Tujenge utamaduni wa kuwapa thamani wachezaji wazawa

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Kuna haka kautamaduni tunako waswahili ka kuwachukulia poa sana wachezaji wazawa. Inafikia wakati wanalipwa mishahara duni, wakitaka kuuzwa wanauzwa kwa pesa ndogo sana kiasi kwamba hata haitajwi kwa aibu. Nadhani wakati umefika tujenge utamaduni mpya. Embu nisome kidogo...

Huko Uingereza wana utamaduni wa kuwathaminisha wachezaji wao. Wengi wa hawa wachezaji wazawa ndani ya EPL mnaowasifia na kuwaimba ni wachezaji wa kawaida katika level za Ulaya na duniani ila wana thamani kubwa katika soko na wanalipwa mishahara ambayo si haba. Ni utamaduni walioujenga ili isiwepo taswira kuwa wageni tu ndiyo wana thamani.

Ningependa kuona wachezaji wetu wazawa hasa ambao wameonyesha viwango vikubwa vyenye muendelezo aina ya kina Feisal, Bacca, Dickson, Awesu nk. wakithaminishwa. Hili litawaongezea sana soko hata huko nje. Wengine utetezi wetu kwa Feisal ulijikita kwenye hoja hii na si kwa ajili ya kuikomoa Yanga.

Hali ilivyo sasa timu za nje zinamuona mchezaji wetu, wakiangalia rekodi ya mchezaji wanaona kila siku anauzwa na kununuliwa kwa shilingi milioni 15 ikizidi sana 25 na mshahara wa milioni 4 wanamuweka pembeni kumbe anaubonda vizuri tu. Tubadilike. Thaminisha kitu chako ili wengine pia wakithamini.

Simba toeni hiyo pesa mumchukue huyo Awesu. Mbona Kibu mlimpa pesa nyingi na bado akazingua?
 
Thamani ya mchezaji hupatikana uwanjani, siyo mambo ya uzawa.

Uzawa au ugeni hauchezi mpira.

Waka uwanjani, timu zitakuja mezani mzungumze wape gharama zako.
 
Uingereza huwa mnaanza kuwaimba wachezaji kabla hata hawajaonyesha mambo makubwa kisa tu thamani yao sokoni kwa jinsi walivyonunuliwa na kuuzwa. Sisi huku mtu tayari star tena katika timu kubwa ila sasa uliza mshahara wake, uliza mara ya mwisho kanunuliwa kwa bei gani. Ukienda kutaka kumnunua wanakuambia bila bilioni 2 aendi popote ila wao wanamlipa mshahara milioni 5. Hesabu hizi hazihesabiki.

Unajua hii itasaidia hata vilabu vidogo vikue kiuchumi, siyo kila siku unaenda ASEC uko radhi kutoa dola 100K na unaona umependelewa ila ukiona mchezaji mzuri Mashujaa unataka upewe bure.
 
Kuna haka kautamaduni tunako waswahili ka kuwachukulia poa sana wachezaji wazawa. Inafikia wakati wanalipwa mishahara duni, wakitaka kuuzwa wanauzwa kwa pesa ndogo sana kiasi kwamba hata haitajwi kwa aibu. Nadhani wakati umefika tujenge utamaduni mpya. Embu nisome kidogo...

Huko Uingereza wana utamaduni wa kuwathaminisha wachezaji wao. Wengi wa hawa wachezaji wazawa ndani ya EPL mnaowasifia na kuwaimba ni wachezaji wa kawaida katika level za Ulaya na duniani ila wana thamani kubwa katika soko na wanalipwa mishahara ambayo si haba. Ni utamaduni walioujenga ili isiwepo taswira kuwa wageni tu ndiyo wana thamani.

Ningependa kuona wachezaji wetu wazawa hasa ambao wameonyesha viwango vikubwa vyenye muendelezo aina ya kina Feisal, Bacca, Dickson, Awesu nk. wakithaminishwa. Hili litawaongezea sana soko hata huko nje. Wengine utetezi wetu kwa Feisal ulijikita kwenye hoja hii na si kwa ajili ya kuikomoa Yanga.

Hali ilivyo sasa timu za nje zinamuona mchezaji wetu, wakiangalia rekodi ya mchezaji wanaona kila siku anauzwa na kununuliwa kwa shilingi milioni 15 ikizidi sana 25 na mshahara wa milioni 4 wanamuweka pembeni kumbe anaubonda vizuri tu. Tubadilike. Thaminisha kitu chako ili wengine pia wakithamini.

Simba toeni hiyo pesa mumchukue huyo Awesu. Mbona Kibu mlimpa pesa nyingi na bado akazingua?
Je kama hawajitumi na hawapendi kujifunza,(individual skills)
 
Thamani zipo tu sema wachezaji wetu waache bangi,,
Mchezaji Kama Ibrahim Ajibu, angekuwa na thamani kubwa. Angekuwa ananunuliwa hata kwa 500M.na Mshahara wa siyo chini 15M lakini kachagua upumbavu.

Juzi kaenda Dodoma Jiji, signing fee milioni 20🤣🤣🤣

Imagine, kina Kibu, Babacar sarr Freddy, Mukwala Wana thamani kubwa yeye kwa upumbavu wake
 
Attachments

  • Technician mwenzangu Ibrahim Ajibu.@ibrahimajibu23.mp4
    658 KB
Nafikiri wengi hawajajua thamani ya vipaji vyao bado and kurizika wengi ndio kunawaangusha,magazeti na waandishi uchwara wakiwapamba kidogo kichwa kinawavimba,nidhamu mbovu kabisa hasa hawa wanaotoka mijini Dar ndio hovyo kabisa kinidhamu
 
Wengi hamjaelewa ninachosema nimeona hata uvivu kuwajibu mmoja mmoja maana wote mmejibu kitu kile kile. Nimewapa mfano perfect wa Uingereza jinsi wanavyothaminishwa wachezaji wao wakiwa baaado wanakuja.

Ndiyo nidhamu ni muhimu, ndiyo muendelezo wa unachoonyesha uwanjani ni muhimu. Basi tuanze kujenga huo utamaduni kwa hao walioonyesha nidhamu na muendelezo.

Mimi kipindi kile cha mgogoro wa Feisal na Yanga nilisema Feisal kwa kile ambacho alikuwa ameshafanya uwanjani alikuwa anatakiwa awe anakimbizana na kina Diamond kimapato badala yake kumbe analishwa ugali na sukari.
 
Hujui tu, Tanzania si wacheza mpira tu. Michezo mingi, wakishapata umaarufu, jina wanatembelea hilo. Wanasahau walipata hayo yote sababu ya huo mchezo.

Huwezi mpa thamani mchezaji, sababu tu ni wa ndani na hajitumi. Angalia wachezaji wengi, wanaotoka nje. Wanacheza kama mashine, wanajua wakishuka kiwango wanaachwa. Ila wachezaji wetu wa ndani, anajua akitoka simba ataenda Yanga.
 
Uingereza huwa mnaanza kuwaimba wachezaji kabla hata hawajaonyesha mambo makubwa kisa tu thamani yao sokoni kwa jinsi walivyonunuliwa na kuuzwa. Sisi huku mtu tayari star tena katika timu kubwa ila sasa uliza mshahara wake, uliza mara ya mwisho kanunuliwa kwa bei gani. Ukienda kutaka kumnunua wanakuambia bila bilioni 2 aendi popote ila wao wanamlipa mshahara milioni 5. Hesabu hizi hazihesabiki.

Unajua hii itasaidia hata vilabu vidogo vikue kiuchumi, siyo kila siku unaenda ASEC uko radhi kutoa dola 100K na unaona umependelewa ila ukiona mchezaji mzuri Mashujaa unataka upewe bure.
Ndio maana wengi wao hawakui ukianzia kwa Delle Alli,Walcott, Chamberlain nk wengineo wengi mishahara mikubwa ila baada ya misimu michache wanapotea, njoo tena kwa Maguire,Andy Caroll (sijui yupo wapi nae) nk.Nenda Spain wale Zubimendi,William,Yamal nk wanakula mizigo ya kawaida ila kawaangalie uwanjani wanavyo kiwasha.

Mchezaji alipwe kutokana na uwezo wake na si huruma ya Uzawa,kwani hatugawi vitambulisho vya taifa.
 
Umeongelea jambo ambalo huwa linanikera sana na ndio moja wapo ya sababu kwanini hata huwa silichukulii serious soka la bongo.

Hii kasumba ya kuwatukuza wageni wa kuwachukulia poa wazawa huwa inaudhi sana kwakweli... kwanza hata hao wachezaji wa kigeni wenyewe huwa wanatushangaa mno kwa huu ulimbukeni tulionao.

Mchezaji wa kigeni akifika hapa hata kabla hajaanza kuonesha makeke yote uwanjani yaani atapambwa,atasifiwa na kuitwa majina yote kuashiria kwamba yeye ni mchezaji mahiri.

Yaani mchezaji anatoka huko kwao unakuta hata hajulikani ila akishatua tu hapa bongo anakuwa bonge la superstar, sio wasemaji wa club, sio mashabiki, media zetu ndio usiseme yaani inakuwa ni mwendo wa kumuimba yeye tu na wakati mwingine unakuta wala hata hana kiwango cha kutisha, na unakuta kuna wachezaji kibao tu wazawa wanamzidi uwezo.

Kuna mwaka fulani alikuja dogo mmoja kutoka Angola anaitwa sijui Carinhos.. haloo hayo mapokezi yake tu kwanza watu wakaenda Airport kumpokea wakambebelea juu juu kama watumwa walivyokuwa wakimbeba Sultan enzi zile za utumwa, hatujakaa sawa mara akaanza kushobokewa na akina Wema Sepetu... haya sasa alichokuwa anakifanya uwanjani huyo superstar Carinhos yaani ovyoo hata akiendani na hypes alizokuwa anapewa.

Ipo haja ya watanzania kubadili fikra zao kuhusu hizo shobo zao kwa wageni... mimi nikiangaliaga hawa wachezaji wa kigeni naona wengi tu hawana maajabu ila ndio hivyo sababu wametokea sijui Ivory Coast au ghana basi ndio wanakula mishaara mikubwa ya bure plus malaya wa kibongo kujirahisisha kwao.
 
Wengi hamjaelewa ninachosema nimeona hata uvivu kuwajibu mmoja mmoja maana wote mmejibu kitu kile kile. Nimewapa mfano perfect wa Uingereza jinsi wanavyothaminishwa wachezaji wao wakiwa baaado wanakuja.

Ndiyo nidhamu ni muhimu, ndiyo muendelezo wa unachoonyesha uwanjani ni muhimu. Basi tuanzekujenga huo utamaduni kwa hao walioonyesha nidhamu na muendelezo.

Mimi kipindi kile cha mgogoro wa Feisal na Yanga nilisema Feisal kwa kile ambacho alikuwa ameshafanya uwanjani alikuwa anatakiwa awe anakimbizana na kina Diamond kimapato badala yake kumbe analishwa ugali na sukari.
Kaka wabongo hawawezi kukuelewa hapa hata uongee vipi, hii kasumba imeshaota mizizi...

Niamini mimi huyo Aziz ki angekuwa ni mzawa(na uwezo wake alionao huu huu) wala hata asingepewa hypes anazopewa sasa hivi na hata hao akina hamisa mubetto wasingekuwa na muda wa kumshobokea, kiufupi angechukuliwa poa tu kama wanavyochukuliwa akina Feisal.... mtanzania ndio mtu pekee duniani anayeona ufahari kumthamini mgeni na kumpuuza mzawa mwenzake, na hii sio kwenye michezo tu hata kwenye sekta nyingine zote hali ni hivyo hivyo... nenda pale Airport ujionee wale wadada wanavyotabasamu tabasamu ovyo na kujifanya wakarimu wakiwa wanamuhudumia raia wa kigeni, ila ifike zamu yako wewe sasa mbongo mwenzao unaweza hata ukajuta kwanini umeenda pale kwa jinsi watakavyokupa huduma mbovu halafu hata hawajali.

Majuzi hapa Aucho(mganda) aliwachana wabongo wapunguze kuwa idiolize wachezaji wa kigeni na kuwapa support wazawa, cha kushangaza kuna watu walimkosoa, aisee mpaka nikahisi au kuna mtu labda alituroga leo hii tunaikumbatia hii kasumba ya kishenzi na hatutaki kuiachia.

Naona hapa watu wanasema eti wachezaji wazawa hawajitumii mara sijui wanalewa na usuperstar... kwani hilo ni suala jipya? Mbona hata hao wageni mbona nao tunaona kuna wanalewa sifa na tena wanaota mpaka viburi na kuanza kuvimbiana na makocha? Mfano mzuri Chama huyo hapo.

Umeongelea uingereza kuwathamini wachezaji wao wazawa licha ya wachezaji hao mara nyingi kuwa na uwezo wa kawaida... well, Decane Rice huyo hapo katua Arsenal kwa dau la £100m+ na endapo angekuwa anatoka taifa lingine tofauti na England dau lake lisingezidi £30m... ila kwa sababu anatoka taifa linalothamini vipaji vyake ndio maana dau lake sokoni ni 100+

Sasa tukitumia mfano huu huu wa wachezaji wa England unakuja kuona hawa wabongo wanaosena eti wachezaji weu wazawa uwezo wao ni wa kawaida sijui hawajitumii ndio maana hawathaminiwi sawa na wageni, hoja yao haina mashiko hata kidogo na ni ya kipuuzi.

Watu kama Mohamed Hussein Tshabalala wamekuwa na consistency ya hali ya juu miaka nenda miaka rudi hata hao wachezaji wao wa kigeni wanaowaletaga kwa mapesa mengi wameshindwa kumtoa kwenye namba yake... ila huwezi kuskia anaimbwa sana na mashabiki au medias.

Watanganyika wako na shida sana kwa aina ya ufikiri waliyonayo.... ulimbukeni ni mwingi sana na kujipendekeza pendekeza ndio wanachokiweza
 
Mpira sio ngono, wafanye vizuri thamani yao itaonekana kiwanjani!.... Usilazimishe kila mtu apewe thamani asiyonayo. Ukute hapo umevaa amerikani jeans... Kwanini usiwmde kununua vitenge vya mwatex ukashon suruali!.
 
Labda utoe mfano mwingine siyo Feitoto huyu hana body language nzuri,(how do you support him),
 
Umeongelea jambo ambalo huwa linanikera sana na ndio moja wapo ya sababu kwanini hata huwa silichukulii serious soka la bongo.

Hii kasumba ya kuwatukuza wageni wa kuwachukulia poa wazawa huwa inaudhi sana kwakweli... kwanza hata hao wachezaji wa kigeni wenyewe huwa wanatushangaa mno kwa huu ulimbukeni tulionao.

Mchezaji wa kigeni akifika hapa hata kabla hajaanza kuonesha makeke yote uwanjani yaani atapambwa,atasifiwa na kuitwa majina yote kuashiria kwamba yeye ni mchezaji mahiri.

Yaani mchezaji anatoka huko kwao unakuta hata hajulikani ila akishatua tu hapa bongo anakuwa bonge la superstar, sio wasemaji wa club, sio mashabiki, media zetu ndio usiseme yaani inakuwa ni mwendo wa kumuimba yeye tu na wakati mwingine unakuta wala hata hana kiwango cha kutisha, na unakuta kuna wachezaji kibao tu wazawa wanamzidi uwezo.

Kuna mwaka fulani alikuja dogo mmoja kutoka Angola anaitwa sijui Carinhos.. haloo hayo mapokezi yake tu kwanza watu wakaenda Airport kumpokea wakambebelea juu juu kama watumwa walivyokuwa wakimbeba Sultan enzi zile za utumwa, hatujakaa sawa mara akaanza kushobokewa na akina Wema Sepetu... haya sasa alichokuwa anakifanya uwanjani huyo superstar Carinhos yaani ovyoo hata akiendani na hypes alizokuwa anapewa.

Ipo haja ya watanzania kubadili fikra zao kuhusu hizo shobo zao kwa wageni... mimi nikiangaliaga hawa wachezaji wa kigeni naona wengi tu hawana maajabu ila ndio hivyo sababu wametokea sijui Ivory Coast au ghana basi ndio wanakula mishaara mikubwa ya bure plus malaya wa kibongo kujirahisisha kwao.

Kaka wabongo hawawezi kukuelewa hapa hata uongee vipi, hii kasumba imeshaota mizizi...

Niamini mimi huyo Aziz ki angekuwa ni mzawa(na uwezo wake alionao huu huu) wala hata asingepewa hypes anazopewa sasa hivi na hata hao akina hamisa mubetto wasingekuwa na muda wa kumshobokea, kiufupi angechukuliwa poa tu kama wanavyochukuliwa akina Feisal.... mtanzania ndio mtu pekee duniani anayeona ufahari kumthamini mgeni na kumpuuza mzawa mwenzake, na hii sio kwenye michezo tu hata kwenye sekta nyingine zote hali ni hivyo hivyo... nenda pale Airport ujionee wale wadada wanavyotabasamu tabasamu ovyo na kujifanya wakarimu wakiwa wanamuhudumia raia wa kigeni, ila ifike zamu yako wewe sasa mbongo mwenzao unaweza hata ukajuta kwanini umeenda pale kwa jinsi watakavyokupa huduma mbovu halafu hata hawajali.

Majuzi hapa Aucho(mganda) aliwachana wabongo wapunguze kuwa idiolize wachezaji wa kigeni na kuwapa support wazawa, cha kushangaza kuna watu walimkosoa, aisee mpaka nikahisi au kuna mtu labda alituroga leo hii tunaikumbatia hii kasumba ya kishenzi na hatutaki kuiachia.

Naona hapa watu wanasema eti wachezaji wazawa hawajitumii mara sijui wanalewa na usuperstar... kwani hilo ni suala jipya? Mbona hata hao wageni mbona nao tunaona kuna wanalewa sifa na tena wanaota mpaka viburi na kuanza kuvimbiana na makocha? Mfano mzuri Chama huyo hapo.

Umeongelea uingereza kuwathamini wachezaji wao wazawa licha ya wachezaji hao mara nyingi kuwa na uwezo wa kawaida... well, Decane Rice huyo hapo katua Arsenal kwa dau la £100m+ na endapo angekuwa anatoka taifa lingine tofauti na England dau lake lisingezidi £30m... ila kwa sababu anatoka taifa linalothamini vipaji vyake ndio maana dau lake sokoni ni 100+

Sasa tukitumia mfano huu huu wa wachezaji wa England unakuja kuona hawa wabongo wanaosena eti wachezaji weu wazawa uwezo wao ni wa kawaida sijui hawajitumii ndio maana hawathaminiwi sawa na wageni, hoja yao haina mashiko hata kidogo na ni ya kipuuzi.

Watu kama Mohamed Hussein Tshabalala wamekuwa na consistency ya hali ya juu miaka nenda miaka rudi hata hao wachezaji wao wa kigeni wanaowaletaga kwa mapesa mengi wameshindwa kumtoa kwenye namba yake... ila huwezi kuskia anaimbwa sana na mashabiki au medias.

Watanganyika wako na shida sana kwa aina ya ufikiri waliyonayo.... ulimbukeni ni mwingi sana na kujipendekeza pendekeza ndio wanachokiweza
Umefafanua vizuri sana hoja yangu. Inawezekana kabisa chanzo cha hili tatizo ni makuzi majumbani mwetu. Wazazi wetu walituzoeza kuthamini sana wageni. Mgeni akiwatembelea, wazazi watakuwa radhi hata muishi kwa taabu ili yule mgeni alale vizuri na ale vizuri hata ikibidi kuzidi nyie watoto wake.

Badala ya hii tabia kuwa jambo jema katika kujenga ustaarabu wa Mtanzania limegeuka kuwa ni tatizo maana tunashindwa kubalance shobo. Kama ulivyosema lipo kila mahali katika jamii yetu.
 
Umenikumbusha zamani tulivyokuwa wadogo, mgeni akitutembelea nyumbani siku hiyo lazima achinjiwe kuku hata kama nyumbani hamfugi kuku basi mzazi ataenda hata kukopa pesa amnunue huyo kuku, kikubwa tu mgeni ale vizuri na aondoke huku amefurahi...

Unachosema ni kweli kabisa hii kasumba imeanzia kwenye malezi... na sasa imeshakomaa mpaka imetufanya tumekuwa wapuuzi na watu wakujipendekeza pendekeza ovyoo.

Leo hii wewe na muhindi mkienda pale Kurasini kushughulikia suala la passport, huyo muhundi anaweza asichukue hata siku tatu akawa akapewa passport yake, ila wewe mbongo halisi unaweza ukazungushwa hata miezi mitatu... inaudhi kwakweli hii kasumba.

Ukienda taifa kam Misri au Morocco huko kwenye ligi hata ufunge goli 100 kama wewe sio mzawa hakuna media yoyote itakayokuimba.. Mayele huyo hapa huwa analalamika pamoja na kuwa yeye ni striker tegemeo wa Pyramid na anafunga sana, lakin hapewi ile King treatment aliyokuwa anapewa hapa Bongo. Kiufupi huko wanamuona ni mtu wa kawaida sana.

Binafsi huwa kuna muda nachukia hata kuzaliwa kwenye hili taifa, maana huwa naona ni kama aina fulani ya laana yaani kuzaliwa Tanzania ni moja wapo ya adhabu ambayo Mungu amekupa... Mungu kama anakupenda basi ungezaliwa kwenye mataifa yanayoeleweka na sio hili
 
Back
Top Bottom