Tujiandae kisaikolojia: Kama itathibitika pasi na shaka kuwa CHADEMA ilitumia ruzuku kinyume na sheria, Msajili atakifuta

Mbona huko mbali, waifute cdm hata leo. Wananchi walishaamka na haiwataki ccm. Hata zitumike mbinu chafu kiasi gani, lakini tumeshaamka. CCM ni chama cha kizazi kilichopita, kizazi hiki sio cha ccm tena.
Acha kuwasingizia wananchi.Mwenyekiti wa CCM Dr Magufuli anasimamishwa na wananchi kwenye misafara yake. Wananchi wanalia kwa furaha wengine wanazimia.
Wewe unasema nini?
 
Mimi nashauri CCM au chombo chochote cha Dola kisiogope kusafisha Chama Chochote kwa kuogopa wanaofaidika.

Chadema wa kweli hawana kelele kwa chama kuwa safi, wanao pigania chama kisiguswe ni wale tuu wanao faidi mapato ya chama.
 
Acha kuwasingizia wananchi.Mwenyekiti wa CCM dr Magufuli anasimamishwa na wananchi kwenye misafara yake. Wananchi wanalia kwa furaha wengine wanazimia.
Wewe nyumbu unasema nini?

Hata Mugabe, Idd Amin, Elbashir pia walikuwa wanaandaa hayo maigizo ya kusimamishwa na wananchi. Ninavyojua mimi kwa ule ulinzi na msafara wa vile, huwezi kusimamisha msafara wa rais bila kupanga hilo agizo, maana utaishia kupigwa risasi za hatari. Karne ya 21 bado mnatumia mbinu za kuhadaa umma kuwa msafara wa rais umesimamishwa na wananchi? Bado mnadhani watu wana mawazo ya kizee hivyo? Yaani mnaandaa propaganda kisha mnaziamini wenyewe! Hiyo inaitwa kujitekenya na kucheka wenyewe.
 
Kwani Albashir, Mugabe hawakuwa na uliinzi ?kwani watanzania wakiamua kumvamia pale pamoja na walinzi waliopo watashindwa?

Uwezo wa kumvamia wanao sema hawawezi kwa kuwa wanampenda na wanamkubali Rais wao mchapakazi.
 
Sawa tu nchi hii si ni yao ...wao ndiyo watunga watunga sheria na ndiyo wao hao hao watafasiri sheria.

After all itasaidia kuwapunguzia kazi maana si wanataka chama kibakie CCM na mapamdikizi yake.
 

Hata Mugabe na Elbashir walikaa madarakani miaka 30+ kwa kujifanya wananchi wanawapenda, na wao walikuwa wanashinda uchaguzi kama wanavyoshinda uchaguzi ccm sasa hivi. Ilipofika siku ya siku wananchi wakaona imetosha.
 
CUF waliingiza ruzuku kwenye akaunti binafsi..hii mijitu inajidai imesoma ila ovyo kabisa zero IQ
 
Mataahira ina maana mmekosa mbinu za kukiua hicho chama?
 
Woga wa nini kiasi hiki? Majidai yote yale ya ndege, madaraja, SGR na Leo mmeweza kushusha bei ya mafuta duniani (sina mbavu mie) badala ya ku relax mnahangaika na Chadema? Chama kilichojifia baada ya kuwachukua wabunge wake "maarufu sana"?

Your browser is not able to display this video.
 
Mimi nadhani mngekuwa na busara mngehangaika kutatua kero za wananchi ili kuondoa fikra za mabadiliko. Leo mkiiua Chadema kesho kitaibuka chama kingine, upinzani upo kwenye mioyo ya watu na sio kwenye chama.
Watu wataingia mitaani kama US wanavyofanya bila chama chochote.

Au kama mabadiliko ya Mashariki ya Kati.
 
johnthebaptist,

Fat chance!!!
Mis appropriation of public funds ni criminal na si kufuta chama.
Anayehusika inabidi anafunguliwa mashtaka.
Chama kina kosa gani?
Tuwe logical!!
Kuna ishu inayohusisha vitu viwili hapo. Kuna criminal na ishu ya chama kama sheria ya vyama vya siasa inavyosema. Kwa hiyo kuna chama kufutwa na wahusika kuburutwa mahakamani.
 


Yaani watu wa system mnashinda mitandaoni kuandika utumbo wakati mnalipwa na serikali/wananchi. CAG Kazi yake ni nini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…