Sijakukoquote kwa ubaya ila kwasabu umetokea kumkubali mtu ambaye na mimi nilimkubali sana tu, ingawa ntakuwa na nyongeza ndogo tu kusaidia kuweka sawa history.
Nimekulia Temeke, Kurasini, nimepata kuwafahamu Inspector na Nature tangu nikiwa primary, Nature shule moja ila alinitangulia madarasa machache mbele, tuliishi mtaa mmoja ila tulitenganishwa na reli, wao upande wa TAZARA kota sisi upande raia-baharini, kabla hata hajaanza rap.
Inspector alikuwa Temeke kama eneo, umbali wa kama nusu saa kutembea kwa mguu kutoka maeneo yetu, ninachokikumbuka na kukijua sabu nilikishuhudia, Temeke ilianza kutambulishwa kibongo flavor na kina Inspector(ie Gangwe Mob), GWM (Kulwa na doto, walikuwa wanaishi kota za uwanja wa Taifa), in reality Inspector nimemfahamu through Nature sabu tulikuwa tunapiga ruti Temeke kupiga free style na kusikilizia opportunities za kuingia studio kwa Inspector, Nature mwenyewe alikuwa anamkubali sana Inspector, baadaye ndio akaja kushirikishwa kwenye Kigetogeto, Maskini jeuri na Mtulize then akahit sana kwa sauti na style yake pia, from there akaja na single zake binafsi.
Mtaa huo huo tulikuwa na vijana wa R&B, B LOVE M(Banana Zoro na mwenzake), wote clan moja, same place for rehearsal and free styles, walihit na wimbo wao wa Nakupenda..!!!)))
In the end Nature alikuja wika zaidi ya wote TMK.
Mpaka mara ya mwisho kukutana naye ana kwa ana aliniambia anajenga maeneo ya Mbagala, nilisikia anaishi huko.