Tujihoji: Kwa nini hayati Julius Nyerere alitaka taifa letu liwe na Viongozi kama hayati Mkapa na hayati Magufuli na Sio Lowassa au Jakaya?

Kwa ujinga wake wa kutaka kufanya mambo kwa haraka haraka bila hata research amesababisha madeni makubwa
 
Kwa ujinga wake wa kutaka kufanya mambo kwa haraka haraka bila hata research amesababisha madeni makubwa
Ni kweli, ila mimi kama 'devil's advocate' au wakili wa shetani (ni mtu ambaye huuchukua upande wa kinyume katika mjadala au majadiliano, mara nyingi akipinga maoni au mtazamo uliopo. Kazi ya mwakilishi huyu ni kuleta changamoto kwa dhana zilizopo, kuchochea mawazo ya kina au kupima nguvu ya hoja kwa kutoa maoni yanayopingana. Mara nyingi, jukumu hili linachukuliwa kwa lengo la kusaidia katika uchambuzi wa kina wa dhana au kutambua udhaifu wowote katika hoja au ushahidi uliowasilishwa. Ni muhimu kutambua kwamba kuwa "mwakilishi wa shetani" haimaanishi kwamba mtu huyo anasaidia uovu au shetani kwa kweli, bali wanatekeleza jukumu la kuleta mjadala wa kina na tathmini ya maoni tofauti.)

ndiyo hatukatai alikua na mapungufu mengi sana, ila katika mapungufu yake alionyesha nia thabiti ya mwananchi wa chini kabisa kufaidika na rasilimali za nchi ndo maana hata kama alijenga vitu bila kufata utaratibu bado faida yake ingebaki kwa mwananchi wa chini ndo kama hizo ndege, bwawa la umeme, kiwanja, hospitali ya rufaa na mengineyo. Hata kama yalikua nyumbani kwao bado wananchi wote wangevitumia kama ilivoyo hizo reli nk. Tofauti na wengine waliofanya kinyume na kujifaidisha wao pekee yao bila mtu wa chini kuambuli kitu.

Pale Congo Kinshasa, kulikua na mtu anaitwa Mobutu Sese Seko, alikuwa katili balaa na alifuja mali za Congo kisawasawa alitafuna hadi mfupa. Wananchi walio wengi walitamani aondoke, alipopinduliwa miaka ya 90s na Laurent Kabila watu walifurahi lakini baadae walikuja kusema haya "Mobutu aliiba na umma (fork) na baadhi ya makombo yalituangukia sisi walala hoi a.k.a wana wa nchi lakini huyu Kabila anaiba na kijiko, anakomba chote hakuna hata tunachopata sisi wasakatonge!"

Ndo maana narudia kusema 'between two evils choose none" kati ya maovu mawili usichague lolote.

A beggar doesn't choose!
 
Hii ni sawa na Mchj au Padri ambaye hataki maongozi ya Mungu na maneno yake BIBLIA, anajitungia mambo yake na kuamua kufanya apendavyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…