Tujikumbushe enzi za ufalme wa Inspector Haroun

Tujikumbushe enzi za ufalme wa Inspector Haroun

Hivi Masiga alipotelea wapi
Tena Ana ID humu as Alex Masiga
Screenshot_20180423-003129.jpg
 
Nasikia yupo somewhere darisalama wanapaita vicheji, nasikia ana mjengo lakini milango inaangalia nje, sasa sijui ndio mjengo gani😀😀😀😀
 
Sijui kwanini verse zake nyingi anapenda kutaja vyakula vyakula i.e makoronya laini laini
 
Huyu jamaa kipindi kile ndio alikua na michano yenye swager alafu watoto wa temeke walikuaga na maneno yao wanayajua wao tu...

Nakumbuka kuna kipindi alisema wana kamusi yao ya gangwe yenye maneno yao tu, japo inaweza isiwe kweli lakini inaonyesha jinsi gani walivyokua na maneno ya kipekee...
 
Hapana sidhani kama alikua juu zaidi ya Sir Nature, nijuavyo walikua wanashindana na kupigana vijembe mpaka aliposalimu amri na kufanya collabo ya Mzee wa Busara remix.

Jamani i miss Mzee wa Kibla, where is he?
Nature [emoji119][emoji119]... haifai kumuongelea humu kwa ukubwa yani anastahili thread yake binafsi
 
Mwaka 2001 pale Pool Side, Kilimanjaro Hotel enzi hizo, Unique Sisterz walikuwa wanazindua album. Wasanii waalikwa kibao walifanya performance zao. Baadae alikuja kupanda Haruna Kahena peke yake, akapiga bonge la show moja sitasahau mpaka kesho.
Mkuu siku hizi watu wanakosa radha ile ambayo watu wa zamani walikua wanaipata ata show za siku hizi za Piga kelelee na mikono juuu hazina vibe kama vile ilikua kitambo...

Siku hizi watu wanalazimishwa kupenda mziki wakati kitambo watu walikua wanaupenda kwa dhati
 
Huyu jamaa ndio aliyekuwa msanii anayepiga show kali tena akiwa amepiga pamba kali na zilimtoa kabla blue byser hajaja kumfunika. Nakumbuka show zake zile ufukweni akiwa na gangwe gear
Salute
 
Pepo mbaya kishatukumba, ukijichanganya tunakudunda, ni king sapeto nature boniventure na p funk tunapeta, hakuna mfano wa wazimu tulionao vichaa tumechoka.

Mkuu niamini mimi fatilia hilo, nyimbo ya kwanza nature kusikika ni Mtulize ambayo alishirikishwa na Mabaga fresh.

Inawezekana nimechanganya.. siku nyingi sana any way
 
Wadau wengi naona wanabishania nani kaanza kati ya Inspector na Nature lakini mimi naona ni mabishano yasiokua na maana yeyote, kwasababu uzi unamuhusu Inspector acha nimuongelee yeye....

Jamaa Alitoa nyimbo ya kwanza mwaka 1998, 'Mauzauza', akiwa na Luteni Kalama kwenye kundi la Gangwe. ...

Baada ya hapo wakatoa nyingine mwaka 2000 'Mtu Be,' kisha ndio akatoa jiwe la 'Mtoto wa Geti Kali' ndio lilimpa umaarufu mkubwa. Aliutoa wimbo huu peke yake ingawa alikuwa bado yupo kwenye kundi lake....

Album walizotoa Gangwe bob

♤Simulizi La Ufasaha(2001)
♤Nje Ndani (2002)

Pia ikumbukwe jamaa ndio wasanii wa kwanza kua na website hapa bongo..

Gangwe=hardcore
Gangwe_Mobb.jpg


Hii cover ya album yao inanifurahisha na kunisikitisha sana jamaa wamegonga ndala tu na pozi za hatari...

We have to respect them kwakweli wameitoa game mbali sana, ndio maana huwa najisikia vibaya mtu akiwabeza hawa wakongwe wa hili game...
 
Back
Top Bottom