Tujikumbushe ma Dj's walioinyanyua Bongo Fleva

Tujikumbushe ma Dj's walioinyanyua Bongo Fleva

John Dilinga alikua Anabwembwe sana. Dizaini sound effect wimbo unaimba unatoa sauti kama unaingizwa kwenye mtungi aloo. Noma sana.
Sikuhizi radio station zimepoteza mvuto asubuhi mpaka jioni unasikia makelele ya mastori ya hao washkaji wa vijiweni hakuna tena burdan kama zamani.
Unakumbuka Lile shindano la kutafuta dj Bora na mshindi Anaenda US
Akashinda Mully B..ACHA nilikua live mzeiyaaaa
 
Zamani enzi za wahenga ma dj walikuwa wakipiga studio unajua kabisa huyu dj fulani walikuwa na their own signature ila siku hizi sijui teknolojia au skillz zimekuwa saturated sana na computer huwezi jua huyu ni nani.

Dj Rankim alias Ramadhan Nyamka alikuwa bonge moja la dj halafu alikuwa ana bonge moja la sauti unaweza ukasema busta rhymes yuko studio. Alikuwa haongei sana ila muziki ndio unaongea halafu ana best scratching na mixing kwa sasa namfananisha na Dj Boat wa Ghana.

Dj JD legend tumpe maua yake kulikuwa hakunaga kipindi kama The cruize East africa radio yaani ikifika saa mbili usiku unaongeza radio sauti unasikiliza mixing za hatari. Halafu yuko vizuri kwenye mic kama hypeman alikuwa akimtaja Salama J. JABIR na couple yao redioni ilinoga sana zaidi hii ya dida na idrisa.

Bony luv legend, Peter more, Dj PQ mtoto wa mwenge tra huyu , Dj Mariz, Dj skills, Majey forshizzle, Venture, Daudi au Mr D silent partner akijiita alikuwa clouds usiku, Nicco track, Dj Ricco wale wazee wa california pale jolly na billicanas, Mulli B, Mr c charles mhamiji mzee wa sebene kulikuwa hakuna kipindi bora clouds kama Afrika Bambataa na tazara club buzuki shrine. Marehemu freddwah nae alikuwa fundi balaa sema hakupenda sana kuendelea, Hata Pfunk enzi hizo coco alikuwa anapewa mashine na bony luv aguse alikuwa ni balaa on 1& 2 . Dj mafuvu, Dj mackay, Dj Ibra kapotea sana siku hizi

Dj joe mfalme huwa namkubali mpaka kesho, Dj shinski, Dj rommy jones sijawahi kumuelewa kabisa sijui sababu ya bia za kontena regent kwa bichuka.

Dj sinyorita, Dj mammie, D ommy, ommy crazy sijawahi kumuelewa kabisa, dj peter nae wazee wa mzalendo wanamjua mdogo wako bonny luv sema bitozi sana. Dj ferouu, kule times yuko producer hermy B nae ni balaa akikamata mashine,

Na madj wengine wote wakali siku hizi platform za kujulikana ziko nyingi shout out kwa madj wa Kitambaa cheupe maana ukiona sehemu inajaza uje kuna vibe, madj wa Juliana, Dj jowzey he is sumn else too
 
Ulipaswa kuanza na Master T na Mike,wao ndio waasisi wa hilo neno bongo fleva

Pia ulipaswa uwaweke top list hawa DJ's

Boniluv
Nico track
Master T na Mike ni kweli ndio watangazaji waasisi lakini nilifikiri huu uzi ni kwa DJs tu hao ni watangazaji. Sisi wengine tumepita generations za muziki 90s hadi sasa! Djs waliotoa mchango kwa Bongo Fleva kwa kuzipiga redioni na club wapo wengi lakini very top Tanzania ni;-

1) DJ John Dilinga a.k.a DJ JD
2) DJ Steve B a.k.a DJ Skills

Wengine wengi wali copy hawa na hasa DJ JD. JD ndio alianza kumix Bongo fleva redio miaka ya 90s kuanzia DJ show Radio one na baadae akaanzisha kipindi cha The heat ( joto la ijumaa) akiwa na SoS B na baadae tena akaanzisha chake mwenyewe Fleva 120( ladha 120) miaka hiyo hiyo ya 90. Akaja pia na kutamba sana na The Cruiz E.A Radio, John 14- 16 Radio Uhuru na Times FM hiyo mapema 2000s.

Dj Steve B alianza kupiga Bongo Fleva mapema miaka ya 90 akiwa EA Radio ingawa hakusumbua sana hadi alivyoenda Clouds na kujiunga kwenye Dr Beat baadae XXL. Baada ya hapo Tanzania ili ngoma yako ifanye vizuri ilikuwa lazima isikike Clouds fm na Dj Steve B ndio alikuwa top dj wakati huo.

Hii sijagusia Producers kama Boniluv na watangazaji kama Master T na Mike Mhagama. Msingi wa Bongo Fleva umelala hapo.
 
Guru aka producer G lover alikuwaga bilicanass na kina jdilinga nyakati fulani.nimekumbuka Blue palms disco.

Blue palms ilikuwa sehemu moja matata kwa vijana
 
Back
Top Bottom