wakitaka kuuzwa wanauzwa kwa pesa ndogo sana kiasi kwamba hata haitajwi kwa aibu. Nadhani wakati umefika tujenge utamaduni mpya. Embu nisome kidogo...
Huko Uingereza wana utamaduni wa kuwathaminisha wachezaji wao. Wengi wa hawa wachezaji wazawa ndani ya EPL mnaowasifia na kuwaimba ni wachezaji wa kawaida katika level za Ulaya na duniani ila wana thamani kubwa katika soko na wanalipwa mishahara ambayo si haba. Ni utamaduni walioujenga ili isiwepo taswira kuwa wageni tu ndiyo wana thamani.
Ningependa kuona wachezaji wetu wazawa hasa ambao wameonyesha viwango vikubwa vyenye muendelezo aina ya kina Feisal, Bacca, Dickson, Awesu nk. wakithaminishwa. Hili litawaongezea sana soko hata huko nje. Wengine utetezi wetu kwa Feisal ulijikita kwenye hoja hii na si kwa ajili ya kuikomoa Yanga.
Hali ilivyo sasa timu za nje zinamuona mchezaji wetu, wakiangalia rekodi ya mchezaji wanaona kila siku anauzwa na kununuliwa kwa shilingi milioni 15 ikizidi sana 25 na mshahara wa milioni 4 wanamuweka pembeni kumbe anaubonda vizuri tu. Tubadilike. Thaminisha kitu chako ili wengine pia wakithamini.
Simba toeni hiyo pesa mumchukue huyo Awesu. Mbona Kibu mlimpa pesa nyingi na bado akazingua?