Tujikumbushe kidogo Wakati watu wako shuleni

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] jamani mbonaa hatariiiiii
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Moments kam hiz ndo hunifanya nkumbke shule mambo ya masomo nehiii [emoji1609]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] shule kuna moments unatamani zijirudie yaani
 
Siku iyo mwalimu wa darasa alikua na mood ya kutandika bakora kaja darasani na vipande vya makaratasi na mzigo wa bakora kama kuni, akaanza kuita list moja moja. Ambao hawajaja mstarini jina langu lipo tukapita mbele tukawekwa bakora, ambao hawajafanya usafi kwenye maeneo yao jina langu lipo tukapita mbele tukawekwa bakora, ambao hawakuwepo darsani jana jina langu tukapita mbele bakora, wapiga kelele darasani jina langu lipo bakora, waliokua wanacheza mpira shuleni wakavunja vioo vya madirisha jina langu lipo bakora.. unaambiwa kila list iliyokua inaitwa mbele jina langu lipo. Tangu siku iyo nikaona mambo ya kwenda darasani jau tu nikawa naonekana shule siku za mtiani na siku za mechi tu.
 
Sijui hata nianze na kipi... Ngoja nianze na hiki cha form 4 . Tukiwa mstarini/parede/assembly mstari wa wavulana wa form ni wa mwisho kabisa so kama ni Jumatatu au Jumatano siku zaku kaguliwa usafi, wa nywele, kucha, socks na nembo ya shule huwa wanaanzia madarasa ya chini kuja kumalizia wasichana wa form 4 then wanakuja kwa wavulana wa form 4 so huwa wanapita upande wa kulia kila siku.
Sasa hiyo siku ikatokea tu dharura kwamba kulikuwa na dalili ya mvua kwa hiyo haku kaguwa mwalimu wa zamu peke yake bali na walimu wengine walimsaidia ili mvua isitukute bado tuko mstarini.
Kwa hiyo mwalimu wetu pendwa wa geography (mnoko hatari) akaanza kukagua form 4 boys ila akaanzia upande wa kushoto ambayo siyo kawaida ila alianzia kushoto kutokana na sehemu aliyo kuwa amesimama. Kanifikia mimi kumbe mguu wa kushoto sina socks kaipandisha suruali ya mguu wa kulia akakuta nimevaa socks moja.​
Kwa kifupi siku za inspection mm na rafiki yangu huwa tunapeana socks ya mguu mmoja ambayo wote tunavaa mguu wa kulia, kwa kuwa ndo walimu huwa wanaangalia Sasa siku hiyo baada ya sisi kufumwa zoezi lilianza upya kuanzia form one kukaguliwa miguu yote kama boys wamevaa socks zote. Too bad ni mimi na rafiki yangu ndo tuli kutwa na hii hatia..hizo bakora, adhabu na aibu yake siyo poa...! Maaana unatoka kwenye adhabu unaingia pindi darasa zima lina angua vicheko mwalimu anaacha pindi nakuanza kuponda kuwa nyie ni form 4 wa aina gani??? And mnawa fundisha nini wadogo zenu....????
 
Ma teacher wenyewe tupo humu humu JF sasa tutakuchapa tena
 
πŸ˜‚πŸ˜‚ Mkuu samahani pm sikupati
 
Da wakati hayo yanatukia wenzenu tulikuwa uwandani tunachunga mbuzi kwahiyo elimu tuliyoipata ni kujua tabia za mbuzi tu
 
Daa kunatich mmoja alinidakak nimemkimbia, alinisakag kinyam yule mwamb. Nilishaga wahi kuchapw na matich mbali mbal ila yule mwamb daa vile vibok vyake huw havinitok kichwan na hii huw inaniumiza sana yaan
 
Mahi lavu Lamomy unamkumbuka yule Ticha aliyekuwa anakuchapa fimbo za makalio πŸ˜” dah alikuwa ananipa hasira knoma ndio mana alikuwa na kitambi cha minyoo.
Simkumbuki mimi sijasoma darasa lolote mahi lavu πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…