Kama Nyerere angelikuwepo wakati wa utawala wa Magufuli wasingeelewana kabisa.
Kwa sababu Nyerere alikua muumini wa Utawala Bora,utawala wa kufuata kaitiba,kuheshimu sheria,miiko ya uongozi,kanuni na taratibu.
Kwa bahati mbaya kabisa Magufuli alikua kinyume kabisa na uongozi unaoheshimu katiba,sheria,miongozo,kanuni na taratibu.
Alikua ni kiongozi anaeendesha nchi hovyohovyo.
Kujenga mabarabara,madaraja,majengo kwa kuumiza watu ni aina ya uongozi uliopingwa na Dunia nzima.
Adolf Hitler,Makaburu wa kusini,jean Bokassa na wengine kama hao walijenga vizuri sana nchi zao lakni walipingwa na Dunia nzima na mmoja wapo aliewapinga watawala wa namna hiyo ni mwalimu Nyerere.
Nyerere aliheshimu Mahakama,bunge ,mabaraza ya madiwani,serikali za mitaa, washauri,wazee,Viongozi wa dini na wataalam,lakini Magufuli yeye alijiheshimu yeye peke yake.
Hakuheshimu Mahakama,bunge,mabaraza ya madiwani,wazee,Viongozi wa dini,washauri na wataalam..
Katika maisha mtu mmoja kukiuka miongozo walioiweka watangulizi wake bila kufuata utaratibu huyo ni mtu wa hovyo kabisa.
Mfano kama unaona sheria Fulani inachelewesha maendeleao,basi fuata taratibu zilezile zilizoiweka sheria hiyo kuiondoa,mfano,tumia bunge kuondoa sheria inayochelewesha maendeleo,sio kuliruka bunge na kujiamlia wewe mwenyewe kufanya jambo Fulani.
Kama jambo Liko mahakamani basi iachie Mahakama ilimalize kisheria.
Na Kuna vitu vingije kwa asili yake havibadilishwi ni kwenda navyo kwa utaratibu huohuo.
Mfano haki ya msingi ya mtu kusikilizwa huwezi ukaifuta lakini Magufuli alikua kinyume na haki hiyo.
Haiwezekani wagombea wote wa ubunge wa vyama vya upinzani wakawa hawajui ama wanakosea kujaza Fomu za ubunge na udiwani.hii imetokea katika utawala wa Magufuli TU hapa Duniani.
Na utashangaa ndani ya wagombea hao Kuna wanasheria wa miaka mingi na wengine wakiwa wabunge wa miaka mingi.
Kiongozi ni yule anaeongoza kwa kufuata matakwa ya anaowaongoza sio kwa matakwa yake.na sauti za anaowaongoza ni kupitia kwa wawakilishi wao yaani wabunge,madiwani,serikali za mitaa na n.k.
Sasa mtu anaamka tu asubuhi anasema kajengeni uwanja wa ndege wa kimataifa chato,nao wanaenda kujenga.
Je mpango huo ulipitishwa na bunge?
Kiongozi asieheshimu katiba na sheria sidhani kama Nyerere angemkubali.
Kama Nyerere aliwapinga wazanzibar kwa kujiunga na OIC peke Yao kwa kutofuata sheria,sijui Magufuli angemshawishi Nini Nyerere kwa kukanyaga katiba.