Zamani enzi za wahenga ma dj walikuwa wakipiga studio unajua kabisa huyu dj fulani walikuwa na their own signature ila siku hizi sijui teknolojia au skillz zimekuwa saturated sana na computer huwezi jua huyu ni nani.
Dj Rankim alias Ramadhan Nyamka alikuwa bonge moja la dj halafu alikuwa ana bonge moja la sauti unaweza ukasema busta rhymes yuko studio. Alikuwa haongei sana ila muziki ndio unaongea halafu ana best scratching na mixing kwa sasa namfananisha na Dj Boat wa Ghana.
Dj JD legend tumpe maua yake kulikuwa hakunaga kipindi kama The cruize East africa radio yaani ikifika saa mbili usiku unaongeza radio sauti unasikiliza mixing za hatari. Halafu yuko vizuri kwenye mic kama hypeman alikuwa akimtaja Salama J. JABIR na couple yao redioni ilinoga sana zaidi hii ya dida na idrisa.
Bony luv legend, Peter more, Dj PQ mtoto wa mwenge tra huyu , Dj Mariz, Dj skills, Majey forshizzle, Venture, Daudi au Mr D silent partner akijiita alikuwa clouds usiku, Nicco track, Dj Ricco wale wazee wa california pale jolly na billicanas, Mulli B, Mr c charles mhamiji mzee wa sebene kulikuwa hakuna kipindi bora clouds kama Afrika Bambataa na tazara club buzuki shrine. Marehemu freddwah nae alikuwa fundi balaa sema hakupenda sana kuendelea, Hata Pfunk enzi hizo coco alikuwa anapewa mashine na bony luv aguse alikuwa ni balaa on 1& 2 . Dj mafuvu, Dj mackay, Dj Ibra kapotea sana siku hizi
Dj joe mfalme huwa namkubali mpaka kesho, Dj shinski, Dj rommy jones sijawahi kumuelewa kabisa sijui sababu ya bia za kontena regent kwa bichuka.
Dj sinyorita, Dj mammie, D ommy, ommy crazy sijawahi kumuelewa kabisa, dj peter nae wazee wa mzalendo wanamjua mdogo wako bonny luv sema bitozi sana. Dj ferouu, kule times yuko producer hermy B nae ni balaa akikamata mashine,
Na madj wengine wote wakali siku hizi platform za kujulikana ziko nyingi shout out kwa madj wa Kitambaa cheupe maana ukiona sehemu inajaza uje kuna vibe, madj wa Juliana, Dj jowzey he is sumn else too