Tujifunze kutafakari: Aliyekimbia toka Kigoma alitumiaje siku 22 umbali wa 1400KM?

Tujifunze kutafakari: Aliyekimbia toka Kigoma alitumiaje siku 22 umbali wa 1400KM?

Hivi nyie mnapoambiwa watu wa Kigoma siyo wa mchezo mchezo,huwa mnaelewaje?

Ukiachana na watu wa Kigoma kuna Wasukuma nao ni balaa tupu.Mwaka 2004 nilishuhudia mashindano ya baiskeli basi kuna jamaa akajitokeza akimbie kwa miguu dhidi ya waendesha baiskeli,yaani jamaa anakimbia kwa miguu lakini bado waendesha baiskeli na speed zao bado aliwaacha nyuma.Hapo mtasemaje?

Tembeeni muone hii dunia ni pana kuliko suruali ya Pepe Kalle.Mambo aliyofanya Mwanamalundi ukiambiwa tu unachoka kabisa (na mengi ya hayo ushahidi wake upo) itakuwa hilo la 'mtu wa Kigoma' kukimbia kwa miguu Kigoma - Dar?Mbona hili ni jambo dogo sana kwa wale 'wenye uwezo wao'!
 
Kila siku tunatafuta wanariadha wa kwenda kutuwakilisha Olympic hatupati halafu kuna mpumbafu mmoja anajifanya kutoka alikotoka kwa siku kadhaa kuja kuangalia tu mpira
 
Siku nyingne atakayejitolea kukimbia huo umbali awe na application ya simu ya kukimbia ili tujue ukwel.
 
TAFAKARI YANGU
Sijawahi kwenda Kigoma niliishia Tabora inawezekana ikawa jamaa kweli alikimbia kwasababu wewe umepiga Kilomita za Tanroads
Sasa kumbuka kuna Shortcut na barabara zetu nyingi zinazunguka sana mfano ukitoka Dar ukienda Tanga ukiwa unakimbia huwezi kupitia wami kitakuwa kuna njia za kati kati huko utakuta amekata nusu Jamaa badala ya ya km 450 ataenda hata 280Km haya ni tafakuri yangu
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Umbali wa kutoka kigoma kwenda Dar ni almost 1400KM

Ili ufanikiwe kutoka kigoma kwa kukimbia inabidi at most ukimbie kwa Speed ya 5km/hr ili kumaintain stability na pumzi!
Kwa maana hiyo, ili kupata mda sahihi ukichukua umbali 1400 gawa kwa mwendo 5 utapata majibu ya 280 ambayo ni idadi ya masaa kwa umbali huo mfululizo NON STOP ( Yaani hakuna kukojoa wala kula)

Masaa 280 ukichukulia alikimbia mchana NON STOP 12 Hours maana yake (280/12) ni sawa na siku 23 na masaa mawili (23.3) NON STOP

Hivyo basi, speed ya 5Km/hr kwa masaa 12 mfululizo bila kupumzika, bila kukojoa,Bila kula na kunywa, bila kuchimba dawa yaani kila sekunde na hatua, tunatarajia mtu angetumia siku 23.3 (JAMBO AMBALO HALIWEZEKANI BINADAM Kukimbia 12hrs bila kusimama)

Kama kwa gari tu ni ngumu kukimbia 12hrs pasipo kuchimba sawa, iweje kwa mkimbia kwa mguu?

Huyu jamaa kawezaje kukimbia kwa siku 22 kutoka Kigoma hadi Dar wakati kiuhalisia 12hrs NON STOP ni siku 23?

Ina maana huyo jamaa alikatiza misitu ya hatari huko nyakanazi, na kupandisha mirima pasipo KUSIMAMA 12 hours Kila siku Hadi atangazwe katumia siku 22?

Tunaambiwa alianza safari tarehe 15 April mchana, na kufika Dar tarehe 7 may ! Amewezaje kutumia mda huo ambao ni mchache zaidi ya uhalisia?

JE, hakusimama kula, kuchimba dawa, kukojoa wala n.k
Mbona sayansi inagoma?
AU NDO TUAMINI ULE MSEMO kuwa alikimbia mijini, inje ya mji alidandia maroli?
Au hii hesabu ikoje?View attachment 1782115View attachment 1782116View attachment 1782117
Mara nyingine kwa miguu unaweza kupita shortcuts ambazo gari haliwezi. Kwa hivyo kama hizo km 1400 unazosema ni za barabara ya gari, kuna uwezekano mkubwa kwa miguu ikawa pungufu kidogo.
 
Wewe unadhani wanateka kifalafal tu, yaani unapita na viazi au mchovu mchovu tu utekwe? Ile Huwa syndicate na unakuwa planned. Mbona magari yanapita kila siku, umesikia yametekwa lini?
Yes hua wanatekwa kifala fala na kupigwa miti kabisa.
 
Wakuu yule jamaa sio lazima afuatishe barabara! Kuna njia za mkato na pia ukumbuke alikuwa peke yake bila mtu mwingine! Sasa kama alikuwa anakula boda boda hyo ni juu yake sie tunajua na tunaamini katumia idadi ya siku hizo kuja Dar kushuhudia UZINDUZI WA KITABU CHA BABU.
 
3,100 MILE RECORD – THE WORLD’S LONGEST RACE

The Self-Transcendence 3100 Mile Race is one of the most extraordinary running events ever. With its 4,989 km it’s the world’s longest running route – and it leads around just one block in New York. Runners can circle the block from 6 a.m. to midnight. German extreme athlete Madhupran Wolfgang Schwerk covered the route in 41 days, 8 hours, 16 minutes and 29 seconds. During this time, he set a total of 74 new world records between 1,400 miles and 5,000 kilometers. On average, Schrenk ran 120 km per day. Plus, he even added a few more rounds after finishing the race to reach the 5,000 km mark.

On average, Schrenk ran 120 km per day (18 hour run per day ,mapumziko masaa sita)
😵
 
Mtoa mada hesabu zako zina walakini mkubwa. Nadhani ulitaka kuonesha kuwa jamaa hawezi kufanya jambo kama lile ilhali BADALA ya kuamini kuwa ni jambo linalowezekana.

Hili ni tatizo kwa sisi waafrika wengi. Tunapenda kukimbilia kwenye kuona jambo fulani haliwezekani na kuanza kulijengea hoja.

1. Sehemu nyingi alipita mchana. Usiku mkali alikuwa akipumzika kwa kuoga, kulala na kula. Mfano Morogoro, Kibaha alipita usiku kwa mujibu wa watu waliomshuhudia. Moro alifika usiku na kupumzika kwa siku nzima kwa ajili ya kupimwa tumbo na kumeza dawa baada ya kugundulika ana typhoid.

2. Mchana aliutumia kukimbia na kutembea kwa masaa zaidi ya 15 kwa siku.

3. Dar-Kigoma ni approx 1200km. Hivyo kwa siku 22 yenye masaa (22x24) = 528. Kwamba alitumia wastani wa saa 1 kwa kila 3km approx. Kwa kuwa hakuwa akikimbia usiku basi inabidi at least tufanye umbali huo mara mbili au tupunguze masaa kwa nusu. Yaani kuna uwezekano alikimbia 6km kwa kila saa moja.
Jambo ambalo ni mwendo wa kawaida kabisa usio na mateso kwa watu wenye mazoezi.

Mimi kila asubuhi hutembea 2.5km kwa dakika 20 tu kulifuata daladala.

Huyo jamaa ni mdau wa marathon kitambo 6km kwa lisaa kwake ni kama kumsukuma mlevi.

2. Mchana aliutumia kukimbia na kutembea kwa masaa zaidi ya 15 kwa siku

HAKIKA HESABU ZAKO HAZINA WALAKINI 😀
 
Kgm Dar kupitia uvinza nguruka kaliua urambo tabora itigi dodoma Moro ni km zisizozidi 1250. Kwa siku 22 ni km 57. Akitembea masaa 10 pekee ni km 5.7 kwa saa au mita 57 kwa dakika. Anatumia masaa 14 kupumzika kula na kulala kidogo. inawezekana kabisa
1620846805752.png

kwa mahesabu ya Google Map mtu anayetembea kwa miguu tu anachukua masaa 291 ukigawa wa 24hrs unapata siku 12 tena kapitia uvinza je Google map ingenyoosha Kazuramimba Tabora, tuseme usiku alale bado angetumia siku 24
 
Umbali wa kutoka kigoma kwenda Dar ni almost 1400KM

Ili ufanikiwe kutoka kigoma kwa kukimbia inabidi at most ukimbie kwa Speed ya 5km/hr ili kumaintain stability na pumzi!
Kwa maana hiyo, ili kupata mda sahihi ukichukua umbali 1400 gawa kwa mwendo 5 utapata majibu ya 280 ambayo ni idadi ya masaa kwa umbali huo mfululizo NON STOP ( Yaani hakuna kukojoa wala kula)

Masaa 280 ukichukulia alikimbia mchana NON STOP 12 Hours maana yake (280/12) ni sawa na siku 23 na masaa mawili (23.3) NON STOP

Hivyo basi, speed ya 5Km/hr kwa masaa 12 mfululizo bila kupumzika, bila kukojoa,Bila kula na kunywa, bila kuchimba dawa yaani kila sekunde na hatua, tunatarajia mtu angetumia siku 23.3 (JAMBO AMBALO HALIWEZEKANI BINADAM Kukimbia 12hrs bila kusimama)

Kama kwa gari tu ni ngumu kukimbia 12hrs pasipo kuchimba sawa, iweje kwa mkimbia kwa mguu?

Huyu jamaa kawezaje kukimbia kwa siku 22 kutoka Kigoma hadi Dar wakati kiuhalisia 12hrs NON STOP ni siku 23?

Ina maana huyo jamaa alikatiza misitu ya hatari huko nyakanazi, na kupandisha mirima pasipo KUSIMAMA 12 hours Kila siku Hadi atangazwe katumia siku 22?

Tunaambiwa alianza safari tarehe 15 April mchana, na kufika Dar tarehe 7 may ! Amewezaje kutumia mda huo ambao ni mchache zaidi ya uhalisia?

JE, hakusimama kula, kuchimba dawa, kukojoa wala n.k
Mbona sayansi inagoma?
AU NDO TUAMINI ULE MSEMO kuwa alikimbia mijini, inje ya mji alidandia maroli?
Au hii hesabu ikoje?
1620847721957.png

dmkali hesabu yako mbona inaniacha njia panda?
Kutoka Kigoma mpaka Dar ni 1400 na siku ina masaa 24 je saa moja kakimbia kilomita ngapi ni 58
1400km / 24hr = 58km je km angekimbia 88km asubuhi saa 12 mpaka usiku wa saa 1 ni masaa 13 ni 107 km
ni siku 13 tu
Huyu jamaa leo hii wamemuingiza katika Historia ya Jengo la Makumbusho ya Taifa ni si Yanga tena mavazi yake yametundikwa pale
 
Back
Top Bottom